Tafadhali msaidie "Mzee Kipara" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tafadhali msaidie "Mzee Kipara"

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by X-PASTER, Sep 7, 2011.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  Sep 7, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Tafadhali msaidie " Mzee Kipara"


  [​IMG]

  Unamfahamu muigizaji mkongwe anayekwenda kwa jina la ‘Mzee Kipara?" Kama jibu ni ndiyo basi soma habari hii.


  Mzee Kipara ambaye jina lake halisi ni Saidi Fundi (pichani) hivi sasa anasumbuliwa na miguu kukosa nguvu, tatizo ambalo endapo atapelekwa hospitali pengine linaweza kupata nafuu kama si kupona kabisa.

  Kampuni ya Global Publishers inayochapisha Magazeti ya Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa, Ijumaa Wikienda na Championi imempa simu ya mkononi msanii huyo mkongwe, ambayo itamsaidia katika mawasiliano na wasamaria wema ambao tunawaomba mumchangie kwa njia yoyote hasa ya M-Pesa.

  Simu hiyo ilikabidhiwa kwa mzee huyo wiki iliyopita na mmoja wa wahariri wa magazeti yetu, Mohammed Kuyunga, Kigogo Mbuyuni jijini Dar anakoishi.

  Kuyunga alisema kuwa kampuni imeguswa na hali aliyonayo Mzee Kipara hivyo kupitia simu hiyo inaamini watu wengi walioguswa na maradhi yake wataweza kumsaidia kwa hali na mali.

  "Hii simu tumempa pamoja na laini yenye namba 0753 92 34 54 ambayo imeunganiswa na huduma ya M-Pesa ili kuwa rahisi kwa watu kuweza kumtumia fedha," alisema Kuyunga.
  Imeandikwa na Mwandishi wa GPL,

  Global Publishers & General Enterprises Ltd
  P. O. Box 7534 Dar es salaam, Tanzania. East Africa
  Tel: +255 22 2773356/57, +255 22 784 888982
  VISIT US:
  www.globalpublisherstz.com

   
 2. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #2
  Sep 7, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,542
  Likes Received: 18,172
  Trophy Points: 280
  Du!, huyu ni wa tangu enzi za RTD na kina Mzee Jongo, Rajabu Hatia, kina viki na Avijawa etc. Hali ya mzee huyu ni uthibitisho wa hali halisi ya siku za jioni kwa wasanii wetu wa zamani.

  Kwa maoni yangu, hayo ni magonjwa ya kiutu uzima ukishavuka 75, matibabu ni relief tuu, hivyo tumsaidieni jamani ili angalau apate hiyo relief!.
   
 3. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #3
  Sep 7, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  pole zake huyu mzee..

  pamoja na kuwa matatizo humfika yeyote but kama tukipata habari kamili za watu
  labda itasaidia kujua makosa kama yapo ya kuyakwepa kwa wengine

  1,je hana watoto?
  2,wako wapi?
  3mke?
  watoto kama wapo aliwasomesha?
  4.huyu mzee yupo dar toka enzi za viwanja vinagawiwa bure au kuuzwa kwa bei poa..
  je alijenga?if nnot why?

  aliacha mke?why?
  aliuza nyumba?why?

  habari kamili ndo ingekuwa ya maana kwa wengine

  tunaona marekani mtu kama mike tyson akitangazwa kafilisika
  unapewa na habari kamili alivyochezea utajiri wa zaidi ya bilioni 300
  unaelewa....nimewahi sikia huyu ,mzee alifanya kazi rtd au trc hivi
  wapo wenzie wako safi tu na walifanya kazi huko huko...so why him?
   
 4. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #4
  Sep 7, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Sasa mkuu, ukiyajuwa yote hayo ndio utamsaidia au utasema kuwa haliyataka mwenyewe?
   
 5. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #5
  Sep 7, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Waislam, msaidieni ndugu yenu.
   
