Table manners

Table manners

Waafrika bhana sisi kweli takataka kwenye nchi ambayo watu hata wenye Meza ya kulia chakula nyumbani hawafiki 2% unakuja kuongelea ,,table manners" kula kwa uma na kisu? Duh! Hii ni IQ ndogo tu hakuna namna nyingine ya kulielezea sasa naelewa kwa nini fisadi Lowasa alisema Watanzania wakadownload kwenye computer ilani ya chadema, sisi ni watu wasio na akili kabisa kusema ukweli inasikitisha sana!


We mwenye IQ kubwa FYI, ukialikwa mahala kula sio uungwana kwenda mikono mitupu, ni vizuri kubeba zawadi kwa wenyeji wako mfano kinywaji.
 
We mwenye IQ kubwa, ukialikwa mahala kula sio uungwana kwenda mikono mitupu, ni vizuri kubeba zawadi kwa wenyeji wako mfano kinywaji.

Utamaduni wa wapi huwo?
 
umenikumbusha kitabu kinaitwa haifai. wanasema. usiongee na mtu ng'ambo ya meza, ukidondosha kijiko usiokote (omba kingine), usiweke viwiko juu ya meza, usijihuzunishe na kujitia kuboreka wakati wa kusubiri msosi, usivute mchuzi hadi kupiga mluzi........
 
umenikumbusha kitabu kinaitwa haifai. wanasema. usiongee na mtu ng'ambo ya meza, ukidondosha kijiko usiokote (omba kingine), usiweke viwiko juu ya meza, usijihuzunishe na kujitia kuboreka wakati wa kusubiri msosi, usivute mchuzi hadi kupiga mluzi........
Jamani endeleeni kutuelezea. Asante sana.
 
Sky Umenikumbusha hii clip ya Pretty Woman na hizi table manners, bidada karusha chakula kwenye formal dinner kwa kushindwa kushika kijiko maalum...lol!

Halafu
V. Where's the salad?
E. The salad comes at end of meal
V. That's the fork I know!... 😀


 
Mchumba naona umemaliza kila kitu, vipi unajua kupika lakn?
 
  • Thanks
Reactions: me1
Kuna siku nlikua mahali, nlikua na njaa nikapewa kuku (kidali) ilibidi nimle kwa mkono watu wakipita najifanya nimeshika umma na kisu, wakiondoka naendeleza kwa mkono
Tabu yote ya nini...ungenawa tu ule kwa amani.....

Ila wakati mwingine ndio maana naagizaga steki.....haina complication kama kuku...mara umegonga mfupa....
 
Hakuna kitu napenda kujifunza kama hivi,asante kwa darasa...
Nimepanua wigo wangu wa uelewa katika haya.
Cheers
 
Hahaha nishazoea kufinya kwa mkono mbona balaa. Hiyo siku ukae tu mbali maana hukawii kukuta uma umeslide hadi jichoni kwako, huku kyuku kimegomea kisu, kyuku chini. Ntamuokota mbona nimfute nimkandamize kwa mkono teh, wageni watanitimuaje teh teh
Hahahahaha itanitia aibu ujue....

Au ndio kila ukipeleka kisu unagonga sahani, kitu ti ti ti macho yote kwako...hahahahahah

Bora uombe radhi una allergy na silver+chuma....unawe uufinye
 
Kuna siku nlikua mahali, nlikua na njaa nikapewa kuku (kidali) ilibidi nimle kwa mkono watu wakipita najifanya nimeshika umma na kisu, wakiondoka naendeleza kwa mkono

Ninavyopenda kula kuku kwa mikono sasa
Uwiiiii
 
Hahahahaha itanitia aibu ujue....

Au ndio kila ukipeleka kisu unagonga sahani, kitu ti ti ti macho yote kwako...hahahahahah

Bora uombe radhi una allergy na silver+chuma....unawe uufinye
Aibu utaona wewe mbona lol.

Yani ntawaumiza masikio kwanza, maana ntagonga gonga sahani hadi ijute. Me ntamkata tu akidondoka namuokota, hadi nizoee, ntafanyaje sasa while nataka na me nisipitwe na table manners, nisije nikakosa dinner na wazungu lol
 
Sky Umenikumbusha hii clip ya Pretty Woman na hizi table manners, bidada karusha chakula kwenye formal dinner kwa kushindwa kushika kijiko maalum...lol!

Halafu
V. Where's the salad?
E. The salad comes at end of meal
V. That's the fork I know!... 😀



nilivyoona huu uzi na mimi nliliikumbuka hii movie. nyingine ni gangster squad. Sean Penn anahangaika na nyuma (forks).
 
  • Thanks
Reactions: kui
Aibu utaona wewe mbona lol.

