Tabora wampokea kwa shangwe Dr. Slaa

Tabora wampokea kwa shangwe Dr. Slaa

Tuacheni mbwebwe Tabora hakuna Chadema bana.

Tabora hamna chadema ndo maana maendeleo duni, Tabora ya sasa ni tofauti mkuu kuna chuo kikuu hapa na sehemu yeyote ambayo kuna chuo kikuu kunakuwepo na elimu ya uraia inayowafanya watu kujitambua kupitia wasomi hao, Tabor unayoijua sio ile ya mwaka 2005 watu wameamka wamepuuza propaganda zenu za udini.
 
nimeipenda hiyo, saa ya ukombozi ni sasa. big up wanatabora kwa muamko wenu dk songambele tukopamoja nawe
 
Tabora hawana mda wa kukusanyika kwa ajili ya wazinifu
 
Huyu anadhani watu watakaa na ujinga wa ccm mpaka lini ? Tabora amka amka mboka manyema achana na upumbavu wa ccm
 
Tabora hamna chadema ndo maana maendeleo duni, Tabora ya sasa ni tofauti mkuu kuna chuo kikuu hapa na sehemu yeyote ambayo kuna chuo kikuu kunakuwepo na elimu ya uraia inayowafanya watu kujitambua kupitia wasomi hao, Tabor unayoijua sio ile ya mwaka 2005 watu wameamka wamepuuza propaganda zenu za udini.

ninakubaliana na wewe 100% hata dodoma mjini hali ni tofauti sana sasa hivi
 
Dk. Slaa: Tukishika dola tutaruhusu utengenezaji pombe ya gongo


Saturday, 14 December 2013 · Posted in OMG, Siasa


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetoa mpya baada ya kueleza kuwa kitakapofanikiwa kushika dola kitaruhu Shirika la Viwanda Vidogo Vidogo (SIDO) kutengeneza mitambo ya kutengenezea pombe aina ya gongo. Katibu Mkuu wa Chadema, Dk.Willbroad Slaa, akizungumza na wananchi wa Jimbo la Kasulu Vijijini alisema kama gongo itatengenezwa kwa mitambo maalum itaondoa mianya ya rushwa kwa polisi ambao wamekuwa wakiwakamata wanaotengeneza kwa kificho na kuwafanya vitega uchumi vyao.


"Gongo sasa hivi ni haramu sababu inatengenezwa kwa kificho katika mazingira machafu, tukishika dola tutataka SIDO itengeneze mitambo ya kutengeneza gongo ili iwe katika hali ya usafi," alisema.


Mitambo hiyo itakayotengenezwa na SIDO itakapouzwa itaiingizia mapato serikali pia wauzaji wa gongo watafanya biashara hiyo kwa amani tofauti na sasa ambapo wanaifanya kwa kificho na wakikamatwa fedha zote wananufaika polisi.


Dk. Slaa alisema hata suala la kukamata watu wanaotengeneza silaha linapaswa kuangaliwa upya kwani wanaokamatwa wakifanya kazi hiyo wangekuwa wanashikiliwa kwa muda na baadaye wanapelekwa katika kiwanda cha serikali cha kutengenezea silaha ili watuhumiwa hao wapeleke ujuzi huo huko badala ya kuwafunga jela.


Dk. Slaa alisema matatizo yote yanatokana na wasomi kutofikiri namna ya kuisogea nchi mbele kimaendeleo.


"Nchi hii imelala, imechoka sababu waliopewa madaraka wamelala, wamejisahau hawatambui kuwa wamepewa nafasi hizo ili kuwatumikia wananchi," alisema.
CHANZO: NIPASHE
 
Wewe unaijua Tabora? Au umetoa macho kwenye mtandao?
Mimi Tabora naijua yote pale mjini, Kanyenye. Bachu, Ngambo, Uwaziri, pale sokoni Meya Hotel nikifika Tabora huwa nakula hapo.

Bado Sikonge, Ulambo, Nzega,
Igunga, kote huko nimefika.
 
Ngoja akina umla na Simbilisi wajipe matumaini huku wazee wa kazi wakifanya kweli mwanza na Tabora wakija kusituka wamebaki CCM watatu Bungeni. Mwaka 2015 hatununuliki ila tutapokea haki tunayopunjwa na kuwanyima kura wanyonyaji
 
we acha ubwege Tabora is my home town naijua zaid unavyoijua wewe kwanza Tabora hakuna chadema hata chembe sasa we unaongea nini acha ushamba bwana mtu mzima unatia aibu.

unadhani Singida mashariki kwa Lissu kulikuwa na cdm.jiulize alipenyaje.na ndio kosa wanalofanya CCM Tabora,wameridhika sana kiasi cha kuamini Munde anaweza kuwa mbunge,huyu nimefanya nae kazi LAAC mwaka huu,hajui kitu ni mtupu.nimeitembelea ofisi ya tawi ikiyopo mkabala na Magamba pale kontena,vijana wana mbinu kali sana
 
Dr Slaa pambana na haya makaburu ya Tanzania. Tunakuunga mkono.
 
