Mimi na dada wa kitanzania mwenye umri wa miaka 26, nilianza mahusiano na kijana mmoja ambaye hadi sasa tuna muda wa miez 5, kijana huyu analikua akionyesha kutonijali wakati tunaanza mahusiano mimi ndiyo nilikua nikililia attention yake mara nyingi na tuna kaa mji mmoja ala alikua hajali hata zikipita siku3-4 hatujaonana, hapo nikaanza mwambia ukweli akaniona mimi mlalamikaji tu, ikafika wakati nikamwambia nina mimba yake,(nia kujua ataamua nini, ila sikua na mimba kweli, (baada ya kujua afya zetu)), majibu yake yalikua ni kunishauri nikatoe mimba since hakuwa tayari kuwa na familia na anafanya kazi na ni mwanafunzi wa masomo ya masters, well nikampa ukweli kwamba sina mimba nilitaka jua maamuz yake na kama yupo siriaz since hapendi condomise.
Pili wakati tunajuana alinidanganya kuhusu habari zake binafsi, kuhusu amekulia wapi, kwamba yeye ni mgeni katika huu mji tuliokutana, only to find out ni mwenyeji sana, alisoma nini akiwa chuo pia, hivyo vyote alinidanganya na hata kuna wakati nilikua nikimkamata anaongea tofauti na alivyoniambia alibisha, then niliamua vunja uhusiano kwa hvyo vigezo, ila alikuja omba msamaha sana na sababu zake kama hakuwa tayari na majukum ya mtoto, alidanganya sababu ya mazingira tuliyokutana(social network).
Then recently alikuwa darasani kwake anaposoma akawa anaongea na wenzake ana mawazo sana kwamba mke wake anatarajia jifungua na nyumba ndogo inamsumbua kama vile hawaelewani.
Yeye yupo darasa moja mbele yangu, my colleagues they overheard akiwa anasema hivyo, mimi nikaingia darasani na wenzangu wakaanza kumrejea aliyokua akisema sababu kuna mmoja aliona ni kitendo cha ajabu mtu kuongea hivyo vitu mbele za watu kama kuwa na mpango wa kando ni jambo la kawaida sana, wale wenzangu wakamchambua sababu walianza nihadithia mimi, (but walikua hawajui kama namfaham vizuri), mimi nkapata shauku ya kujua ukweli ya hayo, well baadae nikamuuliza akakubali alisema hayo na kusema alikua akitania tu na si kweli kwamba ana mke.
Haya yote yametokea wakati ananiomba msamaha turudiane, na anasema yeye anataka kuwa siriaz na mimi na kupeleka uhusiano wetu mbali, ila nina mashaka kama ni mkweli na nilishaanza msamehe ila imani yangu imenitoweka na yeye.Nimesha msamehe ila kurudiana naona kigugumizi sababu hata mimi ni binadamu naweza kosea siku moja,
USHAURI WAKO WA BUSARA PLEASE,