Yani ntawaumiza masikio kwanza, maana ntagonga gonga sahani hadi ijute. Me ntamkata tu akidondoka namuokota, hadi nizoee, ntafanyaje sasa while nataka na me nisipitwe na table manners, nisije nikakosa dinner na wazungu lol
Hihiiiiiiii.
Yani macho yote yatakuwa kwako.....
Heri kula na mkono ti aisee...kwanza inafanya chakula iwe kitamu zaidi
 
Kawaida unapokaribishwa chakula mwenyeji anatakakwa aanze kuweka chakula mdomoni labda ilwe imeruhusiwa vingine. Mwenyeji anaanza kula baada ya wageni wote kuweka chakula kwenye sahani na wote wamekaa mezani. Chakula lazima kionjwe kabla hujaongeza chumvi na pilipili. Kuongeza chumvi au pilipili kabla ya kuonja ni kama dharau kwa mpishi au kuonyesha kuwa mpishi hajui kazi yake au huna imani nae. Inategemea na mkusanyiko wa watu, kama wana Imani basi baraka za chakula zitaanza kabla mwenyeji hajaweka chakula kinywani. Kama ni sherehe wageni wanaweza kuongeza maneno ya ucheshi mbele ya chakula na kumshukuru mwenyeji. Si tabia njema kuanza kula kabla watu wote hawajapata chakula na kuwa tayari kuanza kula.

Umma unashikwa mkono wa kushoto na kisu mkono wa kulia. Kisu mara nyingi kinakuwa chini, na kinatumka kukata chakula au kusaidia kuweka chakula kwenye umma. Kama kisu hakitumiki, umma unaweza kutumika kukita chakula kama vipande vya nyama au vipande vya viazi/chips. Usishike umma kama chepe na vidole kuvizungusha . Kwa kukita chakula umma unaweza kuudhibiti umma kwa kidole cha kunyooshea (cha pili kutoka gumba). Wakati wa kunywa supu, kijiko kinashikwa kwa mkono wa kulia. Kijiko kisiingie mdomoni chote, supu ivutwe kutoka kwenye kijiko bila kelele. Kisu kisisogelee mdomo au kulambwa. Chakula kinapotafunwa, mdomo uwe umefungwa, si tabia njema kuongea na chakula mdomoni, kulamba vidole au kula taratibu pia si uungwana.

Kama ni chakuila maalum (formal dinner) inakubalika kuweka siagi kutoka kwenye bakuli lake kutumia kisu kisu cha mkate na kuweka kwenye sahani ya pembeni. Hii itasaidia siagi kutoka kwenye bakuli kupata chenga za mikate wakati linazungushwa. Visu vitumike kupakia siagi lakini si kukata mkate na mikate inaweza kupasuliwa kati kati kwa kutumia mikono.

Mvinyo (wine) nyeupe au rose ishikiliwe kwenye glass iliyonyooka; nyekundu inakuwa kwenye glass pana. Mvinyo mweupe unapitishwa kabla ya mwekundu na wine nyepesi kabla ya nzito au mpya kabla ya yazamani (vintage). Kujimiminia wine inaruhusiwa kama mko wengi lakini ni tabia njema kuuliza watu wa upende wa pili kama watahitaji.


temp-in-video.jpg

Chakula mara nyingi kinakuwa katikati ya meza. Si uungwana kunyoosha mkono ufikie bakuli au sahani ya chakula, moumbe aliye karibu akusogezee. Kwa mpangilio huo huo chakula kipelekwe moja moja kwa yule aliyeomba. Si uungwa pia kutafuna kwa sauti, au kugonga uma na kisu kwenye sahani na kusababisha kelele.

Ukimaliza kula, kama ni formal dinner mnaweza kuongea na walaji wengine na kukubaliana kuwa mmemaliza, ukisubiri wahudumu, weka kisu na umma pamoja kwenye sahani kwa mpangilio wa saa kumi jioni, umma uwe chini ya kisu na ncha za umma ziangalie juu. Napkins ziwekwe juu ya meza bila kukunjwa chakula kinapokwisha.

Kwa chakula cha kifamilia, watoto wafundishwe kuomba ruhusa ya kuondoka mezani pindi wamalizapo chakula.

Simu za mkono au gadgets nyingine za kisasa hata gazeti au kitabu kiwekwe pembeni wakati wa chakula, kutext wakati wa kula, kuchat, kusoma kitabu au gazeti si uungwana. Kama kuna simu unaitegemea waeleze wenyeji na ikiita omba kutoka nje, fupisha maongezi na urudi ndani. Usicharge simu kwenye meza ya chakula hii si tabia njema.
table-set-jpg.382327
Ungesema Table manners za kizungu...Mfano hizo utensils zote ni za kizungu. Sasa kama jinsi ya kuzitumia nayo sehemu ya "table manners" basi hizo "table manners" ni za kizungu...Hii ni "Effect of Neo-colonialism"...Ukienda Japan hutakuta wanatumia hizo principle/manners ulizozitaja..Wana utamaduni wao tofauti. Na unakuta wanakula kwa namna ya tofauti. Ila wewe unaishi utamaduni wa watu wengine na unajaribu kuutangaza..
 
Back
Top Bottom