Tabia zake utata mtupu

Tabia zake utata mtupu

Niendelee naye?

  • Ndiyo

    Votes: 2 28.6%
  • Hapana

    Votes: 5 71.4%

  • Total voters
    7
Hivi wote mnasema huyu kaka ni muongo lakini huyu dada aliyeanzisha thread je? Mimi nachukia sana wanawake wanaodanganya kuhusu kupata mimba, ni uongo mbaya sana. Ni unafiki kumsema mwenzako kwa kuwa muongo wakati wewe mwenyewe ni muongo. Wanawake acheni hiyo tabia chafu ya kupima wanaume kwa kuwadanganya kuhusu mimba.

Umepaniki mkuu imekutokea nin?
 
That bastard is lying thru his teeth...akili ku mkichwa mama kama wangoja hadi umkamate red handed basi endelea kusubiri
 
Sioni sababu ya kuomba ushauri ilihali maumivu unayoyapata ndo kipimo chako kuamua
 
Mimi na dada wa kitanzania mwenye umri wa miaka 26, nilianza mahusiano na kijana mmoja ambaye hadi sasa tuna muda wa miez 5, kijana huyu analikua akionyesha kutonijali wakati tunaanza mahusiano mimi ndiyo nilikua nikililia attention yake mara nyingi na tuna kaa mji mmoja ala alikua hajali hata zikipita siku3-4 hatujaonana, hapo nikaanza mwambia ukweli akaniona mimi mlalamikaji tu, ikafika wakati nikamwambia nina mimba yake,(nia kujua ataamua nini, ila sikua na mimba kweli, (baada ya kujua afya zetu)), majibu yake yalikua ni kunishauri nikatoe mimba since hakuwa tayari kuwa na familia na anafanya kazi na ni mwanafunzi wa masomo ya masters, well nikampa ukweli kwamba sina mimba nilitaka jua maamuz yake na kama yupo siriaz since hapendi condomise.

Pili wakati tunajuana alinidanganya kuhusu habari zake binafsi, kuhusu amekulia wapi, kwamba yeye ni mgeni katika huu mji tuliokutana, only to find out ni mwenyeji sana, alisoma nini akiwa chuo pia, hivyo vyote alinidanganya na hata kuna wakati nilikua nikimkamata anaongea tofauti na alivyoniambia alibisha, then niliamua vunja uhusiano kwa hvyo vigezo, ila alikuja omba msamaha sana na sababu zake kama hakuwa tayari na majukum ya mtoto, alidanganya sababu ya mazingira tuliyokutana(social network).

Then recently alikuwa darasani kwake anaposoma akawa anaongea na wenzake ana mawazo sana kwamba mke wake anatarajia jifungua na nyumba ndogo inamsumbua kama vile hawaelewani.

Yeye yupo darasa moja mbele yangu, my colleagues they overheard akiwa anasema hivyo, mimi nikaingia darasani na wenzangu wakaanza kumrejea aliyokua akisema sababu kuna mmoja aliona ni kitendo cha ajabu mtu kuongea hivyo vitu mbele za watu kama kuwa na mpango wa kando ni jambo la kawaida sana, wale wenzangu wakamchambua sababu walianza nihadithia mimi, (but walikua hawajui kama namfaham vizuri), mimi nkapata shauku ya kujua ukweli ya hayo, well baadae nikamuuliza akakubali alisema hayo na kusema alikua akitania tu na si kweli kwamba ana mke.

Haya yote yametokea wakati ananiomba msamaha turudiane, na anasema yeye anataka kuwa siriaz na mimi na kupeleka uhusiano wetu mbali, ila nina mashaka kama ni mkweli na nilishaanza msamehe ila imani yangu imenitoweka na yeye.Nimesha msamehe ila kurudiana naona kigugumizi sababu hata mimi ni binadamu naweza kosea siku moja,

USHAURI WAKO WA BUSARA PLEASE,

Ukiona mtu hakujali, basi hakuitaji. pole bi dada.
Anakuona unalazimisha penzi, na unamsumbua.
Kama angekua anakupenda au anakuitaji angekufuata.
wewe unamuhitaji ila yeye hakuitaji.
wewe unamtaka, ila yeye hakutaki. Samahani kwa maneno yangu, ila sasa vizuri unajua ukweli. funguka.

