Tafadhali Kikwete tangaza hali ya Dharura kwa Jiji la Dar; TUONGOZE KWENYE DHARURA HII!

neno sahihi ni "ilipaswa"
Sisi watu wa Kemondo hatuna neno kupaswa tuna kupashwa. Iwe ni kupaswa kufanya kitu ama kupashwa habari yote ni KUPASHWA tu!
Hakina mama anapashwa arudi na kuja kuangalia makazi yalivyoathirika. Pia sasa mama atoe kauli thabiti na iwe kuntu juu ya makazi ya mabondeni. Pesa ya dharura itolewe viwanja vipimwe na watu hawamishwe haraka toka mabondeni zisiwe tena kauli bila matendo. Mama pia asisahau kuvunja nyumba ambazo zimejengwa kwenye mapito ya maji na kusababisha nyumba za wanyonge kujaa maji. Viwanja vya wazi vyote virudi huu ndio wakati muafaka. Mama rudi utende na kama una nia na 2015 basi hapa ndipo pa kutokea!
 
JK ni dhaifu mno, mwezi uliopita walitukata mishahara na sasa watazidi kukata kushughulikia mafuriko.
 
Lakini yawezekana tunatakiwa kumuonea huruma JK ila tatizo ni kwamba hatuna updates kama watanzania, hata North Korea wameshtukizwa, hawakujua ndiyo masmbo ya ki-komunist hayo tuweni wapole tuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu
 
Namsikiliza mkuu wa mkoa wa dar star tv hapa. Anasema hatuna helikopta za uokozi. Ile inayopita ni ya patrol tu. Jamani miaka 50 ya uhuru ati nchi haina helikopta ya uokozi. Haina boti za uokozi. Tumetumia mabilioni ya shilingi kununua ndege ya raisi, mabilioni mengine sherehe za uhuru, mabilioni mengine ya EPA, mabilioni mengine chenji ya radar etc lakini hatuna mabilioni ya vifaa vya uokozi. What a country with a splendid leadership!

Ndio serikali yenu mlioichagua inazijali sana sherehe kuliko maisha ya watu.
 
hawa wengine wote haijalishi; people need to look at their President. Kama kazi anaona ngumu au anaona ni tatizo la "watu wa mabondeni" basi akae kimya tu wananchi wamesurvive without his leadership and I bet they will survive anyway.

Pinda je! Si ndiyo majukumu yake hayo? Umecheki ratiba yake aliko?! Kama yuko Mpanda akirudi tutamshinikiza ajiuzulu!
 
Baada ya kufanya mazungumzo na watu mbalimbali na hasa baada ya kuona kina na uzito wa tatizo la mafuriko na hasa kwa vile mvua bado zinatarajiwa kunyesha tena Alhamisi, Ijumaa na Jumamosi na kwa vile hali hii itakuwa tata zaidi kuna uwezekano mkubwa sana wa kuvunjika kwa amani na utulivu katika Jiji la Dar kuliko wakati mwingine wowote. Vitu vyote muhimu vya kusababisha uvunjivu viko tayari.

- Shida ya njaa
- Kutafuta nafasi ya kujinufaisha na matatizo ya wengine
- Kushindwa kwa vyombo vya usalama kufika maeneo mbalimbali kwa haraka
- kukosekana kwa uongozi madhubuti na makini.

Nilitarajia tangu jana - Rais angekuwa wa kwanza kulihutubia taifa na hususan watu wa Dar juu ya janga hili na mipango ya serikali kulishughulikia na kuhakikisha usalama na utulivu. Nilitarajia kuwa masaa baada ya 12 kupita na hali kuonekana Rais angeweza kuzungumza na kuonesha uongozi kwa taifa na wakazi wa Dar na mara moja kuinitiate Emergency Protocol chini ya Emergency POwers Act of 1986.

