Yeeesss!!! Wanachofanya Chadema ni kulipiza kisasi kwa CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yeeesss!!! Wanachofanya Chadema ni kulipiza kisasi kwa CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Apr 17, 2011.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Apr 17, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Wajumbe JF:

  Sasa naamini usemi kwamba muosha naye huoshwa. Kwa hali ilivyo sasa hivi ni kwamba CCM imeumbuliwa (humiliated) sana na Chadema katika masuala ya ufisadi na hususan baada ya Dr Slaa kutoa majina mengine ya mafisadi ndani ya CCM na serikali yake.

  Kusema kweli hii imewafanya CCM kuchanganyikiwa kabisa na ukiangalia speeches za January makamba na Nape jana utaona wanazunguka zunguka tu, wanashindwa kusema mafisadi ni akina nani hao ambao wanatakiwa wajitoe.

  Lakini hatua hii ya Chadema ni lipizo tu la kisasi kwa CCM. Katika kikao cha Bunge cha Februari CCM iliimbua sana sana Chadema katika sakata la tafsiri ya ‘kambi rasmi ya upinzani’ Bungeni.

  Wakishirikiana na CUF na NCCR, CCM ilihakikisha uwenyeviti wa kamati nyeti zile tatu za Bunge zinashikiliwa na Wabunge inaotaka wao CCM. Ilihakikisha kwamba nafasi hizo haziendi kwa Wabunge machachari wa Chadema kama Tundu Lissu, John Mnyika au Godbless Lema.

  Ilikuwa humiliation kubwa sana waliopata Chadema wakati huo na maadui zao humu ndani ya JF wakawa wanachekelea magego nje.

  Chadema sasa wamefanya Tit for Tat au "an eye for an eye" -- yaani jicho kwa jicho. Au pia “kama wewe unajua huo, mie najua huu” – ni semi ambazo zinafaa hapa. CCM sasa hivi wamejinasa katika humiliation kubwa ajabu – walijifanya wajanja katika uwezo wao wa kutumia uwingi wao Bungeni. Na wautumie uwingi huo sasa hivi kujinasua katika umbuko hili kama wataweza. Nyoooo!

  Wao wanafikiri chejo!! Vita vinaendelea!!
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Apr 17, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Nakuunga mkono moja kwa moja. CCM waijifikiri wanazo kila mbinu. Sasa wamekwama -- ulimi nje!!
   
 3. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #3
  Apr 17, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Kama wamekiri ndani ya Chama kuwa Lowasa ni Fisadi mbona hawamtoi katika kamati Ulinzi na Usalama! Wanafanya maigizo hawa wakina Makamba, Nape na Mkama.
   
 4. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #4
  Apr 17, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ujuaji ukizidi kipimo!!! CCM mtatuletea maafa humu nchini!!!!
   
 5. z

  zamlock JF-Expert Member

  #5
  Apr 17, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  safi sana ccm wanajidai wajanja sana
   
 6. skendo

  skendo JF-Expert Member

  #6
  Apr 17, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  sasa ccm mwisho umeshafikia ndiomaana kila wanachokiona wanadhani kitawaokoa mara haa JF mara cdm wanafadhiliwa mara haaa kuna udini mtatapatapa ila mkitua uwanjani kichapotu kama mnadhani amjachuja pandeni kwenye majukwaa muone wananchi wanavyo wazomea na sio siasa za kwenye vyombo vya habari.NYAMBAFU
   
 7. only83

  only83 JF-Expert Member

  #7
  Apr 17, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  ...........Nadhani ni kawaida kwa CCM kuwa hoi kwenye mambo ya msingi...hawana uwezo wa kujenga hoja...
   
 8. F

  Froida JF-Expert Member

  #8
  Apr 17, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Walikurupuka walitakiwa wafanye utafiti wa kina kabisa namna watavyojiokoa lakini sasa wanaonyesha wamechoka kabla ya kuanza safari,mara wanaonya mafisadi wasimchafue raisi na familia yake huko sio kuishiwa wanadhani watawatoa mafisadi ndani ya chama bila kuandaa mkakati kamili itawarudi na itakuwa mbaya sana ,hawajatulia maana vijana vyuo vikuu,nara uvccm,makonda sekretariati wote na matamko ya kuropoka ropoka tuu ili kuchanganya wanachi wamejidharaulisha kweli
   
 9. D

  Dr Willibrod Slaa Verified User

  #9
  Apr 17, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 675
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 60
  Kafiribangi,

  Ni dakika chache tu nimeingia kutoka Kaliua na Urambo. Tumekuwa na mikutano mitatu ya hadhara, tumefungua ofisi na matawi ya Chama. Hivyo si kweli kuwa Chadema inalipiza kisasi kwa CCM.

