Dar to mwanza, picha linaanza pale ubungo zinaingia familia tatu za ndugu zangu wasukuma (watu kama nane wakiwa na watoto wadogo).
Hawakukaa pamoja, wengine walikaa nyuma kabisa, wengine katikati. Kazi inaanza akina ngosha walipoamua kupiga story kwa lugha yao, yani jamaa yuko siti ya nyuma kabisa ila anapiga story na ngosha mwenzie aliekaa siti ya kati.
Balaa zaidi ni pale walipoanza kupasiana vikombe vya maji (walibeba maji ya kunywa kwenye ndoo ndogo ya lita kumi). Kikombe kinapasiwa toka nyuma kule mpaka kinamfikia mlengwa kule katikati.
Mara watoto wakaanza kuzurula ndani ya bus, toka nyuma kuja kati endivaisi vesa bila kusahau vilio vya hapa na pale. Kuna wakati nikahisi labda niko kwenye darasa la chekechea, kumbe niko kwenye bus asee!
Kusema kweli Mwanza nilifika, ila cha moto nilikiona.
Safari ya kurudi dar, najikuta nimekaa jirani na mbibi msumbufu. Anyway, hiyo ni story nyingine!