Bahati mbaya masaa 24 yanapita sasa na tunaelekea masaa 36. Umuhimu wa kutangaza Emergency Situation ni kuweza kulazimisha resources mbalimbali kuweza kuanza kutumika (public and private) kwa ajili ya kunusuru kwani baada ya muda tutaona kuwa tatizo linalofuatia ni vitendo vya uporaji, ubakaji na matumizi ya nguvu ili watu wasalimike (natarajia kuanza kuona mambo haya 48 hours baada ya kuanza kwa mafuriko). Najua mojawapo ya matatizo ambayo yatatokea ni kuweza kuharakisha huduma mbalimbali hususan za afya - kwani mazingira ya mlipuko wa homa ya matumbo (typhoid) na kipindupindu (cholera) na Ecoli yako tayari. Na kwa vile hakuna mahali pa kujisaidia kwenye maeneo mengi, hali hii itakuwa ni mbaya sana ikianza hasa kwa watoto.

Ninaamini, kama kuna wakati wowote ambapo Rais Kikwete anahitaji kuonesha uongozi na kuwa yuko ontop of things ni kwenye hili lakini hadi hivi sasa haijatolewa kauli ya Ikulu masaa zaidi ya 24 inanitazia. Tunaweza kuwa na issue ya George Bush na Michael Brown wa FEMA pale alipotembelea wahanga wa Katrina. Sitaki (binafsi najisemea) kusikia ati "Rais ametoa pongezi kwa juhudi za uokoaji" and all the regular B.S kama tulizosikia baada ya Mv. Bukoba na Mv. Spice. Tunataka tuwaone wamekunja mashati na hawalali kuhakakisha Watanzania hawadhuriki kwani tayari wameshawalet down kwenye suala la miundo mbinu ya maji machafu na ya mvua na pia kwenye kusimamia ujenzi sasa tunapovuna walichopanda wasikae pembeni.

Tafadhali Rais Kikwete tangaza hali ya dharura na onesha uongozi saa na wakati huu kwani yawezekana Urais wako utaamuliwa na mengi sana lakini hili laweza kuwa ndio "defining moment". Maana kama wanasema mvua kama hii haijawahi kunyesha kwa miaka zaidi ya 57 jijini Dar manake hata Nyerere hakuwahi kujaribiwa kama unavyojaribiwa wewe - will you rise up and be counted? I hope and pray that you WILL answer this CALL OF HISTORY.

Ukiongoza tutakuunga mkono! Tuambie tufanye nini tusaidie, tuambie tusifanye nini ili kufanya kazi iwe rahisi; tuambie kama watu wanaweza kujitolea kuja kusaidia na waje kufanya nini? WE NEED A LEADER!

mmm

HILI NDILO TAMKO LA IKULU:

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Said Meck Sadiq kuomboleza vifo vya watu 13 ambao wamepoteza maisha katika mafuriko makubwa yaliyotokana na mvua ambazo zimekuwa zinanyesha tokea juzi, Jumanne, Desemba 20, 2011. Aidha, Rais Kikwete amempa pole Mkuu huyo wa Mkoa kutokana na uharibifu mkubwa wa nyumba, makazi na mali nyingine za wananchi uliosababishwa na mvua hizo ambazo pia zimesababisha uharibifu wa miundombinu. Rais Kikwete pia ameuelekeza uongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa kusaidiana na taasisi na vyombo vyenye uzoefu wa maafa kushirikiana katika kuendelea kuokoa maisha ya watu, kusaidia waliozingirwa na mafuriko na kuwahifadhi na kuwasaidia wale wote waliopoteza nyumba na makazi kutokana na mafuriko hayo.

Katika salamu zake, Rais Kikwete amemwambia Mheshimiwa Sadiq: “Nimepokea kwa masikitiko habari za vifo vya wenzetu 13 ilivyotokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa ambayo sote tumeishuhudia katika Mkoa wa Dar es Salaam tokea jana. Amesema: “Nakutumia wewe rambirambi zangu kutokana na vifo hivyo, na kupitia kwako kwa familia, ndugu na jamaa waliopoteza wapendwa wao katika balaa hili la mafuriko. Wajulishe kuwa msiba wao ni msiba wangu, naelewa machungu yao na niko nao katika hali ya sasa ya maombolezo. Mungu aziweke pema peponi roho za marehemu wote.”
Ameongeza Rais Kikwete: “Napenda pia kupitia kwako kutoa pole zangu nyingi kwa wote walioumia ama kupoteza mali zao katika mafuriko haya. Wajulishe kuwa moyo wangu uko nao wakati huu wa mazingira magumu. “Chini ya usimamizi wako, ningependa kuona uongozi wa Mkoa kwa kushirikiana na taasisi na vyombo vyenye ujuzi na uzoefu wa kupambana na majanga na dharura za namna hii, kuhakikisha kuwa tunaendelea kuokoa watu ambao badowamezingirwa na mafuriko, tunawapa matibabu wale walioumia katika mafurikohayo, na tunawahifadhi na kuwapa huduma za kibinadamu wote waliopoteza nyumba na makazi yao katika mafurikio hayo.”

