Tafadhali Kikwete tangaza hali ya Dharura kwa Jiji la Dar; TUONGOZE KWENYE DHARURA HII!

Kuna mtu jana nimemsikia kwenye taarifa ya habari sijui ndo anaitwa
kaimu mkuu wa mkoa,ana lalamika watu hawataki kutoka mabondeni ndo maana mafuriko yamewapata.

Haya ni matusi,mimi ninapokaa sio bondeni kihivo kiasi kwamba panahitajia kuhama lakini maji yamejaa kwangu
toka juzi na nimeacha hata kuwaza kuhusu kusafisha au kurudi kukaa pale hadi mvua ziishe.

Tatizo lililo pelekea maji kujaa kwangu sio kuwa bondeni,ila ni mitaro kujaa matope (takribani mwaka mzima ) lakini
hakuna hatua yoyote ile ya serikali kuzibua mitaro hiyo.

Lakini pia,wanasema watu waondoke mabondeni waende wapi?milimani?
kuna milima mingapi dar es salaam?hii ni sababu ya kipuuzi kabisa kama sio uvivu wa kufikiri.

Basi atleast waseme watu wahame "mabondeni" na sehemu salama ni hii na hii kuliko kusema tu hameni
mabondeni bila kwaambia waende wapi.....kwa hali hii tutaombeana mvua inyeshe mwezi mzima ili dar yote
ijae maji ndo tuondoke wote mjini hapa maana wote tuko "mabondeni".

Jana ndo mamlaka ya hari ya hewa inatoa utabiri wake,ili iweje sasa?
kwanini hawakutoa atleast siku moja kabla na kutoa warning kwamba watu waonaodhani wako mabondeni wahame mapeme?
Najua wapo watakao watetea kwamba walitoa utabiri wao miezi mingi ilopita,lakini watu wana sahau,na hata
serikali inasahau na hadi sasa haijakumbuka chochote ingawa watu wanakufa.

Kama utabiri walio toa "mda mrefu" ulopita ulikua na maana basi serikali ingezibua mitaro yooote jijini na sidhani kama kungekua
na kadhia kama iliyopo sasa kwa ukubwa huu.

Tphuuuuuu,sijui nimtepee nani mate.
 
Halafu hii ya leo nadhani haina RADI tu ila inaelekea kuwa kama ya jana

Na radi inakuja - nimeandika toka jana kuwa (masaa zaidi ya 24 yaliyopita) kuwa hii mvua haiishi hadi usiku wa kuamkia Krismasi. Itanyesha Alhamisi, itanyesha Ijumaa na itanyesha Jumamosi na kama watu wanafikiria wameona mafuriko basi hawajaona kitu. Ngoja mgundue watu hawana cha kula, hakuna pa kujisaidia na hapakuna pa kulala - I'm guesstimating kuwa mafuriko yatawaathiri zaidi ya watu milioni 1.5.

Hii ndio sababu ya kutoa wito huu.
 
Nna uhakika kuwa viongozi kadha wa kadha weshawahi kwenda kwenye warsha na makongamano marefu na mafupi nchi za nje kujifunza namna ya kukabiliana na maafa na majanga kama haya. Nna uhakika pia kushafanywa warsha nyengine nyingi mno ndani ya nchi pia.

Kinachosikitika ni kuwa tuna act kama maafa haya ndo kwanza leo kutokea popote pale duniani-kama maajabu ya dunia vile.

Tusema kuwa ni kweli serikali haina uwezo wa kiufundi wa kufanya uokozi au wa kuzuwia kusambaa zaidi kwa maafa hayo, lakini serikali inashindwaje kuweza kuzungumza tu na wananchi wake?

Tuseme hawajui kuwa katika kipindi cha maafa kinachotoa faraja zaidi kwa wote ni ule upatikanaji wa taarifa na kuelewa kuwa watu wote wapo pamoja nawe? Rais, Waziri Mkuu, Mkuu wa Mkoa, Wabunge, mko wapi?
 