  1)Kwanza inaelekea wengi hawafahamu malengo ya mikutano ya vijijini, na hasa kwa kuwa wanapata magazeti, wanatazama TV wanaamini Watanzania wote wanafanana. Lengo la Chadema katika hatua hii siyo kuwaambia CCM mbinu ya kuleta maendeleo wala kuwapa mikakati ya maendeleo. Ikumbukwe kuwa Chadema haikusanyi kodi yeyote ya wananchi na hivyo katika kipindi katika ya Uchaguzi kazi ya Chama cha siasa ni kujijenga kwa uchaguzi ujao,kukosoa Serikali iliyoko madarakani katika sera,Ilani na utekelezaji wa sera na ilani hiyo,kwa lengo la kuwaelimisha wananchi kuelewa udhaifu wa Chama hicho Tawala ili katika uchaguzi ujao tuiondoe. Hii ndiyo kazi yetu ya kikatiba. Chama cha siasa chenye kujua wajibu wake hakiwezi kuwa wasindikizaji tu. Sisi si washauri wa Serikali kwa kuipatia mbinu za kuongoza au mikakati ya kuongza na kuleta maendeleo. Kama yuko anayefikiri hivyo ni vema arejea vizuri majukumu ya vyama vya siasa.

  2)Sisi tunaofika vizuri ndio tuko kwenye mazingira ya kutafsiri nini kizungumzwe katika kijiji fulani tofauti na kingine. Hii inatokana na uelewa unaotofautiana. Katika kijiji kingine hata ajenda iliyokwisha kuzoeleka kwa watu wa vijijini kama Listi of Shame iliyotolewa 2007 inabidi itolewe upya kwa kuwa wananchi hawajawahi kujua ni kwanini nchi yeny utajiri mkubwa kama TZ inaweza kuwa maskini, au inakuwaje wako wanaoogelea katika utajiri mkubwa wakati wao hawana zahanati, maji, wanakula mlo mmoja bila kujua kuwa inatokana na rasilimali nyingi kutafunwa na mafisadi. Najua wako ambao wanaumia kwa sababu zao kila tunapowataja mafisadi, lakini katika mazingira kama hayo Mwanasiasa makini ni yule anayejua mahitaji ya wananchi wake. Hivyo, Msishangae wana JF kuona tunayarudia yale yale. Mtakuwa wabinafsi iwapo hamtapenda watanzania wenzenu wayajue mnayoyajua nyie.

  3) WanaJF wako katika jamvihili wanaoishi dunia yao wenyewe, au kwa kutaka au kwa bahati mbaya. Mathalan, nimestuka sana, kama niliyoelezwa Kaliua ni ya kweli Tanzania kuna ndugu zetu wanaishi bado Tanganyika ni si mwaka 47. Kaliua mtu mmoja aliyetajwa kama Baraka,mtoto wa Kapuya amekuwa tishio kwa wana Kaliua wote.Wanakaliua wanapigwa,wanachomewa nyumba, wanauawa na wakilalamika polisi nao inafyata kutokana baba Baraka kuwa tishio. Katika mazingira kama hayo usifikirie utazungumzia maendeleo zaidi ya kuwajengea ujasiri,mbinu za ukombozi na hata kuwafafanulia ufisadi mkubwa katika Jimbo kama hilo. Haiingii akilini mwa yeyote, kwa umaskini mkubwa tulioona Kaliua, na bado 72 Millioni zimetafunwa kwa jina la au kupitia kasma ya Mishahara (mishahara hewa, mishahara kulipwa kwa watumishi waliofariki, waliofukuzewa watoro n.k.) Kwa bahati mbaya hata tunapokuwa na Waandishi wa habari katika ziara mazingira na hotuba kama hizo hazipati nafasi kwa sababu yeyote ile, au hata kwa vile tu mwandishi anachagua anayotaka yeye.