IMETOLEWA NA:
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
DESEMBA 21, 2011
DAR ES SALAAM

My Take:
Sidhani kama Ikulu wameelewa hata kidogo uzito wa mafuriko haya na jinsi ambavyo ifikapo Jumamosi yatakuwa na madhara makubwa kwa watu, mali, na uchumi wa Dar-es-Salaam (kama siyo nchi). Hili si Tatizo la Mkoa kama taarifa ya Ikulu invyoonesha; ni tatizo linalohitaji uongozi wa kitaifa. Kwani vifo vitakuwa vingi kuliko watu wanavyofikiria. Tusije kusikia tu "tulidhania"...

Mkuu mmm umenena maneno mazito sana na yenye hekima ndani yake. Ni kweli kabisa tunahitaji kauli za kinywa na si kauli za kwenye karatasi. Katika hali kama hii ukiwa mwathirika na ikasikia kauli ya mkuu wako akitoa maelekezo ya nini kifanyike basi unapata nguvu na kufarijika lakini kauli ya kwenye karatasi naona haitoi faraja yoyote.
 
Pinda je! Si ndiyo majukumu yake hayo? Umecheki ratiba yake aliko?! Kama yuko Mpanda akirudi tutamshinikiza ajiuzulu!

Waziri Mkuu hana nguvu ya kutangaza hali ya dharura (ndicho kilichomtia Lowassa matatizoni); only the President can. Na katika hili ni rais anahitaji kuonesha kuwa anajali wananchi wake.
 
Lakini yawezekana tunatakiwa kumuonea huruma JK ila tatizo ni kwamba hatuna updates kama watanzania, hata North Korea wameshtukizwa, hawakujua ndiyo masmbo ya ki-komunist hayo tuweni wapole tuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu

mambo ya kikomunisti ndiyo yapi? Kutumia bi.54 kwa sherehe za miaka 50?
 
Sisi watu wa Kemondo hatuna neno kupaswa tuna kupashwa. Iwe ni kupaswa kufanya kitu ama kupashwa habari yote ni KUPASHWA tu!
Hakina mama anapashwa arudi na kuja kuangalia makazi yalivyoathirika. Pia sasa mama atoe kauli thabiti na iwe kuntu juu ya makazi ya mabondeni. Pesa ya dharura itolewe viwanja vipimwe na watu hawamishwe haraka toka mabondeni zisiwe tena kauli bila matendo. Mama pia asisahau kuvunja nyumba ambazo zimejengwa kwenye mapito ya maji na kusababisha nyumba za wanyonge kujaa maji. Viwanja vya wazi vyote virudi huu ndio wakati muafaka. Mama rudi utende na kama una nia na 2015 basi hapa ndipo pa kutokea!

Mkuu Kimbunga, heshima kwako.......ni muhimu kuheshimu na kuienzi lugha yetu........

unapasha habari, unapasha maji, unapasha misuli/msuli

unapaswa kuwajibika, inakupasa ufanye kazi nk...........

Kwa mfano watu wa kutoka Nyarugusu wengi hupenda kutumia neno "nakuaga" badala ya "ninakuwa/nakuwa"......"nakwendaga"......badala ya "nakwenda/ninakwenda".........kwa hiyo na wao tuwaachie tu waendelee kukosea?
 
Rais alikuwa Mara amekatisha ziara yake, na leo mida ya saa 5 asubuhi atembelea maeneo yote yaliopata athari ya mafuriko na atatoa tamko lake kama Rais
 
mara mia waziri wa makazi amejitaidi japo kwa kutuma salamu za pole ingawa yupo Uganda kikazi.
Mi nadhani amethubutu kuonyesha kujali kuliko kaka mkuu wa nchi.

