Tafadhali Kikwete tangaza hali ya Dharura kwa Jiji la Dar; TUONGOZE KWENYE DHARURA HII!

Waziri Mkuu hana nguvu ya kutangaza hali ya dharura (ndicho kilichomtia Lowassa matatizoni); only the President can. Na katika hili ni rais anahitaji kuonesha kuwa anajali wananchi wake.
Hutu tumafuriko twa Dar Rais atangaze hali ya dharura? Yale ya Kilosa na kwingineko alitangaza?
 
Mwenzenu huwa najiuliza mara nyingi - hivi walipokuwa wanataka kuwa viongozi walikuwa wanafikiria wanatakiwa kuongoza nini magari? au kwa wingi wa saluti wanazopigiwa?

Mkuu,sio wewe peke yako.Siku ya maadhimisho ya miaka 50 nilijiuliza mambo mengi sana.Tumeonyeshwa vifaru vya kivita,magari,ndege na mambo mengine mengi.Kuna majanga mbalimbali yanatokea,mfano ile meli ya MV Slice Islanders,nilitegemea wanamaji (Navy) wafanye kazi lakini hakuna kitu watu wamekufa tu.

Nchi zingine ikitokea disaster serikali inahamishia nguvu kusaidia raia,raia ndio tulioowaajiri hawa jamaa(Serikali),hawachukui hatua za haraka kuokoa watu,wao wapo wapo tu,kazi kupita kwa ving'ora barabarani.

Hatukatai,kuna mambo ambayo ni force of nature yatatokea tu,kwa mfano hili la mafuriko.Kinachotakiwa kufanywa ni vikosi vya uokoaji kuwa active.Lakini hapa kwetu Tanzania ni ubabaishaji tu,hatujawahi kufanya kitu effective tuna appreciate kwamba kazi imefanywa.There must be a problem somewhere.

Jana,nilikua maeneo ya jangwani,nilishuhudia watu wawili wakidondoka kutoka kwenye paa la nyumba na kutumbukia kwenye maji,hawakuonekana tena.Baada ya muda nikaona helicopter inazunguka zunguka mithili ya watalii.Nikaambiwa ni Merky Sadiq anaangalia mafuriko.Hapa nikajiuliza mambo mengine mengi.Hivi ni wasaa wa kuzunguka na kuangalia au ni wa kuchukua hatua?

Bado tunarudi palepale,kuna ubabaishaji mkubwa katika serikali na watendaji wake.Ukiona familia bora na yenye upendo na furaha,Ujue Baba yuko makini kama kiongozi wa familia.Think
 
Haya mafuriko yangetokea huku sumbawanga, hakuna ambaye angeandika thredi. Huwa anapaga hasira sana. Hata EWURA huwa wanatangaza bei za dar tu, na mafuta yakikosekana dar ndo wanahaha. Sisi huku hatuna umeme wala maji, lakin sijaona thredi. Ingekua dar je?

Wewe si ndio uko Sumbawanga kwanini usilete thread ya maafa mnayopata? Sasa unataka mtu wa Dar ndio akuandikie? Mbona tabia ya kulaumu inazidi mipaka
 
Kikwete alikuwa serengeti kwenye hoteli yake ameanza kusheherekea sikukuu huku wananchi wake wanasombwa na mafuriko
Atakatisha starehe zake kama ilivyo ada na atakapofika dar, atapanda helikopta atazunguka kisha ataingia ikulu kulala, just like all other times.... hana jipya
 
Mkuu,sio wewe peke yako.Siku ya maadhimisho ya miaka 50 nilijiuliza mambo mengi sana.Tumeonyeshwa vifaru vya kivita,magari,ndege na mambo mengine mengi.Kuna majanga mbalimbali yanatokea,mfano ile meli ya MV Slice Islanders,nilitegemea wanamaji (Navy) wafanye kazi lakini hakuna kitu watu wamekufa tu.

Nchi zingine ikitokea disaster serikali inahamishia nguvu kusaidia raia,raia ndio tulioowaajiri hawa jamaa(Serikali),hawachukui hatua za haraka kuokoa watu,wao wapo wapo tu,kazi kupita kwa ving'ora barabarani.

Hatukatai,kuna mambo ambayo ni force of nature yatatokea tu,kwa mfano hili la mafuriko.Kinachotakiwa kufanywa ni vikosi vya uokoaji kuwa active.Lakini hapa kwetu Tanzania ni ubabaishaji tu,hatujawahi kufanya kitu effective tuna appreciate kwamba kazi imefanywa.There must be a problem somewhere.

