Tabora to Kigoma via Urambo, Barabara ikoje?

Tabora to Kigoma via Urambo, Barabara ikoje?

Afri-Cast

Member
Joined
Apr 1, 2020
Posts
49
Reaction score
109
Habari ya Asubuhi wakuu, nina safari ya Kigoma from Dar, Mara ya mwisho nilipitia Nyakanazi-Kakonko-Kibondo-Kasulu, Wenyeji wa ile Barabara wakasema nimezunguka mno, Next time nipitie Tabora-Urambo-Uvinza.

Sasa hii njia siijui vizuri naomba ushauri kwa aliyepita siku za karibuni, na lami imeishia wapi kwa sasa? Maana kupitia nyakanazi kuna karibu 200Km za rough road inachosha sana! Naomba ushauri kwa aliyepitia Urambo-Uvinza.
 
Habari ya Asubuhi wakuu, nna safari ya Kigoma from Dar, Mara ya mwisho nilipitia Nyakanazi-Kakonko-Kibondo-Kasulu, Wenyeji wa ile Barabara wakasema nimezunguka mno, Next time nipitie Tabora-Urambo-Uvinza. Sasa hii njia siijui vizuri naomba ushauri kwa aliyepita siku za karibuni, na lami imeishia wapi kwa sasa? Maana kupitia nyakanazi kuna karibu 200Km za rough road inachosha sana! Naomba ushauri kwa aliyepitia Urambo-Uvinza
Kwasasa Atcl inafika dar- kgma mara tatu kwa week bei ni nzuri nakushauri panda hiyo unusuru mda wako
 
Hiyo Njia ya Kigoma kupitia Urambo, Kaliua, Uvinza hadi Kigoma ni inshu sana shimo zake lwenye Vumbi zinaweza fika KM 200.
Nawaza tu kwamba Kwanini ukifika Tabora usipite Sikonge, Ipole, Inyonga, Mpanda, Mishamo, Uvinza hadi Kigoma ambayo shimo lake linafikia KM130 hiii ni baaada ya Barabara ya Tabora - Mpanda kukamilika kwa kiwango cha Lami so unaweza endesha Tabora Mpaka 4 Hrs then Mpanda Kigoma 5 Hrs tena
 
Great Option! Ntafika Tabora alafu niwaulize wadau ili kujua siku hiyo hali ikoje! Ahsante sana
 
Kwasasa Atcl inafika dar- kgma mara tatu kwa week bei ni nzuri nakushauri panda hiyo unusuru mda wako

Kuna Mizigo kusafirisha kwa ndege ni issue mzee! Wazee wa field wananielewa na hapo umepakia watu wa4 wengine!
 
Kuna Mizigo kusafirisha kwa ndege ni issue mzee! Wazee wa field wananielewa na hapo umepakia watu wa4 wengine!
Mkuu huyo ni middle class aliyezikuta tayari, pigana mkuu na mtu asikupangie cha kufanya, wenye Nia ya kukushauri watafanya hivyo,eti kwa nini usiruke kwa ndege!this I bulshit wakati hajui program zako
 
Yap wenyeji wamekushaur vizuri toka dar mpaka singida pale manyoni katisha ingia itigi tokea Tabora mjini pumzika asubuhi saa kumi na mbili anza safari ya kigoma pitia urambo, kaliwa, uvinza ndani ya masaa sita upo kigoma mjini

Barabara ni nzuri ondoa shaka hata sienta unaweza fika nayo
 
Mkuu pita tu hiyo barabara ya Tabora _Urambo_Kaliua_Uvinza_Kigoma haina shida sana.Lami inatoka Tabora hadi Kaliua.Kutoka hapo unakula vumbi hadi Uvinza halafu unakula Lami hadi kigoma.Ni safari ya takribani saa 6 kutoka Tabora hadi Kigoma.Nakutakia safari njema.
 
