Table manners

Table manners

😀😀😀

Thanks for making up my day...lol!
The pleasure has been all mine. Worry not though should you ever decide to invite for dinner I do know how to use knife and fork though I will forever prefer my hands to any other cutlery.
 
  • Thanks
Reactions: kui
Hahaha umenifurahisha sana mm pia napenda kumla kuku kwa mkono
Cku moja nlkuwa mahala akaja dada mmja na jamaa akaagiza wali samaki alikuwa anapata shida kumla samaki hadi huruma,nkajisemea c amle kwa mkono tu?
hahahhaa!sijikalifishi nafsi hata Siku moja!!
 
Wakuu, na wale tunaokula kwa kutumia mikono, table manner yetu ni kama ifuatavyo:

1. Usimege ugali kwa mkono wa kushoto.

2. Using'ate ugali kwa meno kisha kuchovya tonge hilo kwenye bakuri hasa mnapokula kwa kushirikiana (kushare) chakula kwenye sahani moja.

3. Ukinawa mikono kabla na baada ya kula usi-shake mikono yako....acha maji yakauke kwa hewa yenyewe.

4. Usikombe au kunywa mboga mboga.

5. Ukila nyama au kuku usisukutue mdomo wala kupiga mswaki. Fanya hivyo pale tu unapokula mboga za majani au mboga nyingine sizisoeleweka.
 
Kha!hizi mambo sisi wandengereko hazituhusu kwa kweli !mwendo lete maji ya kunawa ,finyanga tonge poteza !kamata paja ng'ata peleka pwani! Na kama nguna kwa ndondo kata tonge ,design shimo moja matata jaza ndondo peleka pwani tena sio kimyakimya hapo hadithi kibao mmezunguka plate!
 
Wakuu, na wale tunaokula kwa kutumia mikono, table manner yetu ni kama ifuatavyo:

1. Usimege ugali kwa mkono wa kushoto.

2. Using'ate ugali kwa meno kisha kuchovya tonge hilo kwenye bakuri hasa mnapokula kwa kushirikiana (kushare) chakula kwenye sahani moja.

3. Ukinawa mikono kabla na baada ya kula usi-shake mikono yako....acha maji yakauke kwa hewa yenyewe.

4. Usikombe au kunywa mboga mboga.

5. Ukila nyama au kuku usisukutue mdomo wala kupiga mswaki. Fanya hivyo pale tu unapokula mboga za majani au mboga nyingine sizisoeleweka.

Katika vitu ambavyo huwa sitaki kujibania kwenye msosi huwa ni mboga, bora mboga izidi ugali au chchte
 
Safi sana ila hii inatumika kwa elite families. Ninafikiria zile familia ambazo zinasubiri ugali kwa samaki wadogo a.k.a vidagaaa. Ukweli hata viongozi wetu wanapopata madaraka inabidi wafundishwe table manners maana wengine walizoea wakirudi wanakuta msosi kwa hot pot na sahani na kijiko tu kama ni chakula cha kijiko au beseni na kajaji ka kunawia kama ni ule ugali wetu pendwa. Kwa misingi hii kwa Tanzania yetu naweza kusema pangine ni 5% ya population wanazingatia yote uliyosema kuhusu table manners and arrangements of cutlery.
 
Ukishamaliza kula hizi ndio sign language unayotumia.
download.jpg
 
Mmmmh! Hadi kula kuna sheria! Hayo makorokoro yooote nitashiba lini, unanawa mikono unapiga kitu, kwisha habari.


..hehe, atoto unakuwa kama yule mdau aliyesema akitumia uma na kisu hashibi.
 
Mkuu shukrani, u
Kawaida unapokaribishwa chakula mwenyeji anatakakwa aanze kuweka chakula mdomoni labda ilwe imeruhusiwa vingine. Mwenyeji anaanza kula baada ya wageni wote kuweka chakula kwenye sahani na wote wamekaa mezani. Chakula lazima kionjwe kabla hujaongeza chumvi na pilipili. Kuongeza chumvi au pilipili kabla ya kuonja ni kama dharau kwa mpishi au kuonyesha kuwa mpishi hajui kazi yake au huna imani nae. Inategemea na mkusanyiko wa watu, kama wana Imani basi baraka za chakula zitaanza kabla mwenyeji hajaweka chakula kinywani. Kama ni sherehe wageni wanaweza kuongeza maneno ya ucheshi mbele ya chakula na kumshukuru mwenyeji. Si tabia njema kuanza kula kabla watu wote hawajapata chakula na kuwa tayari kuanza kula.

Umma unashikwa mkono wa kushoto na kisu mkono wa kulia. Kisu mara nyingi kinakuwa chini, na kinatumka kukata chakula au kusaidia kuweka chakula kwenye umma. Kama kisu hakitumiki, umma unaweza kutumika kukita chakula kama vipande vya nyama au vipande vya viazi/chips. Usishike umma kama chepe na vidole kuvizungusha . Kwa kukita chakula umma unaweza kuudhibiti umma kwa kidole cha kunyooshea (cha pili kutoka gumba). Wakati wa kunywa supu, kijiko kinashikwa kwa mkono wa kulia. Kijiko kisiingie mdomoni chote, supu ivutwe kutoka kwenye kijiko bila kelele. Kisu kisisogelee mdomo au kulambwa. Chakula kinapotafunwa, mdomo uwe umefungwa, si tabia njema kuongea na chakula mdomoni, kulamba vidole au kula taratibu pia si uungwana.

