Tabora to Kigoma via Urambo, Barabara ikoje?

Tabora to Kigoma via Urambo, Barabara ikoje?

Mrejesho:

Nilitoka Dar saa tisa na nusu alfajiri, kufika manyoni nikala kushoto pale kuelekea Tabora (Njia safi kabisa about 250kms pamenyooka hakuna hata traffic wengi, ila hakikisha umeshaweka mafuta Manyoni maana sheli hakuna mpka mbele sana)

Nilifika Kaliua saa 17:00 jioni, Sikuona sababu ya kulala, wenyeji wakanipa moyo, nikaona na orobox kibao zinaenda so nikaunga nao.

Kiukweli ni nzuri sana kulinganisha na ya Nyakanazi. Kama wadau walivyosema rough road ni jumla ya 90Kms tu, kipande cha kwanza 40km na kinahudumiwa sana kukiwa na tatizo, kipande kingine ni 50m hiki ni kutoka Malagarasi mpka Uvinza. Nacho ni barabara safi kabisa,

nikaunga na kufika Uvinza saa moja na nusu jioni, nilikuwa naelekea Nyarugusu via Kasulu so kuna kipande cha vumbi 72kms to Kasulu. Ila kama unaenda Kigoma ni lami all the way from Uvinza. Nilifika Kasulu saa tatu usiku

Nilienda na gari ya chini tena 2WD na sikupata tatizo lolote, Kurudi nilipita same way, nikawahi zaidi kuanza safari, nvua ilikuwa kali sana lakini barabara inapitika kabisa Nikafanikiwa kufika Dar saa tano usiku, Only this time i had longer pauses barabarani kujinyoosha kidogo.

Ahsanteni sana wote mlionipa Ushauri.
Hongera saaana mkuu
Tuelekeze hiyo ni gari gani ulienda nayo ni hizi zenye cc above 1700? Au hivi vi vits, passo nk

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kweli kwa usiku usiku ile njia siyo salama sana ingawa tangu wakimbizi wa Lugufu walipohamishwa angalau matukio yamepungua.

Waliniambia niwe makini tu saa tano usiku watu wanapungua njiani so niwe nimemaliza kipande hicho
 
Back
Top Bottom