Wanawake wengine nyie munapenda kujitaftia matatizo sana.
Waswahili walisema dalili ya mvua ni mawingu.
Hachana nae, kuwa biz na masomo, sikiliza mziki, danse, tumia muda kufanya vitu muhim, hata kazi za kujitolea zipo, utamsau tu.
Atakae kupenda kweli na kukuitaji maishani mwake atajitokeza mwaka wowote ule na utaenjoy life, hadi utajuliza kwanini hakutokea mapema. Mvumilivu ula mbivu. kama ungekua na miaka 40 sawa, lakini ndio kwanza 26 tu? una muda mwingi ndugu yangu. husiwe na haraka haraka ya kupata mpenzi au mume, wengine mabomu
 
Kusoma hujui na picha pia ujui kutazama!!!!!!!!!! Hilo si fungu lako bi dada toka fasta kabla ujatoka na mengine pia
 
Ukiona mtu hakujali, basi hakuitaji. pole bi dada.
Anakuona unalazimisha penzi, na unamsumbua.
Kama angekua anakupenda au anakuitaji angekufuata.
wewe unamuhitaji ila yeye hakuitaji.
wewe unamtaka, ila yeye hakutaki. Samahani kwa maneno yangu, ila sasa vizuri unajua ukweli. funguka.

Wanawake wengine nyie munapenda kujitaftia matatizo sana.
Waswahili walisema dalili ya mvua ni mawingu.
Hachana nae, kuwa biz na masomo, sikiliza mziki, danse, tumia muda kufanya vitu muhim, hata kazi za kujitolea zipo, utamsau tu.
Atakae kupenda kweli na kukuitaji maishani mwake atajitokeza mwaka wowote ule na utaenjoy life, hadi utajuliza kwanini hakutokea mapema. Mvumilivu ula mbivu. kama ungekua na miaka 40 sawa, lakini ndio kwanza 26 tu? una muda mwingi ndugu yangu. husiwe na haraka haraka ya kupata mpenzi au mume, wengine mabomu

ooh ahsante... i got your point n hujatumia maneno makali but huwa nashangaa mwanaume anavyoomba msamaha na kuonyesha anajutia kosa, sababu mimi i dumped him twice but still ana`come asking for forgiveness, na mimi simsaidii kitu chochote kusema aje aniombe msamaha ol these time na kutaka kuganga yajayo, na kama ku`do tulishaachaga 4 months now` nilivyojua ni muongo, hata nikilala kwake nikikataa we wont do it...and he will respect that, well nimeelewa your concern, thank you! :smile-big:
 
Kusoma hujui na picha pia ujui kutazama!!!!!!!!!! Hilo si fungu lako bi dada toka fasta kabla ujatoka na mengine pia
yah ni kweli unayosema, na wala simng`ang`anii ila kwa nini mtu aombe msamaha mda wote huo, sababu mimi siku expect aje arudi kwangu after mimi kujua alinidanganya and i choose to keep a distance, na kama shida yake ni mdegedo, tulishaachaga mda miez 4 sasa as tunaongea na kujaribu solve mambo.. but mh labda ndiyi binadamu tunaweza igiza bila sababu na faida yoyote.
thnks kwa kukoment
 
mbona sielewi?umemsamehe mara hutaki kurudiana nae ah! all in all unadanganywa mama.

Yeye mwenyewe keshatuambia jamaa yake tabia utata mtupu. Unataka ushauri gani mpendwa hujaona tuuu unafanywa falaa
 
nimeelewa dalalitz...tnks
 
Back
Top Bottom