Tabora school(Tabora Boys and Girls) a.k.a vipaji/the head of Tanzania..Mpo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tabora school(Tabora Boys and Girls) a.k.a vipaji/the head of Tanzania..Mpo?

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Da vincci, Oct 10, 2010.

 1. Da vincci

  Da vincci Member

  #1
  Oct 10, 2010
  Joined: Aug 9, 2009
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  WanaJF naomba tukumbushane mambo kadha wa kadha kuhusu shule zetu hizi mbili na kongwe zaidi Tanzania...mimi ni mmojawapo kati ya waliobahatika kuwa Mboyzia au mwana Berlin form 5&6 na najua wanaJF wengi mlikua either ma Warsaw au wanaBerlin.

  Jamani kama tujuavyo huko tulikopita alipita Baba wa taifa,spika wetu wa sasa,jaji mkuu wetu pia wa sasa,mama Sitta na wengine lukuki..kwenye miaka ya 98 au 99 hivi ilifanyika harambee kubwa sana hapa Dar ya ma Old boys na ma Old girls a.k.a ma Warsaw..lengo kuu lilikua ni kuchangisha pesa na kufungua mfuko ili kusaidia matatizo ya Harvard na Oxford zetu hizi ndogo..matatizo kama ya majengo kuwa mabovu,vyoo visivyoingilika na nguo,chakula kibovu na kichache(kilichopolekea shule hizi kufungwa kwa muda mwaka juzi)..

  walimu wa manati,umeme wa kuskilizia,maji ya kufata ng'ambo..na mengine kem kem..wanaJF hadi ninaporipoti hivi sasa mara tu baada ya Baba wa taifa kututoka mfuko ule pamoja na akaunti yake na kilichochangwa kilipopotelea sifahamu..kama Kuna mwanaJF yeyote mwenye taarifa na hili naomba aianike jamvini..

  Lastly naomba tukumbushane enzi za kina mr Mrisho,Bitwale,Abdallah,mwalimu Masele..sir Issa yule ticha mlemavu wa macho but nondo vibaya kwenye somo la history,madam ng'osha,maduka,mama mwita na wengine kibao..take a moment na kumbuka lile beef na Milambo!safari za uhazili,kazima,na ng'ambo kuchakachua mambo flani..dah inafurahisha sana kukumbuka ma bweni kama sina nk..safari za jeshni kucheki football..

  Walimu wakali kama Barosha na Kamrali...picha za baba wa taifa kila kona kule upper school zikiwa na jumbe murua na zenye kuibua fikra za kizalendo..tusisahau ma boogie dance na dada zetu wa warsaw,discussion za jumapili kwa advance..safari za kanisani student centre..mama Kabìgi,kuna mengi sana ya kukumbushana ma old boys wherever you are. . . .
  Nawasilisha.
   
 2. Y

  YgJunior Member

  #2
  Oct 10, 2010
  Joined: Jan 12, 2008
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  :llama: mnnakumbuka milambo tulivyokuwa tuna wapa kichapo kwenye mechi kule mwinyi
   
 3. Da vincci

  Da vincci Member

  #3
  Oct 10, 2010
  Joined: Aug 9, 2009
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kaka nakumbuka sana ila walikua wakikuotea town na jezi zako unakula kipondo mpaka unasahau..ila mwinyi na mpepo cup..huwezi sahau.
   
 4. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #4
  Oct 11, 2010
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  hahahahha, ukitaka kuwajua boyzia hata town utawaona wanatembea kwenye mstali ulionyooka halafu wanapiga kwata. Pia choo kile cha pale bweni la sina kilikuwa kinatoa harufu ile mbaya mpaka tulikuwa na jezi maalumu za kwendea koy pia ukitoka lazima upunge upepo nje ili usijeharibu hewa bwenini

  Pia nakumbuka jinsi boyzia walipokwenda kutoa kichapo wosso baaada ya girls kwenda milambo na walipita pale messi wakipiga kelele kuwa kaka zetu tuliendieni watoto wetu sie tunakwenda kwa shemeji zetu!

  bila kusahau falsafa ya mkuu wa shule wakati huo mrisho na slogani yake ya kula sana, kucheza sana na kusoma sana.
   
