TRA kubomoa Duka usiku na kuondoka na bidha kisa Kodi, ni Ujambazi

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,496
3,461
Nina laani kitendo cha Wafanyakazi wa TRA kuvamia Duka na Stoo usiku wa mane na kuvunja milango kisha kuondoka na mali walizodai ni Magendo bila mwenye duka kuwepo.

Kitendo hicho kimesababisha Wafanyabiashara wa soko la Manispaa ya Tabora kufunga maduka kama sehemu ya mgomo baada ya mfanyabiashara mwenzao kuvunjiwa stoo usiku na watumishi wa mamlaka ya Mapato Tanzania TRA.

Usiku wa tarehe 1 July 2023 watumishi wa TRA Tabora walifika kwenye stoo ya mfanyabiashara mmoja kutaka kukagua lakini hata walipobaini kwamba hayupo walivunja na kuhamisha mali zake zote kisha Mlango wakafunga na Kufuli la TRA.

Mgomo wa wafanyabiashara ulipotokea, Serikali ya mkoa wa Tabora ikaagiza kuondolewa kwa kufuli lililofungwa kwenye stoo ya mfanyabiashara Celestine aliyevunjiwa stoo na maafisa wa TRA nq kisha kuchukuliwa kwa mzigo wa vitenge.

Akizungumza na wafanyabishara soko kuu la Tabora kaimu mkuu wa mkoa wa Tabora Dkt. Rashidi Chuachua alisema baada ya kikao na wafanyabishara wamekubaliana pia kwamba apeleke vithibitisho TRA na kisha achukue mzigo wake uliochukuliwa.

Dkt. Chuachua amesema mzigo huo ulitoka nje ya nchi na kwamba ulikua ukifuatiliwa na watu wa custom tangu ulipoingia nchini mpaka ulipofika Tabora na kuitonya TRA kuhusu jambo hilo kabla ya kuvunja stoo hiyo

Wafanyabishara wa soko kuu la Tabora na kwingineko walifunga maduka yao kama sehemu ya mgomo baada ya tukio hilo.

Mstahiki meya wa Manispaa ya Tabora Ramadhan Kapela amesema kitendo kilichofanywa na watumishi wa TRA Tabora kuvunja na kuhamisha mali za mfanyabiashara ni sawa na tukio la ujambazi.

Meya amesema kwamba sSrikali imesikitishwa na tukio hilo lilipelekea mgomo wa wafanyabishara wilayani Tabora.

Amesema ni aibu kwa watumishi hao kujiingiza katika tukio hilo katika wakati ambao serikali inajitahidi kuboresha mazingira ya wafanyabishara.

TRA wanalalamikiwa kwa tuhuma nyingi ikiwemo Madereva wa TRA kukagua Risiti kwa Wapita njia. Pia Wanalalamikiwa kwa kutengeneza Vishoka ambao wanauja kununua kitu cha elfu 2000 na kuondoka bila Risiti kisha anakuja na mtumishi wa TRA kwamba wamemkamata hajapewa Risiti. Hii inapelekea kutoa Rushwa.

Je Sheria inasemaje na utaratibu upoje?

Chacho cha Video ni CG FM RADIO
 
Huo ni mfumo gani tena wa kukusanya kodi!?
 
Back
Top Bottom