Mkuu Mwanakijiji,
Umefanikiwa kuwapata red Cross? na jitihada zipi zaidi zinafanyika.. Ni Asasi zipi zinapatikana kujihusisha na maafa haya maana nataka kuandaa ukusanyaji wa nguo, blanketi na fedha kama tutaweza ili tuweze kuzituma ktk taasisi inayohusika.. naomba sana unipe taarifa hizi kwa sababu itakuwa vizuri kama tutakuwa na info zilizo kamili...
 
yeah,anachosema mwanakijiji ni sahihi,athari itakayowakumba watu si mafuriko tu bali usalama wao pia coz vibaka wanatek advantage,
 
kwa rais wetu hana muda wa kuona majanga ya kitaifa kama haya,
sijui hata hawa wenzetu wa chadema wako wapi na helkopita yao ili waokoe watu,
sijui hata hawa wabunge wetu wako wapi,
sijui hata serikali yetu iko wapi,
kweli tz haina mwenyewe.
 
Nna uhakika kuwa viongozi kadha wa kadha weshawahi kwenda kwenye warsha na makongamano marefu na mafupi nchi za nje kujifunza namna ya kukabiliana na maafa na majanga kama haya. Nna uhakika pia kushafanywa warsha nyengine nyingi mno ndani ya nchi pia.

Kinachosikitika ni kuwa tuna act kama maafa haya ndo kwanza leo kutokea popote pale duniani-kama maajabu ya dunia vile.

Tusema kuwa ni kweli serikali haina uwezo wa kiufundi wa kufanya uokozi au wa kuzuwia kusambaa zaidi kwa maafa hayo, lakini serikali inashindwaje kuweza kuzungumza tu na wananchi wake?

Tuseme hawajui kuwa katika kipindi cha maafa kinachotoa faraja zaidi kwa wote ni ule upatikanaji wa taarifa na kuelewa kuwa watu wote wapo pamoja nawe? Rais, Waziri Mkuu, Mkuu wa Mkoa, Wabunge, mko wapi?

1.Tatizo bajeti ya Disaster Relief watu washakula.
2. Nini Citywide disaster, bongo hatuna utamaduni hata wa fire drill.
3. Nini fire drill, watu hata kuwa na personal fire extinguisher nyumbani kazi
4. Wamenunua mi Land Cruiser ya bei mbaya kibao, FFU mibunduki mibomu na mirungu kibao, vifaa vya kusaidia maafa hamna.

Aibu, aibu, aibu.
 
Insanity is doing the same thing the same way over and over again, and expect a different result! Tunalipa gharama ya ubwabwa na khanga (lowest quality, zishapauka saa hizi!). Tuna kitengo cha maafa na majanga kwenye ofisi ya waziri mkuu, kazi yao ni kumshauri rais juu ya uwepo wa emergency. Ukiwauliza bajeti yao ya miaka 50 ya uhuru unaweza ukazimia! Na hawana hata boya moja!
Tumethubutu, tumewezwa, tunazidi kusonga mbele!
 
Jk na pinda wameshaanza likizo? Wako wapi kwenye matatizo haya yanayotokea dar? Ivi kweli tunaachia uchumi unasimama siku nzima kutokana na mvua ya masaa?65percent ya wafanyakazi hawajaenda maofisini.

Kama idara ya hali ya hewa makini, walikua wapi kuannounce kwenye media zote tuanze kuhama na kusogea? kama viongozi wetu walikua wapi kutoa misaada kama wanajua mvua kubwa ilikua inakuja? Jana usiku naangalia news ni wananchi tu ndo wanahangaika, haya matatizo yalianza tokea saa kumi asubuhi, walikua wapi kurescue watu mpaka saa nane mchana? Kule marekani wanapata matatizo ya hali ya hewa makubwa zaidi, kawaida yao lazima umuone kiongozi wa juu aende kutoa pole na kuwapa moyo kwasababu ni 'natural disaster'. Na binadamu huishi kwa kuangalia viongozi na kupewa moyo, leo hii hawa viongozi sijawaona kokote,wangetaka credibility, wangeenda hata kuwaona waliolala mashuleni, wangeenda kutoa tamko hadharani kwa misaada kuongezeka.