Jana,nilikua maeneo ya jangwani,nilishuhudia watu wawili wakidondoka kutoka kwenye paa la nyumba na kutumbukia kwenye maji,hawakuonekana tena.Baada ya muda nikaona helicopter inazunguka zunguka mithili ya watalii.Nikaambiwa ni Merky Sadiq anaangalia mafuriko.Hapa nikajiuliza mambo mengine mengi.Hivi ni wasaa wa kuzunguka na kuangalia au ni wa kuchukua hatua?

Bado tunarudi palepale,kuna ubabaishaji mkubwa katika serikali na watendaji wake.Ukiona familia bora na yenye upendo na furaha,Ujue Baba yuko makini kama kiongozi wa familia.Think
Mnalikuza sana suala hili la mafuriko ya Dar. Halilingani hata na mafuriko ya Kilosa. Kwa kuwa JMK ndie Rais basi "mnachooonga"! Anzisheni michango tuwasaidie wenzetu waliopoteza shuka na vikombe vyao.
 
Nna uhakika kuwa viongozi kadha wa kadha weshawahi kwenda kwenye warsha na makongamano marefu na mafupi nchi za nje kujifunza namna ya kukabiliana na maafa na majanga kama haya. Nna uhakika pia kushafanywa warsha nyengine nyingi mno ndani ya nchi pia.

Kinachosikitika ni kuwa tuna act kama maafa haya ndo kwanza leo kutokea popote pale duniani-kama maajabu ya dunia vile.

Tusema kuwa ni kweli serikali haina uwezo wa kiufundi wa kufanya uokozi au wa kuzuwia kusambaa zaidi kwa maafa hayo, lakini serikali inashindwaje kuweza kuzungumza tu na wananchi wake?

Tuseme hawajui kuwa katika kipindi cha maafa kinachotoa faraja zaidi kwa wote ni ule upatikanaji wa taarifa na kuelewa kuwa watu wote wapo pamoja nawe? Rais, Waziri Mkuu, Mkuu wa Mkoa, Wabunge, mko wapi?

Taifa letu ni sikio la kufa... si viongozi si wananchi! Wananchi kila leo hii wanakumbwa na majanga yanayofanana-fanana na ambayo yangeweza kabisa kupunguzwa makali yake. Lakini wananchi haohao nyakati za uchaguzi wanarudia kuchagua miviongozi ileile ambayo huwa inawatelekeza baada ya chaguzi kupita. Miviongozi nayo hivyo hivyo. Ahadi nyingi, posho nyingi, safari na semina zisizoisha lakini utendaji na ubunifu ni zero!! Linchi limeharibika na kuwa la porojoporojo tu na kuchumia tumbo. Mijitu mingi ni mibinafsi. Miviongozi inaongopa hadi kwenye hotuba za Kitaifa. Aaarrgghhh!!!!

Gaijin, siyo tu kwamba wamefika na kujifunza mbinu ya kukabiliana na majanga kama haya; bali kuna watu na vitengo wanalipwa na kuhudumiwa na kodi za wananchi kwa ajili ya kupunguza maafa na kadhia ya majanga kama haya lakini ndiyo hivyo tena, hamna linalofanyika!
 
Hata Nape aulizwe yuko wapi aelezee kuguswa kwa Chama katika hili na kiasi cha rambi rambi..........mbona alipogongwa mtoto mmoja pale Igunga alienda na kuita waandishi wa habari? leo watu 13 wamefariki kwa mafuriko yuko kimya???????
 
Pale alitaka kura, now keshazipata hautamsikia hivi karibuni
 
Mnalikuza sana suala hili la mafuriko ya Dar. Halilingani hata na mafuriko ya Kilosa. Kwa kuwa JMK ndie Rais basi "mnachooonga"! Anzisheni michango tuwasaidie wenzetu waliopoteza shuka na vikombe vyao.

Mkuu katamke haya mbele ya mtu aliyepoteza ndugu au jamaa... ndiyo utajua kama tunalikuza! Kaongee haya mbele ya watu wenye malori yaliyobiduliwa na bidhaa zao kuchotwa na maji ndiyo utajua kama tunalikuza...

Na nikirudi kwenye msimamo wako, sasa kama janga hili tunalikuza kwanini basi sisi kama Taifa tumeshindwa kulitatua mara moja?!
 
Hutu tumafuriko twa Dar Rais atangaze hali ya dharura? Yale ya Kilosa na kwingineko alitangaza?

