Dodoma: Ajali ya gari la CAG, yaua watu 7 baada ya kugongana na gari la NSSF

warakaJr

Member
May 13, 2015
10
8
Kuna ajali mbaya imetokea usiku huu maeneo ya Mbande, Dodoma

=====

Watu saba waliokuwa wakisafiri katika gari STL 6250 mali ya CAG wamekufa papo hapo na wengine watatu kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na gari SU 41173 mali ya NSSF, katika eneo la Mbande Chalinze Mkoani Dodoma leo.

Taarifa za awali zinasema kuwa waliokufa katika ajali mkoani Dodoma leo katika gari la Ofisi ya CAG ni dereva wa ofisi hiyo na wengine 6 ni ndugu wa Naibu CAG waliokuwa wakitoka katika msiba huko Chato mkoani Geita.

Dereva wa CAG aliyefariki ametambulika kwa jina la Uson Kitanda Mjita. Alikuwa akitokea Dodoma kwenda Dar huku gari la NSSF lilikuwa likitokea Dar kwenda Dodoma. Majeruhi wote ni wa gari la NSSF. Maiti zipo Hospitali ya Kongwa.

Chanzo cha ajali ni Lori Reiland lenye tela lililoharibikia njiani. Dereva wa CAG aliligonga Lori hilo kwa nyuma na kupoteza uelekeo ndipo akagongana na gari la NSSF.
IMG_20181103_093846.png
tapatalk_1541233035198.jpeg
tapatalk_1541233041060.jpeg
tapatalk_1541233044061.jpeg
 
Aise ,, gari moja nasikia lilikua limebeba familia, so sad

Basi ile njia ya kulipia ingejengwa kuelekea huko kuwanusuru walio wengi, naona serikali inahangaika na madereva wakasome badala ya kutafuta namna nzuri ya kubadili tabia za madereva kuepuka ajali.

Mbaya zaidi watumiaji wengine wa barabara hawana haki pale yanapotokea magari ya serikali

Ipo haja ya magari ya serikali kufungwa machine maalumu za kurekodi mwenendo wa madereva wao kwasababu wengi wanaokufa kwa ajali ni abiria wasio na hatia, ukiwauliza madereva wanasema wanalazimishwa na maboss kuwahi waendako.
 
Back
Top Bottom