  Hali inatisha, ndiyo maana Chadema tumedhamiria kutoa elimu katika vijiji mbalimbali kati ya sasa na 2015. Wanaoumia na hiyo waumie tu. Wananchi wengi vijijini ndicho wanachohitaji kwa CCM siku mmoja haitawapa elimu hiyo. Wilaya/Jimbo Maskini kama Kaliua haingii akilini inapotokea Halmashauri inashindwa kutumia Tshs 659,697 Millioni katika mwaka wa Fedha, na hatimaye isionekane katika B/F kwa kuwa mfumo wa uhasibu wa almashauri hauna utaratibu huo. Matokeo yake hakuna anayejua fedha hizo zimeenda wapi. Kama Madfiwani wa Kamati ya Fedha hawajapangia matumizi ni nani anapangia matumizi. Kama Chadema hatutakemea ufisadi wa namna hiyo nani akemee. Ikumbukwe hii ni wilaya iliyokuwa hadi mwaka wa ukaguzi yaani Juni 30, 2010, mawaziri wawili na Spika wa Bunge.

  Ndugu zangu wengine kwenye jamvi hili wanazungumza tu nadharia bila kujua hali halisi ya nchi yetu, au kwa makusudi tu wanataka kutuondoa kwenye ajenda zetu. Hatoki mtu hapa "ngo"(kwa lugha ya kina Kombani. Atakuwa mwanasiasa wa ajabu ambaye anahutubia mbele ya Ofisi ya "Spika" iliyojengwa Urambo, wakati Urambo haina Bunge na hivyo haina Spika. Hii ni ofisi iliyojengwa kwa milioni zaidi ya 300 na kuwekewa fenicha ya zaidi ya 170 Millioni, katika jimbo ambalo hakuna zahanati, vituo vya afya n.k. Mwanasiasa atakayeacha kutaja Ufisadi huu kwa kuwa wanaJamvi wachache wadhani wamechoka kusikia habari ya ufisadi atakuwa siyo mwanasiasa Makini. Kafiribigiri,naamini nimeeleweka.

  Tushuke chini, tusidhani maisha ndani ya jamvi hili ndivyo yalivyo vijijini. Hata kama sisi tuna maisha mazuri, tuwafikirie wazazi wetu,shangazi zetu,wajomba zetu ambao bado wanaishi nyumba za tembe na majani, ambao mlo wa siku ni shida, ambao wameacha kula nyama kwa kuwa bei haishikiki nakadhalika. Hizi ni ajenda za kudumu na ndiyo namna ya kuondoa umaskini wa wananchi wetu kwa kuikaba serikali ngazio zote iache ufisadi na ielekeze rasilimali zote kuwahudumia wananchi badala ya kujijengea mahekalu, kutembelea mashangingi ya millioni 500. Hii ndiyo ajenda,inaewzerkana wewe huipendi lakini vijijini ndiyo mambo yenye "mshiko"

   
 10. Freema Agyeman

  Freema Agyeman JF-Expert Member

  #10
  Apr 17, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,284
  Likes Received: 1,432
  Trophy Points: 280
  Dr, with all due respect naomba urekebishe post yako kwa kuweka paragraph. Ukichapa kwenye ms word ukapost hapa format inabadilika kidogo.
   
 11. n

  niweze JF-Expert Member

  #11
  Apr 17, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  I think you are missing a major point that Chadema is fighting for changes in Tanzania. Siwezi kuita Hoja za kudai Katiba ya Watanzania, Vita dhidi ya Corruption ni Vita vya eye for an eye. Ni wrong to assume that Chadema don't care about the country while we all in pain na Tumefanikiwa Kusimamisha Katiba ya Kikwete na Kikubwa Tumeua ccm. Focus on Issues sio Ushabiki.
   
 12. m

  mwanza_kwetu JF-Expert Member

  #12
  Apr 17, 2011
  Joined: Mar 2, 2011
  Messages: 684
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Dr Slaa kwa kweli sisi tuko nyuma yako umefafanua kwa umakini mkubwa; Dr tunaomba sana ujasiri na msimamo hhuu uendelee hadi Tanzania tupate uhuru tena; maisha ya ndugu zangu huko mwanza vijijini mfano ni mabaya wanategemea mvua tu ili maisha yaende wanachofanyiwa zaidi ni kuwatisha ili waogope upinzani hata kama wamepigika; hakika napata faraja kubwa sana kwa jinsi unavyoshughulika Dr Slaa. Usikate tamaa; pls songa mbele; songa mbele; Mungu yu pamoja na wewe pamoja na timu nzima ya chadema. Mwitikio wa huko sijui ukoje lakini naomba wana wa Tanzania kuunga mkono mageuzi haya mwanzo mwisho
   
 13. m

  mwanza_kwetu JF-Expert Member

  #13
  Apr 17, 2011
  Joined: Mar 2, 2011
  Messages: 684
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hujaelewa nini usiku huu
   
 14. Freema Agyeman

  Freema Agyeman JF-Expert Member

  #14
  Apr 17, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 3,284
  Likes Received: 1,432
  Trophy Points: 280
  Sijasema sijaelewa, una makengeza nini usiku huu.

