Tafadhali AAR msichukue Maamuzi haya kwani Tanzania ya sasa tuna Rais mzuri Mama Samia Suluhu Hassan ( Mrejesha Tabasamu ) kwa Wananchi

Hiyo insurance wing iliondoka 2019. Consolidation tunayofanya tutazalisha Tanesco nyingine. Serilali haitakiwi kufanya kila biashara maana haina efficiency test. Kwa mfano elimu isingekua vital ningeshauri ibinafsishwe. Ukiangalia elimu inayotolewa Na private ni quality nzuri mno. Ni tofauti Na elimu ya serikali lakini malengo ya private yanaweza kuwa tofauti ndo maana haiwezekani kuibinafsisha. Maadam watu wanakatwa mishahara yao hats huko BOT, TANAPA Na kwingine wangepewa Uhuru Wa kuchagua wanataka kutibiwa wapi. Kukiwa Na competition unawafanya watoa huduma Wa serikali kuamka.
 
Wanaachaje kuzibeba kwa mfano?.
 
Hutomuona CAG akipelekwa huko kwenye NHIF, wala pension funds, maana, mafundi uashi walijua kuzikopa bila maandishi ya kisheria kwa vimemo tu...
Pension Funds kuna kipindi wakopaji walikuwa karibia ni wanasiasa wa vyama vyote, wana misala yao, hapo huwa wanaungana maana wanajua wakiletwa wadaiwa sugu n.a. wao wamo ndani, watawala kwa wapinzani.

Wanaharakati wataaibika!

Everyday is Saturday..............................
 
One day Sunday will marshal. Then we shall do to them as French did to Maria Antoinette. History is a good teacher for those who can learn it.
 
AAR Insurance waliondoka (exit) 2019. Sasa AAR Healthcare nao wanaondoka. Soma vizuri post ya mleta mada.
 
Waliowahi kuhudumiwa na AAR miaka ya 2005 n.k watakubaliana na mimi kuwa miaka hiyo AAR ilikuwa habari nyingine,watu tulijivunia kuwa na bima za AAR,lakini kwa kipindi kilichopita hata kabla ya ujio wa corona huduma ilishayumba,makampuni yanayojiweza au kuwajali wafanyakazi wake wengi walishachukua maamuzi mengine.Binafsi siamini kama ni hali ya kisiasa au corona kuna jambo lililokuwa linaendelea ndani. Tukumbuke AAR walianza kwa kuhudumia wateja wao tu,yaani waliokuwa na bima zao na hapa huduma ilikuwa supper,baadae wakaanza kutoa huduma kama mahospitali mengine kwa kupokea bima nyingine na shida ikaanzia hapa.
Mimi naona kama wataamua kuondoka ni sawa,maana hatuwezi kuwapangia,mambo ni free market.ukiona point A hupati faida unahamia point B wanaokutaka watakufuata
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA........
 
Umeandika hawana matatizo compire na Jubilee... mimi nijuavyo na nilishajionea kabisa watu wote wanaochukua kampuni za bima cha kwanza huwa ni wababaishaji, Wakora dhurumati waongo na watu wa shortcut... na hao ndio huwa mabalozi wakubwa wa kuvumisha uongo wao waonekane wameonewa ili wapate huruma... kuna kipindi walikuwa wanacheza michezo yao hadi na taasisi na mamlaka ziwasaidie kulazimisha uongo zilipwe mafao yasiyostahili kwao... na hii ni kweli kabisa.

Bima halali inalipika bila matatizo na bima fake hata mtoto anajua kuwa ni fake na akitumwa investgator hata hachukui lisaa anajua fake.. so wapingaji ndio huja juu kuwa wamedhurumiwa haki zao.. kungekuwa na mamlaka sahahi Tanzania wote wanataka kuibia kampuni za bima wangekuwa wanakamatwa na Takukuru kisha wakasote jela upuuzi wao utapotea maana kuna kundi fulani ndio lina michezo hii ya wizi kutokea kwa mabroker na ma agent so mbinu zinasambaa kila kukicha.. nakumbuka kuna kampuni ilikuwa inatumua polisi live kuchunguza ajali n.k mabroka waliikimbia kupeleka biashara zao hadi ile kampuni ikaacha watu wanadeal na kuziibia tu Kampuni za bima.. huko Hospital ndio mufilisi kabisa ukiumwa mafua kicha n.k kwa kadi ya bima inaondoka hadi elfu 50 kupima kumuina dr na vidawa vya mafua au kikohozi. Unategemea kampuni zitasurvive vipi na group la wezi walio mahospitalini.. kwa mfano Aga khan niliwahi sikia dr huwa ana target anapewa mgonjwa lazima kadi yale ikamuliwe haswa ikiwezekana aongeze na cash yake binafsi...
 
So far provider mwingine labda Strategies, maana jubilee walishajifia, mashirika makubwa yote yalikua yanatumia AAR na taasisi za maana, binafsi naona ni pigo kubwa maana hakuna provider ambae amejitosheleza mpaka vijijini kama aar
Ah! waondoke tu
 
Umeongea kweli pia.
Kuna jamaa fulani wanufaika wa medical insurance; walikua wanashirikiana na mmiliki wa pharmcacy kuwaibia kampuni ya bima. Walichokua wanafanya, yule mmiliki wa pharmacy alikua pia ana duka kubwa la cosmetics. So, wale wanufaika walikua wanaandikiwa dawa labda za 50,000 halafu akienda pale pharmacy anapewa vipodozi na vitu vingine vyenye thamani ya 50,000 ila kule inakua recorded kama vile mhusika amechukua hizo dawa!
Hao ndo Watanzania.
Mlaleo
 
Uko sahihi kabisa. na AAR wamebadilisha jina kwa sasa wanaitwa Assemble Insurance 100% owned by Tanzanian.
 
Ni wakati sasa turudi kwenye misingi ya ushindani wa kibiashara kwa kuachia free market economy, Mashirika ya Bima yashindane ndo hapo tutaona uwezekaji zaidi katika ndustry hii.

Bima ya afya kwa wote haina maana kuwa lazima kila mtu ajiunge NHIF (Compulsory scheme), la hasa, Bima ya afya kwa wote ina maana kuwa almost kila mwananchi awe covered na bima ya Afya bila kujali ni aina gani ya mfuko.

Hebu angalia NHIF inatoa tija na ajira kiasi gani? Ila unaporuhusu mazingira ya kiushindani ambapo pia mifuko mingine inapelekea kutoa huduma pia ajira kwa vijana.

Serkali ifikirie mara mbili hapa, mfumo wa serkali kuhodhi kila sekta umepitwa na wakati.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…