Kama kigoma walimpiga mawe kwanini sio tabora?
 
unadhani Singida mashariki kwa Lissu kulikuwa na cdm.jiulize alipenyaje.na ndio kosa wanalofanya CCM Tabora,wameridhika sana kiasi cha kuamini Munde anaweza kuwa mbunge,huyu nimefanya nae kazi LAAC mwaka huu,hajui kitu ni mtupu.nimeitembelea ofisi ya tawi ikiyopo mkabala na Magamba pale kontena,vijana wana mbinu kali sana

Acha pombe za kienyeji wewe, huo mtukuru wa ikungi umekuchubua uso na ubongo na hizo gongo zenu. Tabora sio singida mashariki. Lazima mpigwe mboko za mgongo.
 
Tabora hawana mda wa kukusanyika kwa ajili ya wazinifu

Tatizo lenu siyo wabunifu kiasi kwamba mtu kuona komenti yako hata bila kuisoma anajua umeandika nini. Mmesoma kweli au mmekuwa kasuku tangu mwaka 2010 mpaka leo bado hayohayo !!!!!?Tafuteni kitu kipya tumechoka na haya ya uzinzi, ulaghai n.k
 
Wakati Mwanza wakijiandaa na mkutano mkubwa wa hadhara wa Mkiti wa Taifa, Freeman Mbowe leo, hapa Tabora kuna mapokezi makubwa sana msafara wa Gwiji wa Siasa Tanzania na Katibu Mkuu CHADEMA Dkt. Wilbroad Slaa unapita Tabora mjini kwenda Jimbo la Tabora Kaskazini.

Wananchi wa Tabora mjini wamejitokeza kwa wingi sana kumpokea Katibu Mkuu wa CHADEMA. Ni msururu wa Pikipiki na Magari ambayo idadi yake kwa harakaharaka ni vigumu kutoa hesabu yake.

Watu wamejipanga barabara zote huku wakimshangilia Dr Slaa kwa mfano ambao ni historia.

Source: Afisa Habari Mkuu CHADEMA Tumaini Makene

Wacha upumbavu tafuta kazi ufanye we pimbi! Hadi leo unapotezewa muda na wanasiasa,mafanikio ya Dk Slaa yatakusaidia nini wewe! Hangaikia tumbo lako na familia yako kama Slaa anavyo hangakia Maisha yake ktk siasa. Unadhani yupo kwa ajili yako!.
 
Last edited by a moderator:
ninakubaliana na wewe 100% hata dodoma mjini hali ni tofauti sana sasa hivi
Majimbo yote ambayo chadema iliazimwa na ccm 2010 yatarudi 2015 kwa kishindo. Wauwaji hawatakiwi tena tz
 
Hii misukule ni janga la taifa


Angalia sasa wanachoandika Chris na Ritz.

Ritz: Hii kweli ni breaking news
Lukosi: Hii misukule ni janga la taifa


Yaani maandishi yote ni pumba, hata watoto wao wakisoma wataona mibaba mijinga.

Jamani plz, hata kama mnaichukia chadema, andikeni kitu chenye mashiko siyo haya maneno ya kijinga. Ritz kwa mfano, nani kaandika breaking news?
 
Nilifika masasi mwaka 2008 na nipo hapa hadi sasa.hakukuwa na vyama vya upinzani kabisa.kwa hiyo lindi na mtwara zaidi ya 90% ilikuwa ni ccm pekee.mambo yamegeuka ghafla mwaka jana.watu hawataki hata kuisikia ccm.vijijini kabisa kule ni chadema tu.
Mimi naamini kuwa kwa ninayoyaona huku kusini ccm kushinda katika uchaguzi mkuu ujao itakuwa ni muujiza wa shetani.
Hii ni kwa sababu ccm imewakorofisha watu katika makundi yao yote; wakulima,wafanyabiashara,wafanyakazi,akina mama na vijana.pia watumishi katika idara nyeti kama vile usalama wa taifa na askari wako tayari kuona ccm ikitokomea.
 
Wacha upumbavu tafuta kazi ufanye we pimbi! Hadi leo unapotezewa muda na wanasiasa,mafanikio ya Dk Slaa yatakusaidia nini wewe! Hangaikia tumbo lako na familia yako kama Slaa anavyo hangakia Maisha yake ktk siasa. Unadhani yupo kwa ajili yako!.

Akili ya CCM hii.
 
Back
Top Bottom