Emc2
JF-Expert Member
- Sep 26, 2011
- 16,808
- 16,874
Nawasalimia wote ndani ya jukwaa hili la East Africa.
Poleni na uchovu wa shughuli mbalimbali. Wengine siku ya leo wameenda kuabudu huku wengine wakiendelea na shuguli za kujenga Taifa.
Bila kupoteza muda. Napenda kuongelea jambo hili nililoandika katika kichwa tajwa hapo juu. Kwamba Tanzania pekee ndiye rafiki wa kweli na mshindani wa Kenya.
Najua kabisa Kenya ni bwana wadogo kwa Tanzania ndiyo maana wakipata shida huwa wanakimbilia kwa kaka yao kupata msaada. Kuna matukio mengi sana yameshawahi kutokea hapa Afrika huku Tanzania ikibaki kuwa kaka mkubwa kwenye mataifa mbalimbali hususani Kenya.
Tanganyika ilipata uhuru wake mwaka 1961, kipindi kile Jommo Kenyatta alikuwa katika jitihada ya nchi yake kupata uhuru. Kitendo hicho kilimfanya Kenyata kutembea toka Nairobi hadi Dar es salaam kuja kushuhudia uhuru huo. Inaonesha ni namna gani mzee Jommo Kenyatta alivyokuwa anampenda sana kaka yake Tanzania.
Pamoja na hayo kulitokea machafuko ya uchaguzi kwa ndugu zetu wakenya. Kweli mambo yalikuwa makubwa sana. Lakini Tanzania ilijitahidi kurejesha amani ndani ya nchi hiyo. Hakika Kenya anajivunia kuwa na rafiki makini na anayeona mbali kama tai.
Katika suala la EPA Kenya ilitaka kujiingiza mkenge, kwamba kutaka kurudisha ukoloni Afrika kwa mgongo wa mikataba. Lakini kwa kuwa kaka mkubwa anaona mbali alikataa kitu kama hicho. Kitendo ambacho bwana mdogo aliona anaonewa kwa sababu zake kadha wa kadha. Baada ya kuelezwa kwa kina bwana mdogo alielewa lakini ilimbidi ake kimya na kumuachia kaka aubebe mzigo wa bwana mdogo. Kwa kuwa ni bwana mdogo Kaka amesimama kidete kuhakikisha mkataba huo hauingiwi.
Sijawahi kusikia ugomvi wa mipaka kati ya Tanzania na Kenya. Lakini ukiangalia majirani wengine wa kenya ni ugomvi ugomvi tu wa mipaka na maeneo. Upande wa Somalia kuna ugomvi, Upande wa Ethiopia kuna ugomvi, Upande wa S. Sudani kuna ugomvi na Uganda napo kuhusu kisiwa. Hakika upande wa Tanzania diyo pumziko la Kenya.
Nikija kuongelea upande wa ushindani. Tanzania na Kenya siyo maadui lakini ni washindani kiuchumi. Halafu ikumbukwe sisi sote ni waafrika lengo letu ni kuondokana na ukoloni wa watu weupe.
Kwa miongo mingi sasa Kenya imekuwa ikiwa juu kiuchumi hapa Afrika Mashariki.
Lakini kwa muongo huu uliopita Kenya imeanza kuona kuna nchi inakuja kwa kasi kuteka uchumi wa Africa Mashariki. Nchi hiyo ni Tanzania, Imeanza kuchukua idara mbalimbali. Mf: Utalii, Ujenzi, Usafirishaji nk. Kitendo hicho kimemfanya kenya aone kwamba Tanzania ni adui wake. Lakini kusema ukweli ni ushindani mkali wa kiuchumi.
Tanzania imekuwa ikijitahidi sana kuweka mazingira mazuri ya biashara. Hayo mazingira yamefanya watu wengi kupenda kufanya biashara zao Tanzania.
Nchi mbali mbali zimeanza kuhamisha biashara zake toka Kenya na kuja Tanzania. Mfano kiwanda cha vigae kilichopo Kenya kuanza kuhamishia Tanzania
Wawekezaji wakubwa wa viwanda vya cement kuwekeza Tanzania
Dagote Cement
Kiwanda cha Saruji Tanga
Pamoja na hilo jambo kubwa ambalo limeifanya kenya kutetemeka ni baada ya Rais wa uganda kuamua kupitishia bomba la mafuta Tanzania
Na kuna taarifa za chini chini zinasema huenda Uganda wakaamua kupitishia bidhaa zao Bandari ya Dar es salaam.
Nawakaribisha kwa hoja.