Kawaida unapokaribishwa chakula mwenyeji anatakakwa aanze kuweka chakula mdomoni labda ilwe imeruhusiwa vingine. Mwenyeji anaanza kula baada ya wageni wote kuweka chakula kwenye sahani na wote wamekaa mezani. Chakula lazima kionjwe kabla hujaongeza chumvi na pilipili. Kuongeza chumvi au pilipili kabla ya kuonja ni kama dharau kwa mpishi au kuonyesha kuwa mpishi hajui kazi yake au huna imani nae. Inategemea na mkusanyiko wa watu, kama wana Imani basi baraka za chakula zitaanza kabla mwenyeji hajaweka chakula kinywani. Kama ni sherehe wageni wanaweza kuongeza maneno ya ucheshi mbele ya chakula na kumshukuru mwenyeji. Si tabia njema kuanza kula kabla watu wote hawajapata chakula na kuwa tayari kuanza kula.
Umma unashikwa mkono wa kushoto na kisu mkono wa kulia. Kisu mara nyingi kinakuwa chini, na kinatumka kukata chakula au kusaidia kuweka chakula kwenye umma. Kama kisu hakitumiki, umma unaweza kutumika kukita chakula kama vipande vya nyama au vipande vya viazi/chips. Usishike umma kama chepe na vidole kuvizungusha . Kwa kukita chakula umma unaweza kuudhibiti umma kwa kidole cha kunyooshea (cha pili kutoka gumba). Wakati wa kunywa supu, kijiko kinashikwa kwa mkono wa kulia. Kijiko kisiingie mdomoni chote, supu ivutwe kutoka kwenye kijiko bila kelele. Kisu kisisogelee mdomo au kulambwa. Chakula kinapotafunwa, mdomo uwe umefungwa, si tabia njema kuongea na chakula mdomoni, kulamba vidole au kula taratibu pia si uungwana.
Kama ni chakuila maalum (formal dinner) inakubalika kuweka siagi kutoka kwenye bakuli lake kutumia kisu kisu cha mkate na kuweka kwenye sahani ya pembeni. Hii itasaidia siagi kutoka kwenye bakuli kupata chenga za mikate wakati linazungushwa. Visu vitumike kupakia siagi lakini si kukata mkate na mikate inaweza kupasuliwa kati kati kwa kutumia mikono.
Mvinyo (wine) nyeupe au rose ishikiliwe kwenye glass iliyonyooka; nyekundu inakuwa kwenye glass pana. Mvinyo mweupe unapitishwa kabla ya mwekundu na wine nyepesi kabla ya nzito au mpya kabla ya yazamani (vintage). Kujimiminia wine inaruhusiwa kama mko wengi lakini ni tabia njema kuuliza watu wa upende wa pili kama watahitaji.
Chakula mara nyingi kinakuwa katikati ya meza. Si uungwana kunyoosha mkono ufikie bakuli au sahani ya chakula, moumbe aliye karibu akusogezee. Kwa mpangilio huo huo chakula kipelekwe moja moja kwa yule aliyeomba. Si uungwa pia kutafuna kwa sauti, au kugonga uma na kisu kwenye sahani na kusababisha kelele.
Ukimaliza kula, kama ni formal dinner mnaweza kuongea na walaji wengine na kukubaliana kuwa mmemaliza, ukisubiri wahudumu, weka kisu na umma pamoja kwenye sahani kwa mpangilio wa saa kumi jioni, umma uwe chini ya kisu na ncha za umma ziangalie juu. Napkins ziwekwe juu ya meza bila kukunjwa chakula kinapokwisha.
Kwa chakula cha kifamilia, watoto wafundishwe kuomba ruhusa ya kuondoka mezani pindi wamalizapo chakula.
Simu za mkono au gadgets nyingine za kisasa hata gazeti au kitabu kiwekwe pembeni wakati wa chakula, kutext wakati wa kula, kuchat, kusoma kitabu au gazeti si uungwana. Kama kuna simu unaitegemea waeleze wenyeji na ikiita omba kutoka nje, fupisha maongezi na urudi ndani. Usicharge simu kwenye meza ya chakula hii si tabia njema.