  Back to the topic.
   
 15. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #15
  Apr 18, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  CCM naona mnaikadiria kwa kujilidhisha tu hapa JF! Slaa mtu mzima amewambia JF mnaweza kundelea kushabikia tu na yakajirudia yale yale! Akiamanisha kupigwa tena 2015! Watu mnaanza kujadili CCM kushindwa mwaka 2015 leo! Kwani ni muda gani tangu CCM imepata ushindi wa kutosha kwa Wabunge na upinzani kupa viti 50 tu kati ya 300+,JF isipo angalia tutabaki watu wa kushadadia tu na kushabikia tukijiaminisha CCM imedhoofika! Nashauri tuwape mkakati CDM na sio kujiridhisha kwa ushabiki tukaja shinda tena 2015 tukasingizia kuchakachua! Komaeni kisiasa na sio ushabiki tu pasipo kutoa ushauri kwa wapiganaji wetu!
   
 16. m

  mwanza_kwetu JF-Expert Member

  #16
  Apr 18, 2011
  Joined: Mar 2, 2011
  Messages: 684
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Toa point sio kuongelea mapambo; ujumbe umeelewa? then jadili ujumbe Dr Ana kazi nyingi na wana Tabora na wewe uwe unachanganya na za kwako pia
   
 17. m

  mwanza_kwetu JF-Expert Member

  #17
  Apr 18, 2011
  Joined: Mar 2, 2011
  Messages: 684
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Agree

  CDM
  1. wawe na radio
  2. wawe na TV ya mlengo wao
  3. mkakati wao wa kwenda kijijini mhimu sana na uendelezwe bila kuchoka
  4.bunge liendeleze vita kali sana ya utalaam ili activity yao iweze ku-outpay ccm na wingi wao; ref Lisu yesterday
  5. kuongeza kada za aina na jamii zote kuanzia wasomi hadi wakulima na wajisikie wako huru na salamanhuko na waone huyo ndio mkombozi
  6. waongeze na washinde propaganda ya Amani ambayo inatumia miaka yote na CCM; wapewe wananchi ujasiri kwa amani ili waone huko kuna amani maneno ya ccm yasiwe na guvu na kuepuka uhuni wa ccm ktk hilo
  7. etc
   
 18. D

  Dr Willibrod Slaa Verified User

  #18
  Apr 18, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 675
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 60
  Mwanza Kwetu,
  Thanks a lot. Ushauri umepokelewa na ninakuhakikishia yote yanafanyiwa kazi. Usichoke, na wana JF msichoke kutushauri. Ukombozi ni wetu sote na jamii yetu. Nguvu ya umma ni pamoja na mchango wa kila mmoja wetu. Thhanks a lot. Kesho tuko Jimbo laa Bukene na Nzega na Kesho kutwa tunaingia Igunga. Tusindikizane wote.

   
 19. mwana wa mtu

  mwana wa mtu JF-Expert Member

  #19
  Apr 18, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 220
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Dr Slaa, well said....huo ndio ukweli wilaya nyingi hapa Tanzania ambazo zimekuwa na mawaziri, wabunge etc ambao 'wanaheshimika' na maarufu karibu Tanzania nzima, ni wilaya maskini za kutupwa..nendeni Sumbawanga, Nkasi(kina Kimiti,Mzindakaya..)..hali ni mbaya, twende hiyo mikoa ya Tabora,Shinyanga, etc(ambako madini yamejaa-tumewasikia siku nyingi kina Msekela,Kapuya, etc)-hali za maisha ni duni sana...twende sehemu za kusini n.k....wananchi wapewe elimu,na kuweza kutambua kuwa 'hawastahili kuishi maisha wanayoishi,' watoke katika lindi la 'KURIDHIKA NA HALI HIZO DUNI'....
   
 20. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #20
  Apr 18, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,445
  Likes Received: 19,811
  Trophy Points: 280
  Je , nani anatakiwa kumtoa Lowasa kamati Ulinzi na Usalama? au ufisadi ni ndani ya chama tu? sijui nani anaweza kujibu hili swali
   
Loading...