 5. Da vincci

  Da vincci Member

  #5
  Oct 11, 2010
  Joined: Aug 9, 2009
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Dah kaka nilisahau hako ka terminology ka 'koi'..thanx
   
 6. Che Kalizozele

  Che Kalizozele JF-Expert Member

  #6
  Oct 11, 2010
  Joined: Jul 20, 2008
  Messages: 778
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Naukumbuka msimu wa viazi,ukipiga kiazi chako cha ishirini na bakuli lako la uji ni lazima ukale darasani.Tulipokuwa tunaenda kuangalia mpira kule jeshini kulikuwa kuna wazee fulani walikuwa wanaleta raha sana,utawasikia,"Muraaa,unariona hiro ristam,kule musoma ringekuwa darasa la ngapi,utasikia mwengine anajibu,ra nne muraa".Unamkumbuka ndugu D aka Nkumba na mwenzake Madafu,kwa wale tuliosoma science unamkumbuka Mombeki.Those days.
   
 7. Chona

  Chona JF-Expert Member

  #7
  Oct 11, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 513
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 45
  Wazee mmenikumbusha nchi yangu, mmenikumbusha shule yangu mmenikumbusha mbali sana. Nimekumbuka nyangala za boys ukiwa na kitumbua au kiazi unamgawia kidogo mwenzio. Umenikumbusha "TUKUTUKU" tulikokua tunaenda kuchota maji. Au unapiga puff yani unavuta maji kwaenye bomba hiyo ilitegemea pumzi yako na kifua chako. Nimemkumbuka mwl.madafu mzee wa sifa. Mmenikumbusha siku za nyali na nyama watu wanapiga mbalala, waboyzia watanielewa.

  Kuhusu michango iliyochangwa 1999 kwa ajili ya jubelee ya mika 75, nakumbuka waziri wa elimu enzi hizo Kapuya alipiga misele sana pale tena wakati mwingine bila taarifa sijui ndo alikuwa anazisalandia wazigawane. Ila tulikula wali mchana,chai na mkate asubuhi + disco jioni mambo yameisha. Sijui zile zambarau bado zipo? Watu wengine walikuwa na vyeo eti 1/4 master. Mnakumbuka Umuhofia, Los Angels, Califonia etc.

  Siku watu wakitaka kwenda woso basi wanajiandaa na siku hiyo mabafu yanajaa watu inabidi kusubiliana. Utasikia "HAPO PII VIPI" Mambo mengi sana ningependa siku zijirudie nikutane na rafikizangu tunamengi ya kukumbushiana. But gone are those days.
   
 8. m

  mwita ke mwita JF-Expert Member

  #8
  Oct 11, 2010
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 5,491
  Likes Received: 1,220
  Trophy Points: 280
  nakumbuka kuna jamaa alikuwa anaitwa papa fm wa milambo, alikuwa akigawa kichapo kwa waboyzia kama hana akili, wadau wa milambo mnakumbuka nyimbo za kimbembe? stimu stimu,santiago, na nyinginezo mnamkumbuka majubwa, katondola na zoma?
   
 9. S

  SNAKE HOUSE Member

  #9
  Oct 13, 2010
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Duuuuh aisee walirudia tena ...Kweli walikuwa sugu !
  Peruzi ubaini chanzo cha kujivazi uniform kila mahala....Utabaini chanzo.
  Kundi la makomando toka berlin walienda kuwasalimia waungwana fulani,waliowaahidi kibano pale warsar siku ya visiting .....Aisee Kweli nyuki anang'ata !!!!!!
   
 10. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #10
  Aug 12, 2013
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,840
  Trophy Points: 280
  Dah aisee mnenikumbusha mbali sana enzi za Nyangara na zile zambarau aiseee...ha ha ha ha ...dah...
   
 11. Duniaze

  Duniaze Senior Member

  #11
  Aug 12, 2013
  Joined: Feb 27, 2013
  Messages: 151
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  ha ha ha kakaa..ZOMA VS KATILIGE.POLA NYALI .BABU MSENGI.DH we acha tu MILAMBO ni JKT tosha wana.
   
 12. Duniaze

  Duniaze Senior Member

  #12
  Aug 12, 2013
  Joined: Feb 27, 2013
  Messages: 151
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  MNAJUA WALAMBO LAKN??Wazee wa NGWASUMA,
   
 13. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #13
  Aug 12, 2013
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Mambo ya Nyangara, Eintein Chamber, Kitu Magesa mzee wa Chemistry anakuambia hapa hakuna special yeyote humu wote vilaza!! akikuchapa Physical Chemistry anasahihisha anasema "vague" hahahah!!
   