Dar Es Salaam, Manyoni, Itigi, Hadi Tabora, Urambo, Uvinza, JK Bridge, Mpeta Hadi Kigoma .Buses Hizi Ndiyo Njia Hupita Kila Siku
Adventure, Saratoga, Aifola, Majinja, Takbiir, Hizo Toka Dar Es Salaam ~Kigoma
AN, Satco Kutoka Dodoma ~ Kigoma

Njia Wanayoipita Hawa Kila Siku Maana Yake Toa Shaka Fuatana Nao
 
Ukitokaa taboraa Rami mpk mitaa ya isawima mbelee kabisaa yaa kaliua then unatembea kwenye vumbi mpk sehem mojaa anaitwaa ilalanguru ipo Nguruka hapoo unapandaa Rami kiwango cha USA mpk mpetaa baada ya hapo unakulaa vumbi mpk uvinza ukikanyaga Rami uvinza ni mpka kigoma
 
Habari ya Asubuhi wakuu, nna safari ya Kigoma from Dar, Mara ya mwisho nilipitia Nyakanazi-Kakonko-Kibondo-Kasulu, Wenyeji wa ile Barabara wakasema nimezunguka mno, Next time nipitie Tabora-Urambo-Uvinza. Sasa hii njia siijui vizuri naomba ushauri kwa aliyepita siku za karibuni, na lami imeishia wapi kwa sasa? Maana kupitia nyakanazi kuna karibu 200Km za rough road inachosha sana! Naomba ushauri kwa aliyepitia Urambo-Uvinza
Barabara sehemu kubwa Ina lami. Kuna vipande viwili vya barabara vinajumla ya 50Km ambavyo havina lami, lakini kuna wakandarasi wameanza kazi. Huna haja ya kupitia Nyakanazi, pitia Urambo safari itakuwa nyepesi
 
Hiyo Njia ya Kigoma kupitia Urambo, Kaliua, Uvinza hadi Kigoma ni inshu sana shimo zake lwenye Vumbi zinaweza fika KM 200.
Nawaza tu kwamba Kwanini ukifika Tabora usipite Sikonge, Ipole, Inyonga, Mpanda, Mishamo, Uvinza hadi Kigoma ambayo shimo lake linafikia KM130 hiii ni baaada ya Barabara ya Tabora - Mpanda kukamilika kwa kiwango cha Lami so unaweza endesha Tabora Mpaka 4 Hrs then Mpanda Kigoma 5 Hrs tena
Ofcourse haijakamilika lami kama 200km hivi ila inapitika.

Best option kama ni kupita Dar Tabora Mpanda Kigoma ila wasi wasi wangu nauli itakuwa kubwa sana karibia mara mbili ya nauli ya Dar Tabora Urambo Kaliua Uvinza Kigoma. Kwa sababu hakuna gari ya moja kwa moja inayopita njia hiyo na probably utakuwa umeongeza urefu wa Safari.
 
Nilipita hapo mwezi wa 8 mwaka Jana.. kimsingi barabara ni nzuri unless mvua zinazoendelea ziwe zimeharibu barabara.

Kuna kipande cha km 80 kutoka kaliwa kwenda Nguruka halafu kingine ni kama km 50 hivi katikati ya Nguruka na Uvinza.

Inategemea na aina ya gari na hali ya hewa siku hiyo itakuwaje otherwise I recommend upite tu
 
Pita ndg Isawima to Ilalanguru rough road ni 38Km then unakula lami ya maana ya kifilipimo Hadi Malagarasi bridge then unapiga rough road Hadi Uvinza town 45 km barabara pamoja na kuwa rough inapitika vyema kabisa, karibu mkuu Mimi nipo Uvinza hapa chuma inapumua baada ya safari ndefu
 
Yap wenyeji wamekushaur vizuri toka dar mpaka singida pale manyoni katisha ingia itigi tokea Tabora mjini pumzika asubuhi saa kumi na mbili anza safari ya kigoma pitia urambo, kaliwa, uvinza ndani ya masaa sita upo kigoma mjini

Barabara ni nzuri ondoa shaka hata sienta unaweza fika nayo
Mimi nililala Kaliua saa moja nikaliamsha saa tano niko Kigoma...
 
Asanteni sana wakuu! Nimeamua ntapita njia ya Urambo Kaliuwa to Uvinza! Nimependa ushirikiano wenu
 
Back
Top Bottom