Tabia za madereva wa aina mbali mbali za magari

Tabia za madereva wa aina mbali mbali za magari

Madereva wa mabasi ya mwendo kasi Kimara

Habari za asubuhi mabibi na mabwana. Mimi ni mmoja ya watumiaji wa usafiri wa BRT baada ya kuona huu usafiri unasaidia kufika haraka mjini.

Pamoja na kufeli kwa mradi huu kwa kuwa na Magari machache, yasiyokuwa na mpangilio malumu wa kuondoka, basi madereva wake sijui tuseme wamelewa kazi! Hasa hawa wanaoendesha Magari ya Kimara, wamejaa sifa za kijinga, nyodo, kisirani na kuwakomoa abiria.

Tabia zao ni kama wavuta bangi tu. Hawa madereva wa Kimara wanatabia za kuwakomoa abiria wanaopanda hayo Magari na wanashuka vituo vya njiani hadi ubungo maji. Hawasimami hadi kibo hata kama si gari la express.
Then yale yanatoka Kimara hayasimami kibo ili kuwakomoa walipitishwa vituo, wanapita kama hawaoni kwa maksudi.

Wanasahau kuwa nauli za abiria hao wanaowafanyia hivyo ndizo zinawafanya wapate chochote kwa maslahi yao na ya familia.
Nawakimbusha tu nyinyi madereva pamoja na kazi zenu heshimuni Wateja wenu na muwe na utu. Unapata faida gani kumsumbua mwenzako? Hizo ni kazi tu ipo siku hutakuwepo nayo ukifanyiwa vile na wewe utafurahi?
Jitekebisheni yale si Magari yenu binafsi. Kunahaja ya kuweka ushindani kwenye Huduma ya BRT.
 
#5 inanihusu..now nimetoka kuweka zutu la buku 3
 
14.) Suzuki carry
Madereva hawa ni wahanga wa njaa za ajabu ajabu za matrafiki barabarani, huwa wanatabia ya kuandaa milungula ya shs.2000/= hadi 5,000/=tayari kwa kuwahonga matrafiki kwa makosa yahusuyo ubebaji holela wa mizigo (overloading & misloading). Huwa wanalazimika kupeleka hesabu ya hadi 120,000/= kwa wiki kwa matajiri wao hali inayopelekea kuwa ni watu wa stress sana. Wengi wao huwa na ndoto za kukabidhiwa Town ACE au Mazda BONGO na matajiri wao ili waweze kuongeza kipato chao, kiufupi ni watu wenye vision, na wengi hufanikiwa kimaisha.

001.jpg
 
Back
Top Bottom