Tafadhali naomba msaada wenu ushauri na tiba nateseka sana

Ukitoka kazini kuja kupumzika hakikisha unakula mihogo ya kutosha, kunde au bajia za kunde kwa wingi na au vitumbua.

Usikose muhogo au kunde.

Hizo ni tiba mbadala za asili kwa kuleta usingizi haraka.
Naona kwa mara ya kwanza sky eclat, unakubaliana na Faiza foxy
 
Anyways sijaoa kibachela tu so nikitoka job ni kulala. Jamaa yangu tunafanya kazi kampuni moja ila analala mpaka naona wivu, nilipomuomba ushauri alinishauri niwe nalewa kabla ya kulala nitumie kilevi au Bangi, na mwisho niligundua alikuwa anatumia bangi analala unaweza kumuiba kabisa akilala saa moja asubuhi saa nane ndo anaamka wakati nimetoa macho tu
ukitoka mzgoni piga show, option #1 mchumba ako , kama huna second option inakuhusu vipusa vipo vingi tu, kama n muoga wa option ya pili bas ultimate option nikupiga selfiee ride
 
Habari ndugu zangu, pole sana na majukumu.

Ni matumaini yangu nitapata msaada hapa kutoka kwenu.

Nafanya kazi katika Kampuni kubwa ya michezo ya bahati Nasibu, hivyo basi uwa kuna shifti kama sita hivyo kwa siku na mara nyingi zinakuwa za usiku.


Mfano,
Naweza kuingia kazini saa mbili usiku natoka saa kumi na moja Alfajir au naweza kuingia saa nne usiku natoka saa moja asubuhi. Hivyo shifti zote kadhaa uwa tunatakiwa kulala vizuri ili tuweze kumdu next shif usiku wake tena.

Mimi tatizo langu sipati usingizi kila nikitoka kazini nashindwa kusinzia kabisa na ukiwa kazini si ruhusa kusinzia ni mwiko unaweza kufukuzwa kazi. Sasa nisipo lala uwa nalala nikiingia usiku tena yaani next shift tena mapema sana, natishiwa kufukuzwa kazi kwa sababu ya kusinzia kazini.

Tafadhali naomba msada wenu nifanye nini niwe napata usingizi nalala vya kutosha!! Napata taabu sana mimi !! Sina msongo wa mawazo nakula vizuri hela ninayo ila usingizi nakosa.

Cha ajabu nikitoka kazini mapema yaani nimeingia shifta ya mchana napata usingizi mpaka asubuhi kabisa tatizo linaanza ninapotoka kazini saa moja asubuhi au kumi na moja alfajir! Nisaidieni tafadhali

Mawazo
Ushauri
Tiba
N.k.
ukifika chumbani vua nguo baki na nguo ya ndani tu mfano: boksa , washa redio kwa sauti ya chini sana fungulia kitu ambacho unapenda kama ni miziki laini au ni kingine. Jifunze kujifunika huku umelalia tumbo. Acha kuwaza chochote enjoy ule mziki huku upo ndani ya shuka lakujifunika na uwe umefunga macho pia umelalia tumbo. Baada ya kama wiki moja hivi utaanza kuwa addicted na hiki kitabia na mwishoni utakuwa unalala vizuri tu. Kumbuka usinywe supu jion, maji mengi au kahawa.
 
Ahsante sana mazoezi nafanya lakini wapi, juzi nimewaza mpaka nikalia machozi kabisa nikijiuliza kwa nini sipati usingizi! Nimejipiga kichwa kwa asira nateseka sana basi tu
Fanya haya yatakusaidia:
1. kama unapoishi pana kelele hama, kama ni kwako waambie kelele kwako ni mwiko usingizi unaathiriwa sana na kelele
2. Ukirudi nyumbani hiyo saa moja au 11 hakikisha chumba chako kina giza yaani hakuna mwanga, ikibidi chukua vitu ziba mlangoni, na dirishani usione mwanga wowote ule itasaidia sana
3. ukiwa kwenye kutafuta usingizi "ACHA KUTUMIA SIMU, LAPTOP, TV" ule mwanga ni LED light ambayo inaathiri sana nerves za macho mpk kwenye ubongo hapo usingizi utausikia kwenye bomba zima simu kabisa ndipo ulale
4.Chumba chako KISIWE NA JOTO KALI SANA mara nyingi joto linapozidi linapunguza sana uwezo wa mtu kulala usingizi mnono

Angalia video hii itakusaidia sana ndugu, pole sana....

 
Back
Top Bottom