Tabora: Dk Slaa ataja orodha mpya ya mafisadi!

Status
Not open for further replies.
Nape ajue CCM bila Mwl.J.K.N haiwezi,watabisha,watagangangamala,watajivua mpaka nguo lakini hawataweza tena..katu ccm haipo tena,

binafsi nikishukuru kwa dhati kabisa chama chetu CDM kwa kusikia wito wetu wanachama kuja Tabora,tunaomba wafanye kweli mpaka wilaya mbovu kabisa ya SIKONGE,...VIVA CHADEMA,VIVA TABORA!
 
Huu sasa uchokozi watu wameshajivua gamba chokochoko za nini. Ngoja tusibiri tuone itakavyokuwa inawezeka kweli bado kuna mafisadi wamejificha ndani ya chama ukizingatia tumeambia orodha ni mpya.
 
Nape Nauye kaingia na spidi ya zile radio zilizowahi kutolewa na coca cola ambazo hazitumii betri, badala yake zinatumia mfumo fulani wa kunyonga gurudumu, nadhani wale tulokuwepo enzi hizo mnazikumbuka. Redio hizo zilikuwa zinalia vizuri tu kwenye dakika za mwanzo. Lakini muda ulivyokwenda sauti inazidi kupungua na mwisho kuzima kabisa. Mpaka ujaze tena.

Sasa na huyu jamaa yenu Nnauye ndivyo alivyoingia, anapiga kelele sana sasa hivi ili kuwaridhisha walompa hilo chaka. Mpeni muda mtamwona ataishiwa hata neno la kuongea, maana hana timu.

Anataka tuamini kwamba kubadili CC ndo chama kimekuwa kisafi!! Anamdanganya nani?? Mafisadi wote bado wamo ndani ya chama na wengi wamo serikalini ambao hawajaguswa kabisa.

Nnauye ajue kwamba Daktari akishaugua na kuzidiwa atahitaji daktari mwingine wa kumtibu. Hatajitibu. CCM imeugua na haiwezi kujitibu haya maradhi ya ufisadi, lazima chama mbadala kitibu haya maradhi. Walipofikia panatosha.
 
Nape, ina maana unakiri mlikuwa mnacheza ngoma ya CHADEMA kabla ya kuvua magamba?
Kwa vile CHADEMA ni chama makini na kinatetea masilahi ya wananchi walalahoi,kupambana na mafisadi ambapo CCM chama tawala kimejaa mafisadi na kutetea mafisadi.CCM WATAENDELEA KUCHEZA NGOMA YA CHADEMA MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Huyo slaa angeanza kutaja mafisadi waliyomo ndani ya chama chake! Hii kukimbilia kujitia anajua sana mambo ya CCM ni kutafuta ujiko usio na mshiko!

Wewe uwataje maana hakuna mtu ajihukumuye peke mwenyewe, vinginevyo utaonekana hajajiandaa kutoa mchango hapa JF.
 
Huyo slaa kaishiwa ile mbaya! Ndio maana anatafuta namna ya kutoka tena... Jiandaeni kupata pumba zaidi toka kwake!
CCM tumeshawazoea awali mlisema CCM haina msamiati wa neno fisadi leo kwenye vikao vyenu limekuwa sala ya kufungulia mikutano kuanzia m/kiti wenu hadi washikilia mapembe.
 
Ikiwa tunangoja ccm watimize ahadi yao ili sisi wananchi tuone nani fisadi, wavukazane ndani ya chama tutoke kwenye kucha ya mafisadi. dk slaa huyo kutochanganya.
Hana uvumilivu, subira hili linatufanya tuanze kuamini uwezo wake wa kuongozataifa kubwa tz likawa salama. kauli ya Msajili wa vyama vya siasa kuhusu dk slaa inaanza kuonekana
hekima ni kitu muhimu, subira ni muhimu pia.
 
Ikiwa tunangoja ccm watimize ahadi yao ili sisi wananchi tuone nani fisadi, tutoke kwenye kucha ya mafisadi. dk slaa huyo kutochanga.
Hana uvumilivu, subira hili linatufanya tuanze kuamini uwezo wake wa kuongozataifa kubwa tz likawa salama. kauli ya Msajili wa vyama vya siasa kuhusu dk slaa inaanza kuonekana
hekima ni kitu muhimu, subira ni muhimu pia.

Holy crap!
 
sasa Kikwete na Slaa nani mwenye busara?au nani mwenye subira? mawazo ya wezi wa kura siku zote yako kama yako...
 
Sitashangaa kusikia Bashe, Martina (jina la kike kwa mwanamme) Nape na Makamba pamoja na JK(kwa mara ya pili) nimefurahi kusikia CCM wakisema, watuhumiwa wa ufisadi, kwa kweli neno hilo au watuhumiwa hao wametuhumiwa na CDM so CCM wanatekeleza sera za CDM! nimeipenda sanaaaa! Big Up cdm
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom