Tabia za madereva wa aina mbali mbali za magari

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
36,066
40,725
1.)Toyota Brevis - ai Series / Mark X
Madereva wa magari haya hujisikia very powerful and classic wawapo barabarani, hii inatokana na gari hizi kufungiwa engine kubwa mithili ya fuso ndogo na kuwa na muonekano ambao ni very commanding.
Wengi wao ni vijana wa kipato kizuri wenye kati ya miaka 25 - 40 hali inayosababisha gari hizi kuhusishwa na uporaji wa wake/ wapenzi wa watu, kiukweli kwa interior ya hizi gari ni ngumu kwa mtoto kuchomoa pindi aingiapo humo, akishakalia tu ile leather ni amekwisha.
Toyota_Brevis.jpg


2.) Toyota Altezza / Subaru Forester - Noisy Series
Asilimia kubwa ya madereva wa magari haya ni vijana wanyoa viduku wasio na staha barabarani; kwanza wanaweka milio mikubwa mno bila sababu za msingi na hupenda kuendesha kwa mihemko kutokana na kelele kubwa za magari hayo. Wengi huonyesha dalili za matatizo ya kisaikolojia, ambapo hu-compensate kushindwa kwao katika nyanja mbalimbali za maisha kwa ku-seek attention mabarabarani kwa kuendesha kwa fujo na makelele yasio na msingi.
images-3.jpg


3.) Toyota Harrier /Lexus - G Series
Kiwango cha juu cha madereva wa magari haya ni wanawake wa makamo wenye umri wa kati ya miaka 38 hadi 45; na nimebaini wengi wao hua ni wamehongwa hayo magari na waume zao ambao kimsingi ni wazee wenye miaka 50 kwenda juu. Madereva hawa huwa na mashauzi barabarani hasa wanapokutana na gari zenye caliber ndogo kama vitz na kujihisi wapo kwenye ndege, hii hujionyesha kwa tabia yao ya kupenda ligi za kijinga barabarani.
images-4.jpg


4.) Toyota Landcruiser - V8 series
Wengi wao ni madereva wa magari ya serikali au mashirika mbalimbali ya kimataifa. Wengi wao hujisahau na kufikiri kwamba muda wote wapo kwenye msafara wa kiongozi na hawapaswi kabisa kukaa foleni. Hutanua kwa fujo bila aib wala uoga, na matrafiki nao huyagwaya magari haya na huyaacha yatanue as if yapo kwenye msafara. Wengi wao hujihusisha na upigaji nyoka mafuta hasa yale yanayotumia diesel na kwenda kuyauza kwenye black market. Hulipwa vizuri japo wengi huwa hawatoboi kimaisha.
images-5.jpg


5.) Toyota IST, Vitz ect - Baby walker Series
Kigezo kikubwa cha watu kununua gari hizi ni ulaji mdogo wa mafuta, hivyo ni an inherent characteristic ya madereva wengi kama si wote wa IST/vitz like cars kuwa ni wabahili mno hasa wanapokuwa fuel station; ni kawaida sana kuwaona wakiweka hadi mafuta ya buku 5 kwa kujiamini kabisa. Pia wana tatizo la kisaikolojia ambalo kitaalamu huitwa 'Inferiority complex', ni ile hali ya kujisikia unadharaulika hata kama hakuna aliekudharau, muda wote anahisi kama anapopita watu wanamnanga ..." check jamaa na kitoy chake...."

images-6.jpg


6.) Range Rover / Land rover - Discovery series
Nimebaini asilimia kubwa ya madereva wa magari haya ni wazungu wa balozi mbali mbali pamoja na waarabu koko waishio nchini; hupendelea sana kutumia njia kuu na kamwe hawapendi kutumia michepuko hata foleni iwe kali vipi. Pia hupendelea kuendesha mijini na high suburbs tu, as if waliambiwa wakipita Tandale wata tekwa flani hivi, it goes without say, huwa wanajihisi ni raia wa daraja la juu zaidi ya madereva wengine wawapo barabarani. Na tabia yao kubwa ni kuning'iniza suti kwenye seat ya nyuma, sijui maana yake nini, nisaidieni hapa.

images-7.jpg


7.) Toyota Tacoma / Tundra ect - Off road Series
Madereva hawa ni wale wapendao kutumia ile misemo ya "A real man uses three pedals", na hata slogan za magari haya utakuta zinasema " Acar that understands men". So ni watu wenye tabia ambazo kwa lugha ya malkia tunawaita 'Chauvanists', yaani wanajifanya wa kiumeni zaidi, needless to say wana mifuko mirefu sana coz hizi gari ni very expensive but powerful and luxurious with very good looks!

images-8.jpg


8.) Toyota pick-up(1984 - 1992)
Mara nyingi madereva wa gari hizi ni wamama wazee wa Kichagga ambao wengi wana tabia za kupenda ufugaji wa ng'ombe wa maziwa na kilimo cha migomba ya ndizi hasa pembezoni mwa jiji, hii hupelekea magari haya ambayo mengi ni makuu kuu kutumika kubebea majani ya ng'ombe na mbolea. Wamama hawa ni 'wagumu' na ni ma-fighters sana katika masuala ya kiuchumi, na mara nyingi ni wanene wanene hivi na huwa ndio tegemeo la familia.
320px-1981_Toyota_HiLux_(RN40R)_2-door_utility_(2015-07-14)_01.jpg


9.) Toyota Noah - Family Series
Madereva wengi wa magari haya ni wababa wa nyumbani (Family guys) wenye familia za atleast watoto wawili na kuendelea. Watu hawa wana tabia za kuonyesha upendo kwa watoto na wake zao kwa kupenda sana kuwatoa outing za beach nk, na ndio maana wakanunua 'daladala' yenye uwezo wa kubeba mke, watoto, housegirl, wakwe na mashemeji bila matatizo. Ni watu wa kipato cha kawaida ila wana moyo wa upendo kwa familia zao. Ila pia hupenda kuendesha biashara za stationery na pharmacy ambapo hutumia hizo noah kusafirishia bidhaa kama macounter book na madawa ya aina mbali mbali.
images-12.jpg


10.) Land rover - Defender Series
Asilimia kubwa ya madereva hawa ni mapolisi na hata kama gari haina namba za polisi bado kuwa makini, hawa polisi huwa wanatabia ya kubandua plate namba kila baada ya operesheni na kubandika namba nyingine randomly ili kukwepa kufuatiliwa na kigundulika kirahisi. Huwa wanatabia ya kutohudumia magari yao vizuri, huwa wanajisahau na kufikiri kwamba gari likiwa chafu chafu, lenye mikwaruzi mikwaruzo, pasi kila mahali na kuoza oza kwa kutu ndio linaonekana gari la kazi. Na pia wana tabia ya kutojaza mafuta hadi yakaribie kuisha kabisa; Tabia hii ya madereva hawa ndio imechangia magari mengi aliyopeleka Makonda kule Arusha kutorudi.
1-1.jpg


=====================================
CHAPTER II

11.) Hyundai Santa FE - 4WD Series
Mwanzoni nilifikiri utani, lakini siku zilipozidi kwenda ndio nikagundua kwamba wanaondesha haya magari ni wahindi tu, sikujua chanzo ni nini at first, ila nikaja kugundua hawa madereva wana tabia za kupenda vitu vya kutoka nchini kwao kwani Hyundai ni kampuni ya magari yenye tawi kubwa India (Subsidiary company). Wengi wao husomesha watoto wao kule Upanga kwenye shule kama Aga-khan (nilisoma hapo na wengi walifuatwa na Hyundais), Shaaban robert na Al-muntazir. Ni watu wenye tabia ya kujitenga mno na hawapendi kujichanganya na locals. Inafikia stage hadi mabus ya shule za watoto wao huandikwa 'Indian school', tena ni zile TATA za India. Na hata kama amezaliwa na kuishi TZ maisha yake yote, madereva hawa wana tabia ya kujifanya hawajui kiswahili.., sijui kwann, ila kihindi sasa..
images-16.jpg


12.) Suzuki Samurai/ Jimmy - 4WD Series
Wengi ni madereva wa makampuni ya ulinzi ya daraja la chini kabisa, kiukweli wana kiwango kidogo sana cha elimu kuanzia darasa la 7 hadi form 2. Wanamishahara midogo sana na hivyo hata maisha yao ni magumu pia, hii inapelekea wao kupanga katika maeneo ya uswahilini mno kwani gharama za pango huko ni nafuu. Madereva hawa wana tabia ya kuwanyenyekea sana waajiri wao na kuvumilia manyanyaso ya kucheleweshewa mishahara na wako tayari hata kuwalamba miguu mabosi wao ili wasipoteze ajira, ni watu wenye very low regard for themselves.
images-19.jpg


13.) Fiat 643N (Mbaula) - Flat bed Series
Madereva wengi wa malorry haya ni waajiriwa wa wasomali koko waishio nchini, magari haya toka Italy yalianza kuzalishwa miaka ya 1967 huko Turin, na kwakuwa Somali iliwahi kuwa chini ya utawala wa Italy, wamiliki wengi wa kwanza wa hizi mbaula wamekuwa ni waSomali. Madereva wengi wa magari haya wana tabia ya kujifunga usongo kichwani na kuvua shati wakibaki na vest tu; hii hutokana na malorry haya chakavu kuwa na steering wheel ngumu sana na kukosa A/C kabisa, kazi wanazopenda madereva hawa ni kubeba mifuko ya cement na makontena ya town trip toka bandarini.
b49306a7525cda86670e7ddc2cac3de1--truck-iveco-vintage-trucks.jpg


14.) Suzuki carry
Madereva hawa ni wahanga wa njaa za ajabu ajabu za matrafiki barabarani, huwa wanatabia ya kuandaa milungula ya shs.2000/= hadi 5,000/=tayari kwa kuwahonga matrafiki kwa makosa yahusuyo ubebaji holela wa mizigo (overloading & misloading). Huwa wanalazimika kupeleka hesabu ya hadi 120,000/= kwa wiki kwa matajiri wao hali inayopelekea kuwa ni watu wa stress sana. Wengi wao huwa na ndoto za kukabidhiwa Town ACE au Mazda BONGO na matajiri wao ili waweze kuongeza kipato chao, kiufupi ni watu wenye vision, na wengi hufanikiwa kimaisha.
001.jpg


________________________________



PIA, SOMA: Fahamu tabia za watu kulingana na magari wanayomiliki
 
Back
Top Bottom