USSR
JF-Expert Member
- Jul 15, 2015
- 12,012
- 28,379
KAMA NILIVYOZUNGUMZA JUZI KUWA MAMBO YAMEBADILIKA SANA, SIO KILA ANAEKUTONGOZA SASAHIVI ANAKUTAKA KIMAPENZI WENGINE WAKO KAZINI
HUYU BINTI ALIKUJA KWANGU MAJUZI NIKAMUOMBEA AKAFUNGULIWA NA BADO YUKO KWENYE MAOMBI YA KUFUNGULIWA KUTOKA KWENYE VIFUNGO MBALIMBALI
ANAANZA KWA KUSIMULIA
Pastor Anni Mimi ni Binti mrembo na msomi, Mimi ni Mtu mwenye kibali sana. Popote nitakapoenda au nitakaa huwa watu wanafurahiwa na uwepo wangu na wengi huwa wanatamani nisiondoke. Kazini kwangu nimekuwa ni Mtu ninaependwa sana na Boss wangu kutokana na ufanyaji kazi wangu. Wazazi wangu wameokoka na ni watu wa kusali sana ila Mimi sijasimama kivile kama wazazi, japo naenda Ibadani nasali ila sometimes nimekuwa nikianguka anguka.
Nimekuwa na mahusiano na vijana kadhaa na nimeachana nao sio kwasababu ya chochote ila ni kwasababu ya maono niliyonayo. Kwa umri wangu huu sihitaji kijana mdogo nataka kijana mkubwa aliyekomaa tufunge Ndoa tujenge familia. Sikutaka tena mambo ya u Boyfriend na kuchezeana.
Pastor ninafanya kazi kwenye kampuni na maranyingi sana huwa nashinda bandarini kwaajili ya kusimamia kazi.
Siku moja nikiwa pale bandarini alitokea Mkaka mkubwa smart sana, ananukia balaa. Kwa muonekano tu alionyesha kuwa ni tajiri sana. Akanisalimia akaniuliza unafanya nini kila siku nakuona huku nikamwambia niko kazini, akasema hata Mimi nina nina fanya biashara na niko kusimamia mizigo yangu. Akaniomba namba akasema nitakupigia tuongee, nikasema sawa.
Sikumtafuta wala hakunitafuta kama wiki mbili hivi. Sasa Siku hiyo ilikuwa ijumaa akanipigia simu kuniomba tuonane. Aliomba usiku akitoka kazini tukutane mahali kwa dinner, nikasema sawa. Sasa siku hiyo nilikuwa na ratiba ya kwenda kanisani ibada ya jioni, hivyo nikaenda kanisani kwenye Ibada nikatoka mida ya saa kumi na mbili na nusu jioni, akanipigia simu uko wapi nikamwambia niko kanisani ndio natoka, akastuka umetoka kanisani tena, nikamjibu ndio nilikuwa Ibadani. Akasema basi nitakutafuta wiki ijayo, nikamwambia ndio nilikuwa najiandaa kuja tuonane akasema hapana next week.
Nilipata mashaka lakini nikapotezea.
Hakunitafuta tena mpaka jumanne, akanipigia akaniuliza leo unaenda kanisani? Nikamwambia hapana. Akasema kama hautaenda basi tuonane jioni. Akaniambia nakuomba sana usiende kanisani, tuonane kwanza nikamwambia sawa. Sijakaa vizuri akanitumia Laki tano kwenye simu akasema huwa sitembei na Cash naomba wewe ndio ulipie gharama zote tutakazo tumia kwa dinner nimekutumia hela, na chagua twende wapi, nikasema sawa. Nikamwambia ninapotaka kwenda, akasema sawa basi tukapanga tukutane huko saa mbili.
Ni Mkaka ambaye anavaa macheni mengi makubwa, na mapete makubwa vidoleni, kiufupi ni Mtu anayejipenda. Nilifika pale hotel akaniambia nishafika nikamuona anashuka kwenye Prado nyeupe mpyaaa, na ana driver na Mtu mwingine kama mlinzi. Kiukweli nilisema moyoni kuwa nimeopoa Dodo kwenye mkorosho. Mimi kutongozwa na tajiri aisee ni bahati.
Basi tukafika tukakaa tunaongea, akaniambia Yeye hana Mke, Mke wake alishakufa, ila anawatoto wanasoma nje ya nchi. Akanionyesha Picha. Akasema Mimi nimekuona nimekupenda nataka uwe mpenzi wangu. Sisemi kwamba nitakuoa leo au kesho ila naomba uwe mpenzi wangu, unisaidie kupunguza stress huko mbeleni basi tutafunga ndoa. Huwezi amini niliitikia pale pale SAWA HAINA SHIDA 😂😂 sikuwa na sababu ya kukataa. Basi tukala tukaongea tukaondoka.
Nilifika nyumbani nikamwambia asante kwa dinner, akanijibu nashukuru Mke wangu na hapohapo akanitumia Million 1 kwenye simu akasema nataka jumapili hii tutoke tena. Naomba ukanunue nguo nzuri, kiatu uende na salon. Napenda mwanamke anaependeza na kunukia. Nikastuka nikasema sawa. Akasema katafute Wig zuri nataka uwe mwanamke wa kisasa. Kiufupi sikulala usiku namuwaza Yeye.
Sio siri nilichanganyikiwa na huyu mwanaume, jamani Jamani yani nilikuwa tayari kulala nae bila shida na nilikuwa tayari hata nihamie kwake hata kesho, kiufupi nilipagawa nae.
Cha ajabu sasa, nilienda nikatoa ile hela nikaenda shopping jamani nilirudi nyumbani sina hata senti, nikajiuliza nimenunua nini mbona vitu vichache hela imeisha? Nilijilaumu sana ila nikasema niache next time nitakuwa makini.
ITAENDELEA