... hawezi! Na hana haja ya kufanya hivyo! Nchi yetu ni ya amani na usalama isiyo na majanga wala ufisadi! CCM Oyeeeeh!! Zidumu fikra za Mwenyekiti!!
 
Mkuu Mwanakijiji,
Umefanikiwa kuwapata red Cross? na jitihada zipi zaidi zinafanyika.. Ni Asasi zipi zinapatikana kujihusisha na maafa haya maana nataka kuandaa ukusanyaji wa nguo, blanketi na fedha kama tutaweza ili tuweze kuzituma ktk taasisi inayohusika.. naomba sana unipe taarifa hizi kwa sababu itakuwa vizuri kama tutakuwa na info zilizo kamili...

..."Waziri Mkuu wa Tanzania Mzee Mwanakijiji ametoa tamko kuhamasisha taasisi za serikali na zile binafsi kusaidia upatikanaji wa mablanketi..."
 
Kaaazi kweli kweli, Mwanakijiji tafadhali ni PM kama ukipata mwongozo...maana siwezi fuatilia mada hizi kesho..
Kila la Kheri jamani - MaaSalaam.
 
Najihisi kukosa nguvu kila nikicheki namna tunavyopeleka mambo yetu!!

Taifa la juhudi binafsi za watu wake......
Hongera
MMM na Mkandara ( na watanzania wengine wote wenye fikra na jitihada kama zenu) kwa initiatives zenu....

Japo ni wazi sana hatutafika kwa staili hii.
 
Kama ni salaam!!!! hata JK kamtumia mkuu wa mkoa, msipotoshe mada mama tibaijuka ni kiranja wa zamu kwa hili anapashwa kuwepo ili kuripoti matukio kwa kiranja mkuu

Ametoa jana.
Nazungumzia hali yakujali na sio kuupotosha umma.
 
Mkuu katamke haya mbele ya mtu aliyepoteza ndugu au jamaa... ndiyo utajua kama tunalikuza! Kaongee haya mbele ya watu wenye malori yaliyobiduliwa na bidhaa zao kuchotwa na maji ndiyo utajua kama tunalikuza...

Na nikirudi kwenye msimamo wako, sasa kama janga hili tunalikuza kwanini basi sisi kama Taifa tumeshindwa kulitatua mara moja?!
Jambo likitokea Dar mnalikuza sana. Barabara zetu zinachinja wangapi kila wiki? Janga la asili kama hili halitatuliki mara moja kiasi hicho. After all, mvua hadi dakika hii tunayojibizana humu zinaendelea kunyesha.
 
Hali ya hatari mbona imetangazwa na kamanda kova tangu jana watu wote waliokuwa wanataka kutoka majumbani mwao walikatazwa na wale walioko mjini na maofisini waliambiwa warudi kwao ikibidi. Tangazo hili lilisaidia waajiri wengi kuwaruhusu wafanyakazi kurudi majumbani ili serikali, JWTZ na Polisi waendelee na zoezi na kuokoa na kulinda amani. mimi ni mmoja wa waliosaidiwa sana na tangazo hilo na wenzangu tuliambiwa mara moja tuondoke ofisini kwenda kuangalia majariwa ya familia zetu na kutoa taarifa kadri ilivyooneka ni muhimu kufanya hivyo.
 
Ameongeza Rais Kikwete: “Napenda pia kupitia kwako kutoa pole zangu nyingi kwa wote walioumia ama kupoteza mali zao katika mafuriko haya. Wajulishe kuwa moyo wangu uko nao wakati huu wa mazingira magumu. “Chini ya usimamizi wako, ningependa kuona uongozi wa Mkoa kwa kushirikiana na taasisi na vyombo vyenye ujuzi na uzoefu wa kupambana na majanga na dharura za namna hii, kuhakikisha kuwa tunaendelea kuokoa watu ambao badowamezingirwa na mafuriko, tunawapa matibabu wale walioumia katika mafurikohayo, na tunawahifadhi na kuwapa huduma za kibinadamu wote waliopoteza nyumba na makazi yao katika mafurikio hayo.”

IMETOLEWA NA:
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
DESEMBA 21, 2011
DAR ES SALAAM

Ikiwa hii paragraph haijeditiwa na aliyeiweka hapa, basi hii ndio picha halisi ya ikulu yetu. Utafikiri imeandikwa na kindergarten kid fulani hivi huko kijijini. How can they be serious ?
 
Back
Top Bottom