Kama ni chakuila maalum (formal dinner) inakubalika kuweka siagi kutoka kwenye bakuli lake kutumia kisu kisu cha mkate na kuweka kwenye sahani ya pembeni. Hii itasaidia siagi kutoka kwenye bakuli kupata chenga za mikate wakati linazungushwa. Visu vitumike kupakia siagi lakini si kukata mkate na mikate inaweza kupasuliwa kati kati kwa kutumia mikono.

Mvinyo (wine) nyeupe au rose ishikiliwe kwenye glass iliyonyooka; nyekundu inakuwa kwenye glass pana. Mvinyo mweupe unapitishwa kabla ya mwekundu na wine nyepesi kabla ya nzito au mpya kabla ya yazamani (vintage). Kujimiminia wine inaruhusiwa kama mko wengi lakini ni tabia njema kuuliza watu wa upende wa pili kama watahitaji.


temp-in-video.jpg

Chakula mara nyingi kinakuwa katikati ya meza. Si uungwana kunyoosha mkono ufikie bakuli au sahani ya chakula, moumbe aliye karibu akusogezee. Kwa mpangilio huo huo chakula kipelekwe moja moja kwa yule aliyeomba. Si uungwa pia kutafuna kwa sauti, au kugonga uma na kisu kwenye sahani na kusababisha kelele.

Ukimaliza kula, kama ni formal dinner mnaweza kuongea na walaji wengine na kukubaliana kuwa mmemaliza, ukisubiri wahudumu, weka kisu na umma pamoja kwenye sahani kwa mpangilio wa saa kumi jioni, umma uwe chini ya kisu na ncha za umma ziangalie juu. Napkins ziwekwe juu ya meza bila kukunjwa chakula kinapokwisha.

Kwa chakula cha kifamilia, watoto wafundishwe kuomba ruhusa ya kuondoka mezani pindi wamalizapo chakula.

Simu za mkono au gadgets nyingine za kisasa hata gazeti au kitabu kiwekwe pembeni wakati wa chakula, kutext wakati wa kula, kuchat, kusoma kitabu au gazeti si uungwana. Kama kuna simu unaitegemea waeleze wenyeji na ikiita omba kutoka nje, fupisha maongezi na urudi ndani. Usicharge simu kwenye meza ya chakula hii si tabia njema.
table-set-jpg.382327
Mkuu shukrani, umenifundisha ustaarabu zaidi, ila kwenye kushika umma na Kijiko nashindwaga ku balance kwa sababu ni left handed, hayo mengine ni dhahabu, ahsante sana.
 
..hehe, atoto unakuwa kama yule mdau aliyesema akitumia uma na kisu hashibi.
Kuna kipindi tulikuwa tunakwenda mahali, acha tupewe semena ya table maners, aisee kidogo nighairi maana huo mlolongo! Lkn taratibu nikazoea.
Hawa wazungu wanatuletea balaa tu, maana hata hauli kwa amani unaogopa kukosea.
 
  • Thanks
Reactions: kui
Tatizo ni kwamba mnafanya maisha yawe magumu bila ya sababu, kuna haja gani Mtanzania kujua kula kwa uma na kisu wkt zaidi 98% ya Watanzania kwenye maisha yao ya kila hawahitaji umma na kisu kula?
Mtu mwenye akili hujadili mambo yenye faida na manufaa kwa jamii yake, mambo ambayo yataisaidia na kuiboresha jamii yake yaani mambo muhimu sasa kula na Uma na Kisu kuna umuhimu gani kwa Mtanzania? Isitoshe Wazungu ni watu waelewa sana na ndiyo maana ukimkaribisha kwako kama mnakula Ugali kwa mkono atakula kwa mkono na akikukaribisha kwake kama haujui kutumia uma na kisu siyo ishu kwa maana najua siyo utamaduni wako ...
Hao Watanzania 2% ndio wamelengwa hapa. Kama mzungu kaja kwako akakukuta unakula kwa mkono naye akala kwa mkono kwanini wewe ukienda kwake usile ki utamaduni wake? IQ kubwa hujengwa kujua masuala mengi tofauti tofauti. Huwezi kuwa na IQ kubwa kwa kujua tu namna ya kusaidia 98% ya Watanzania wasiotumia uma na kijiko wakati wa kula. Umefanya kitu gani katika jamii yako ambapo utaendelea kukumbukwa milele kama anavyoendelea kukumbukwa hayati Mwl. J. Nyerere?
 
Hao Watanzania 2% ndio wamelengwa hapa. Kama mzungu kaja kwako akakukuta unakula kwa mkono naye akala kwa mkono kwanini wewe ukienda kwake usile ki utamaduni wake? IQ kubwa hujengwa kujua masuala mengi tofauti tofauti. Huwezi kuwa na IQ kubwa kwa kujua tu namna ya kusaidia 98% ya Watanzania wasiotumia uma na kijiko wakati wa kula. Umefanya kitu gani katika jamii yako ambapo utaendelea kukumbukwa milele kama anavyoendelea kukumbukwa hayati Mwl. J. Nyerere?


Ni ujinga kwa sababu hao chini ya 2% hawahitaji kufundishwa kutumia uma na kisu kwani wanajua tayari!
 
Back
Top Bottom