 6. Amyner

  Amyner JF-Expert Member

  #6
  Sep 7, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 2,404
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 145
  <br />
  <br />
  It wasnt so necessary to say that!
   
 7. Amyner

  Amyner JF-Expert Member

  #7
  Sep 7, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 2,404
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 145
  <br />
  <br />
  You have a point tho!
   
 8. M

  MWENDAKULIMA JF-Expert Member

  #8
  Sep 7, 2011
  Joined: Jul 17, 2009
  Messages: 961
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Kwa hiyo dini nyingine tusimsaidie? crap!!
   
 9. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #9
  Sep 7, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,046
  Likes Received: 13,259
  Trophy Points: 280
  Na mimi namalizia kwa kuuliza ina maana kundi la kaole limeshindwa kumpeleka hospital? simshauri ndugu yangu yoyote kujihusisha na huu upumbavu unaoitwa sanaa hapa Bongo, hii ni aibu yaani mpaka simu ya mkononi apewe na Global Pubrishers, oohh! my foot. sichangi hata mimi nina majukumu.
   
 10. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #10
  Sep 7, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,401
  Likes Received: 736
  Trophy Points: 280
  Well said bro.
   
 11. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #11
  Sep 7, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,401
  Likes Received: 736
  Trophy Points: 280
  bora kuumwa ukimwi kuliko udini.
   
 12. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #12
  Sep 7, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Chuki zako zinakufanya uonekane mzee wa miaka mia, wakati ndio kwanza upo 40's.
   
 13. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #13
  Sep 7, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Hizo ni hazina kubwa kwa kukuza sanaa Tanzania.

  Pamoja na kumpa pole nafikiri JMT ina takiwa kutoa msaada mkubwa kwa nguli huyu wa sanaa.
   
 14. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #14
  Sep 7, 2011
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  hiyo simu ina gharama gani? hizo hela walizonunulia hiyo simu si ndio wangempa akajitibu?
   
 15. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #15
  Sep 7, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ....Naona mzee hata wembe wa kusafisha kidevu amekosa masikini...Dah! mbaya sana...
   
 16. N

  Ntambaswala JF-Expert Member

  #16
  Sep 7, 2011
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 255
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mhh..........kitanda chake ni cha ghorofa........mti mweupe.....labda kama kahamia chumba cha watoto kwa urahisi watu kumuona kuliko angekaa chumbani. Maswali ya Boss hapo juu ni muhimu sana kwa kizazi hiki.

  Hajazeeka (kuchoka kivile) nadhani akipata matibabu sahihi anaweza kupona.....naomba tumsaidie ngoja niende hapa Biafra nitume hata msimbazi
   
 17. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #17
  Sep 7, 2011
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,036
  Trophy Points: 280
  Too low for a JF Senior Expert Member .....

  Ubaguzi si kitu kizuri hata kidogo....
   
 18. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #18
  Sep 7, 2011
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,753
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Kuna kipindi nilikuwa namuona pale Maeneo ya Ferry kwenye ile Canteen ya Mangesho... Duuuh!!!
   
 19. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #19
  Sep 7, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,229
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  inawezekana alikuwa fit kiuchumi lakini ktika hali ya kujiuuguza ndio akaishiwa kila kitu. ukiona mtu anafikia hali ya kuomba msaada ujue hali ni baya, haina maana tukiendelea kujadili alivyokuwa zamani alivyotumia keki aliyokuwa nayo. kwa hali iliyomfika sasa, ni muhimu kumsaidia. kumbukeni msaada ni moyo usambe si utajiri.!!!!
   
 20. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #20
  Sep 7, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,798
  Trophy Points: 280
  global publishers wameponza huruma ya watz kumsaidia mzee kipara, wameitafsiri habari kiudaku zaidi. namkumbuka akiwa na p&p co.ltd nijamsaka kwa namba mlotoa, hata hivo kutoa ni moyo wapendwa!!
   
Loading...