Sifa za lowassa ndo maana mpaka leo zinasimama, kipindi kile nakumbuka aliairisha likizo akaenda na helicopter mkoa wa tanga barabara ilikua imefurika. Leo akipongezwa tunatafuta mchawi wetu. Ivi serikali ina invest kwenye v8 na safari za nnje tu? Haya magari mpaka katibu wa halmashauri anaendeshwa na mapolice, tunashindwa kweli kupata maboya na viboti vidogo, tunashindwa kweli kuita misaada hata miji ya pembeni?tunashindwa kuungana na kuwa kitu kimoja leo tusaidiane. Wazungu wanakwambia 'real leaders are ordinary people with extraordinary determination'huyu yuko determined kufanya lipi kwa lipi?

Xmas na mwaka mpya tunaingia bila umeme, bila mafuta, mafuriko ya hali ya juu na bila uongozi.. Kweli jk bado utasimama na kutuchekea??
 
MM, umesahau athari za kiuchumi. Jana watu wameshindwa kufika maofisini na kwenye shughuli zao za kuwaingizia kipato. This is going to touch everyone!
hawa wengine wote haijalishi; people need to look at their President. Kama kazi anaona ngumu au anaona ni tatizo la "watu wa mabondeni" basi akae kimya tu wananchi wamesurvive without his leadership and I bet they will survive anyway.
 
Atatangaza hali ya dharura saa ngapi wakati yuko Bilila Serengeti anakula Kuku. Hayo ya mafuriko ni juu yenu wananchi wenyewe
 
Haya mafuriko yangetokea huku sumbawanga, hakuna ambaye angeandika thredi. Huwa anapaga hasira sana. Hata EWURA huwa wanatangaza bei za dar tu, na mafuta yakikosekana dar ndo wanahaha. Sisi huku hatuna umeme wala maji, lakin sijaona thredi. Ingekua dar je?
 
Namsikiliza mkuu wa mkoa wa dar star tv hapa. Anasema hatuna helikopta za uokozi. Ile inayopita ni ya patrol tu. Jamani miaka 50 ya uhuru ati nchi haina helikopta ya uokozi. Haina boti za uokozi. Tumetumia mabilioni ya shilingi kununua ndege ya raisi, mabilioni mengine sherehe za uhuru, mabilioni mengine ya EPA, mabilioni mengine chenji ya radar etc lakini hatuna mabilioni ya vifaa vya uokozi. What a country with a splendid leadership!
 
Mwanakijiji mimi niko na wewe kabisa lakini naomba niende mbali zaidi, tangu jumatatu tuymeona coverrage ya habari ya Mama Tibaijuka eti yuko Uganda kwa ziara ya kuwapeleka wapiga kura wake kujifunza namna ya kudhibiti ugonjwa wa mnyauko wa MIGOMBA.Nilijiuliza swali je hii kweli ni kazi yake???? Afisa kilimo wa wilaya atafanya kazi gani sasa.

Halafu jana nilisikitika zaidi baada ya mama Tibaijuka kuhojiwa na TBC akiwa uganda bado, nilitegemea kuwa ANGEKATISHA ZIARA NA KURUDI KUJA KUANGALIA NYUMBA NA MAKAZI YANAVYOHARIBIWA, kwa kweli nilisikitika na kugundua nchi kwa sasa haina viongozi.Huyu mama nimesikia anatafuta kukubalika kwa wakuu wa nchi za EA ili kujiandaa kugombea URAHISI 2015.Watanzania tunahitaji kufanya kitu kujikomboa kwani viongozi hatuna kuanzia mkulu hadi diwani.
Nawasilisha
 
Back
Top Bottom