Dr Shekilango
Senior Member
- Dec 30, 2013
- 192
- 120
Habari ndugu zangu, pole sana na majukumu.
Ni matumaini yangu nitapata msaada hapa kutoka kwenu.
Nafanya kazi katika Kampuni kubwa ya michezo ya bahati nasibu, hivyo basi huwa kuna shifti kama sita hivyo kwa siku na mara nyingi zinakuwa za usiku.
Mfano, naweza kuingia kazini saa mbili usiku natoka saa kumi na moja Alfajiri au naweza kuingia saa nne usiku natoka saa moja Asubuhi. Hivyo shifti zote kadhaa hwa tunatakiwa kulala vizuri ili tuweze kumudu next shift usiku wake tena.
Mimi tatizo langu sipati usingizi kila nikitoka kazini nashindwa kusinzia kabisa na ukiwa kazini si ruhusa kusinzia ni mwiko unaweza kufukuzwa kazi. Sasa nisipolala huwa nalala nikiingia usiku tena yaani next shift tena mapema sana, natishiwa kufukuzwa kazi kwa sababu ya kusinzia kazini.
Tafadhali naomba msaada wenu nifanye nini niwe napata usingizi nalala vya kutosha. Napata tabu sana mimi. Sina msongo wa mawazo nakula vizuri hela ninayo ila usingizi nakosa.
Cha ajabu nikitoka kazini mapema yaani nimeingia shift ya mchana napata usingizi mpaka asubuhi kabisa tatizo linaanza ninapotoka kazini saa moja asubuhi au kumi na moja alfajir!
Nisaidieni tafadhali. Mawazo, ushauri, tiba n.k.