Nchi hii watu hawako serious kweli! Yaani anatuma salamu badala ya kurudi na ndege ya kwanza mara tu aliposikia kwamba makazi.nchini kwake yameathirika! Anamtumia nani salamu huyo? Hajui kwamba wizara yake ina mchango mkubwa katika maafa haya?
 
Rais alikuwa Mara amekatisha ziara yake, na leo mida ya saa 5 asubuhi atembelea maeneo yote yaliopata athari ya mafuriko na atatoa tamko lake kama Rais

Kwa nini ziara ya siri ndiyo mambo tusiyoyataka, yeye tumempa kazi sisi anatakiwa atoe taarifa kuwa yuko wapi na kwa nini je akidhurika nani atalaumiwa, au ndiyo mambo yetu ya Barrick, si mwisho wa mwaka yawezekana migao inatembea
 
Mkuu Kimbunga, heshima kwako.......ni muhimu kuheshimu na kuienzi lugha yetu........

unapasha habari, unapasha maji, unapasha misuli/msuli

unapaswa kuwajibika, inakupasa ufanye kazi nk...........

Kwa mfano watu wa kutoka Nyarugusu wengi hupenda kutumia neno "nakuaga" badala ya "ninakuwa/nakuwa"......"nakwendaga"......badala ya "nakwenda/ninakwenda".........kwa hiyo na wao tuwaachie tu waendelee kukosea?
Mkuu nilikuwa nachagiza tu! Ndio maana nikaonyesha tofauti ya kupaswa kufanya kitu na kupashwa habari! Utatuua bure manake mwishowe utataka tutamke ng'ombe ama ng'ambo badala ya mazoea yetu ya ngombe ama ngambo!
 
Inawezekana labda mheshimiwa anajiandaa na safari ya mazikoni si unajua kuna Taifa limepoteza kiongozi wake? Au ndio unataka kusema hutuwalikishwi kwenye maziko?

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
hawa wengine wote haijalishi; people need to look at their President. Kama kazi anaona ngumu au anaona ni tatizo la "watu wa mabondeni" basi akae kimya tu wananchi wamesurvive without his leadership and I bet they will survive anyway.

Niliuliza hili jana na nilisema binasfi nilitarajia kiongozi mkubwa wa nchi i.e rais au waziri mkuu akae kitako na watu wa hali ya hewa apate taarifa kamili then kwa kushirikiana na kitengo cha maafa ahutubie taifa ili wananchi wajue what to do. Hili halijafanyika.
Sasa ikulu inatoa salamu za pole/rambirambi kwa mkuu wa mkoa! Aibu gani hii ya kutumia akili ya miaka 47 kwamba tatizo linatokea then rais anatuma pole kwa mkuu wa mko? Dar es Salaam, roho ya nchi iko kwenye mafuriko tena ya kihostoria rais anatoa pole kwa maandishi? where is he?
 
Kwa nini ziara ya siri ndiyo mambo tusiyoyataka, yeye tumempa kazi sisi anatakiwa atoe taarifa kuwa yuko wapi na kwa nini je akidhurika nani atalaumiwa, au ndiyo mambo yetu ya Barrick, si mwisho wa mwaka yawezekana migao inatembea
Sio ziara ya siri. JMK ni mbia kwenye hoteli moja kule Serengeti.
 
nchi nyingine vyombo vyote vya habari vingekuwa vinaongelea maafa haya oa kutoa updates,hii ingehamasisha uokoaji,wale wanaokaa mabondeni kuchukua taahadhari nk. Ajabu vyombo vyetu vya habari wanapiga muziki ni aibu.uzalendo utatoka wapi kwa mtanzania wa kawaida?

Khususan hawa wa Clouds TV nadhani uungwana na ubinadamu wao umesombwa na mafuriko pia!Ni heri wazime matangazo yao badala ya kuwawekea muziki watu wanaozama majini.Huu sio wakati wa burudani hata kidogo!
 
Back
Top Bottom