Table manners

Table manners

Hii mada nimeipenda sana hongera mkuu.Binafsi nikikaribishwa chakula kwa mtu anatakiwa aanze kula yeye...naogopa sana kuediti mapishi, atakama chumvi imezid au kupungua nitakuwa mvumilivu tu na kula hivyo hivyo...hiyo aya ya mwisho nafikiri ni muhimu mno.
BWANA WEE KUNA WATU WANA MAJIBU SANA MEZANI..UTASIKIA "MICHUMVI CHUMVI TUU".WAKATI KUJUA KUPIKA NI KWIKWI,HATA BAKULI KUOSHA TABU.NAKUMBUKA TULIMKARIBISHA MGENI ,ALIKICHAMBUA CHAKULA MPAKA TUKAJUTA.EDIT CHAKULA UKIWA UNAJUA NA SI UKOSEWE UKIWA UPO MEZANI,FANYA HIVI SIKU YA PILI KAMA NI MKE AU MUME NENDA JIKONI NA UONESHE USTADI WAKO.KAMA UNA MKE AU MUME MWELEWA ATAKUKUBALI SANA.KWA AFRIKA NI BAADHI TU WANAWEZA HAYO.
 
Ungesema Table manners za kizungu...Mfano hizo utensils zote ni za kizungu. Sasa kama jinsi ya kuzitumia nayo sehemu ya "table manners" basi hizo "table manners" ni za kizungu...Hii ni "Effect of Neo-colonialism"...Ukienda Japan hutakuta wanatumia hizo principle/manners ulizozitaja..Wana utamaduni wao tofauti. Na unakuta wanakula kwa namna ya tofauti. Ila wewe unaishi utamaduni wa watu wengine na unajaribu kuutangaza..
Ninaelewa na kama mnataka nilete za Kijapan nitazileta, nilidhani hizi ni ziko more genera as we are part of the Common Wealth.
 
vizuri
na ni vyema wamama wakawafunza watoto wao haya mambo mapema sana
Ni kweli hata kuwapeleka hotelini mara moja moja, usingoje msichana anafika University ndiyo anaumbuka kwenye first date.
 
Adabu za kuanza kula chakula kwa Muislam ni:-
1. Kunawa mikono yako yote miwili kabla ya kuanza kula.
2. Kumtaja Mwenyezi Mungu kwa kusema ‘BismiLlaah’ (Jina la Allaah Subhanau Wa taala).
3. Kula kwa mkono wa kulia na kula kilicho mbele ya sahani upande wako kama mnakula kwa pamoja.
4. Inapendekezwa kukaa chini ( kwenye mkeka/ jamvi) ukiwa umekunja miguu.
5. Kuacha kuongea / mazungumzo wakati wa mlo.
6. Kumshukuru Mwenyezi Mungu baada ya kula na utamshukuru mwenyeji wako/ aliyeandaa chakula na kumwombea dua.

Nimewalilisha. Ahsanteni
Asante mkuu tumekupata.
 
Ehh mambo ya kizungu on fleek...tunashukuru mana mashikoro mageniii
 
BWANA WEE KUNA WATU WANA MAJIBU SANA MEZANI..UTASIKIA "MICHUMVI CHUMVI TUU".WAKATI KUJUA KUPIKA NI KWIKWI,HATA BAKULI KUOSHA TABU.NAKUMBUKA TULIMKARIBISHA MGENI ,ALIKICHAMBUA CHAKULA MPAKA TUKAJUTA.EDIT CHAKULA UKIWA UNAJUA NA SI UKOSEWE UKIWA UPO MEZANI,FANYA HIVI SIKU YA PILI KAMA NI MKE AU MUME NENDA JIKONI NA UONESHE USTADI WAKO.KAMA UNA MKE AU MUME MWELEWA ATAKUKUBALI SANA.KWA AFRIKA NI BAADHI TU WANAWEZA HAYO.
Kweli kabisa mkuu mezani tunakula kilichopo kwa amani...jikoni tunafundishana kwa uvumilivu.
 
Teh Teh huu ni utani karibu na kweli aisee
Shost aliniambia date alipelekwa dinner sehemu, akashika bakuli la supu na kuanza kuria, akamuona jamaa anaangaza macho, salad ilikuja letuce, nyanya na vipande vya mayai ya kuchemsha, mdada alikamata kwa mkono. Baada ya hapo kila akipiga simu jamaa hapokei.😀😀
 
Shost aliniambia date alipelekwa dinner sehemu, akashika bakuli la supu na kuanza kuria, akamuana jamaa anaangaza macho, salad ilikuja letuce, nyanya na vipande vya mayai ya kuchemsha, mdada alikamata kwa mkono. Baada ya hapo kila akipiga simu jamaa hapokei.😀😀
He he he sasa afanyaje mwee. Ila jamaa naye, hivyo si vitu vya kufundishana tu. Ni bora mtu aagize chakula ambacho amekizoea na hakina mbwembwe kuliwa
 