 14. upendodaima

  upendodaima JF-Expert Member

  #14
  Aug 12, 2013
  Joined: May 23, 2013
  Messages: 2,314
  Likes Received: 1,492
  Trophy Points: 280
  Ndugu D na madafu sina hamu nao kabisa kwa ule ukali wao,vp Mrs Mrisho aka Numeral?
  Safari za Tukutuku kuchota maji na kuonana na Warsaw je?
  Kwa Mrema na Kwa Sonda kama sikosei kucheki mpira je?
  Mwalimu Masele na kamsemo kake ka My Boys?
  Aiseh umenikumbusha mbali sana yaani,naimiss sana Berlin..
   
 15. The Hyper

  The Hyper JF-Expert Member

  #15
  Aug 12, 2013
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 890
  Likes Received: 263
  Trophy Points: 80
  Dah,namkumbuka Katilige na ile bakora yake kama mzee kifimbo cheza.
  Zoma nae,bonge la muonevu ilkuwa ni full kuamshwa alfajiri kama Jkt vile.
   
 16. A

  ANTCCM MISSILE Member

  #16
  Aug 12, 2013
  Joined: Jan 2, 2013
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ninamkumbuka afande chacha kwa sababu alikuwa mtu kwanza kunitukana tusi kubwa sana,
   
 17. h

  hamidshaban JF-Expert Member

  #17
  Aug 13, 2013
  Joined: Jan 4, 2011
  Messages: 259
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Amidu shaban. Greyson ludovic. Japhet komba. Ngolly. Ally kalufya. Mashaka ndonde robert alfred. Seneda patrick saulo. Shemu. Maiko kasongwa.1brahim somea.
  Pawasa.malifimbo. Ngasa.

  Nzela kasomi. Mahuba. Shaban katoto. Magesa sarota. Ayub masenza.wiliam yotham. Abdallah.ahmed. Athman magesa..wemgine nngezeen. My number 0756494249
   
 18. Advocate J

  Advocate J JF-Expert Member

  #18
  Aug 14, 2013
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 3,880
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 160
  Mwaka huu mawoso wamefanya vizuri asee
   
 19. Mbwiga88

  Mbwiga88 JF-Expert Member

  #19
  Aug 14, 2013
  Joined: Jul 9, 2012
  Messages: 640
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kwa mtazamo wangu tabora boys ni shule ya vipaji maalum inayopotea na zisipofanyika juhudi zozote zile za makusudi baada ya miaka mitano hii shuke itapotea katika chati na i think kisimiri ni shule inayokuja kwa kasi kureplace tabora boys.....kwa mfano kwa upande wa advanced level tabora boys imekuwa ikionekana mara chache sana katika top 5 best schools and mwaka huu imekuwa ya kumi na tano...is that a special school??? haipo katika hata shule 10 tu bora za hapa tanzania...na olevel wao ndo hata hawasikiki tanzania ukicompare na olevel wa kibaha au mzumbe...kwa upande wa olevel ushahidi upo hapo chini katika attachment......SPECIAL SCHOOLS HAPA TANZANIA NI:
  1.KIBAHA
  2.MZUMBE
  3.ILBORU
  4.KISIMIRI
  5.TABORA GIRLS
  6.KILAKALA
  7.MSALATO
  Na kuna hii inaitwa Kibaha Girls kwa habari za jikoni in the coming years serikali ina mpango wa kuifanya special school
  ******Tabora Boys nimewaweka hapa makusudi coz wasipoangalia watapoea katika chati muda si mrefu****

  NOTHING PERSONAL BROTHERS IM JUST TRYING TO THINK OUT OF THE BOX
  Ushahidi hapa
   
 20. ndupa

  ndupa JF-Expert Member

  #20
  Aug 14, 2013
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 4,448
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  Hakuna shule za vipaji maalumu...labda vyuo vya vipaji vya uimbaji na uigizaji!! Special skul kwa mawazo yako pia hakunafa siku hizi...labda za vipofu na wenye ulemavu!! Hizo shule ni miaka ya sabin na tisin...
   
Loading...