  • Thanks
Reactions: kui
mkono wa kukamatia umma na kisu unategemeana na imani ya mtu..unaweza kushika umma kwa mkono wa kulia kwa sababu imani nyengine kula kwa mkono wa kushoto ni taboo
 
Nawa mikono yako vizuri, futa maji kwa kitambaa, chukua sahani yako,weka chakula kadiri ya mahitaji yako baada ya hapo soma dua/neno anza kukandamiza kwa mikono yako kimya kimya bila maongezi ukimaliza nawa vema mikono yako na umshukuru Mungu kwa chakula alichokujalia. Inatosha
upo sahihi uzungu tuwaachie wenyewe..watu wanashindwa kuelewa tu hata vyakula vyetu vya kiafrika sio rafiki kwa kuliwa kwa umma na kisu
 
Kawaida unapokaribishwa chakula mwenyeji anatakakwa aanze kuweka chakula mdomoni labda ilwe imeruhusiwa vingine. Mwenyeji anaanza kula baada ya wageni wote kuweka chakula kwenye sahani na wote wamekaa mezani. Chakula lazima kionjwe kabla hujaongeza chumvi na pilipili. Kuongeza chumvi au pilipili kabla ya kuonja ni kama dharau kwa mpishi au kuonyesha kuwa mpishi hajui kazi yake au huna imani nae. Inategemea na mkusanyiko wa watu, kama wana Imani basi baraka za chakula zitaanza kabla mwenyeji hajaweka chakula kinywani. Kama ni sherehe wageni wanaweza kuongeza maneno ya ucheshi mbele ya chakula na kumshukuru mwenyeji. Si tabia njema kuanza kula kabla watu wote hawajapata chakula na kuwa tayari kuanza kula.

Umma unashikwa mkono wa kushoto na kisu mkono wa kulia. Kisu mara nyingi kinakuwa chini, na kinatumka kukata chakula au kusaidia kuweka chakula kwenye umma. Kama kisu hakitumiki, umma unaweza kutumika kukita chakula kama vipande vya nyama au vipande vya viazi/chips. Usishike umma kama chepe na vidole kuvizungusha . Kwa kukita chakula umma unaweza kuudhibiti umma kwa kidole cha kunyooshea (cha pili kutoka gumba). Wakati wa kunywa supu, kijiko kinashikwa kwa mkono wa kulia. Kijiko kisiingie mdomoni chote, supu ivutwe kutoka kwenye kijiko bila kelele. Kisu kisisogelee mdomo au kulambwa. Chakula kinapotafunwa, mdomo uwe umefungwa, si tabia njema kuongea na chakula mdomoni, kulamba vidole au kula taratibu pia si uungwana.

Kama ni chakuila maalum (formal dinner) inakubalika kuweka siagi kutoka kwenye bakuli lake kutumia kisu kisu cha mkate na kuweka kwenye sahani ya pembeni. Hii itasaidia siagi kutoka kwenye bakuli kupata chenga za mikate wakati linazungushwa. Visu vitumike kupakia siagi lakini si kukata mkate na mikate inaweza kupasuliwa kati kati kwa kutumia mikono.

Mvinyo (wine) nyeupe au rose ishikiliwe kwenye glass iliyonyooka; nyekundu inakuwa kwenye glass pana. Mvinyo mweupe unapitishwa kabla ya mwekundu na wine nyepesi kabla ya nzito au mpya kabla ya yazamani (vintage). Kujimiminia wine inaruhusiwa kama mko wengi lakini ni tabia njema kuuliza watu wa upende wa pili kama watahitaji.

temp-in-video.jpg

Chakula mara nyingi kinakuwa katikati ya meza. Si uungwana kunyoosha mkono ufikie bakuli au sahani ya chakula, moumbe aliye karibu akusogezee. Kwa mpangilio huo huo chakula kipelekwe moja moja kwa yule aliyeomba. Si uungwa pia kutafuna kwa sauti, au kugonga uma na kisu kwenye sahani na kusababisha kelele.

Ukimaliza kula, kama ni formal dinner mnaweza kuongea na walaji wengine na kukubaliana kuwa mmemaliza, ukisubiri wahudumu, weka kisu na umma pamoja kwenye sahani kwa mpangilio wa saa kumi jioni, umma uwe chini ya kisu na ncha za umma ziangalie juu. Napkins ziwekwe juu ya meza bila kukunjwa chakula kinapokwisha.

Kwa chakula cha kifamilia, watoto wafundishwe kuomba ruhusa ya kuondoka mezani pindi wamalizapo chakula.

Simu za mkono au gadgets nyingine za kisasa hata gazeti au kitabu kiwekwe pembeni wakati wa chakula, kutext wakati wa kula, kuchat, kusoma kitabu au gazeti si uungwana. Kama kuna simu unaitegemea waeleze wenyeji na ikiita omba kutoka nje, fupisha maongezi na urudi ndani. Usicharge simu kwenye meza ya chakula hii si tabia njema.
table-set-jpg.382327
Jifunze kusummarize ...rihabari rilefu kama nini.wala siwezi poteza muda wangu kusoma
 
duh we ni kabila gani?
 
Back
Top Bottom