Tabia za kishamba za mabasi ya mikoani

Tabia za kishamba za mabasi ya mikoani

🤣🤣🤣🤣🤣🤣 vya sukari sukari siyo kivileee ila kwa kuwa umesema mtoto Kajojo... Mangi fanya hivyo..... bwana weeee hela ya nn.... si umeambiwa unaletewa....weeee mangi acha bange basi Kajojo anakuja kukupatia....Asante Kajojo nimepata.... waiter nimerudi hizo bia zangu nitaendelea nazo ngoja kwanza nikipige kijoti zawadi kwa mtoto Kajojo...Sema Kajojo....naaam
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Waha, Wasukuma, Wamasai na Wanyakyusa haya makabila ni wasumbufu sana safarini.

Waha ubishi ubishi, Wasukuma kula kula, Wamasai mafuta yao wanatopakaa na kuongea na simu kwa sauti, Wanawake wa kinyakyusa wanajamba sana akigeuka kajamba.
hahahaha uwiiiii sina mbavu et kula kugeuka wanajamba hahaha wamekuwa mbuzi akishiba kula kukihowa must ajambe hahaha,
 
Bila kusahau wale kina mama wanaosafiri na watoto wawili huku wamekata seat moja

Nilishawahi kujikuta dada msaidizi wa mtoto mwanzo hadi mwisho wa safari, yaaani kale kadogo nimekashikilia mimi, kale kengine kadada mtu kameshikwa na mama yake

Mbaya zaidi kale katoto kalinipenda na kunizoea mapema sana, kila muda dada hivi dada vile mara kanilishe vitu kanavyopewa na mama yake

Sio kwa ubaya, lakini ni usumbufu... kama una watoto wadogo wawili jitahidi kuweka seat mbili aseee

Siku hizi namuagiza anayenikatia ticket ahakikishe nakaa na mkaka
Jamani bahati hizi lini tena una mpango wa kusafiri hivi karibuni labda na mimi niangalie uwezekano wa kusafiri pamoja
 
Kuna Wale wanaotapika tapika hovyo

Kuna mdada Aliwahi nitapikia kwenye Paja kidgo tuu, Likawa linasema Sorry Sorry mdogo wangu huku ananifuta...Yani nilitamani nimpige kichwaa
Yakaisha tukaongea ongea likanipa Namba , Mpaka Leo nimemsave Vomit hahah

NB, Sijaomba mzigo
angekuwa me vp!!usingemuacha salama mkuu hahaha
 
Kuna mdada tulipanda basi ubungo tulikuwa seat moja kuelekea Dodoma, kufika chalinze anaanza kunilalia ,nikamwacha kabisa anilalie huku nimemshika kiuno.

Tunakaribia Dodoma nikamwambia vipi kwanini tusichukue chumba upunzike kabisa kwa uchovu wa safari.
Unajisikiaje kuleta stori nusu isiyo na mizania?
 
Ila kusema ukweli hizi mnazo ita kero huwa ni changamoto ndogo ndogo na zingine sio za kumlaumu mtu

Mfano kutapika....hii ni hali ambayo haizuiliki inakuja tu bila mwenyewe kupenda
Kujamba pia haizuiliki
Na kuna watu AC hawaziwezi lazima atafungua dirisha

Kula kula, kuongea sana, kuongea na simu nk ni hulka ya mtu inabidi ukubali tu

Hizi changamoto nyingi zilizo tajawa na wadau huwa zinapungua sana ukipanda mabasi ya kampuni amabazo zipo vizuri hata bei zao zinakua zimeshiba

Ila sasa ukipanda haya mabasi yasio na utaratibu mzuri na bei zao zinakua nafuu ndio kuna changanyikeni haswa

Naenda sana Singida, ukipanda ABC hadi utaona raha, panda sasa sijui Imo, Najimunisa nk
Unakuta Ac hakuna wengine wanataka viioo vifungwe inakua joto vikifunguliwa wengine wanalalamika upepo

Mabasi ya bei chee hawaangalii idadi ya watoto kwa abiria na uingiaji wa mizigo ndani ya basi
Mabasi smart angalau wanao kata tiketi huko wanakua na kaustaarabu fulani
 
Kuna mdada tulipanda basi ubungo tulikuwa seat moja kuelekea Dodoma, kufika chalinze anaanza kunilalia ,nikamwacha kabisa anilalie huku nimemshika kiuno.

Tunakaribia Dodoma nikamwambia vipi kwanini tusichukue chumba upunzike kabisa kwa uchovu wa safari.
Mkuu hukula kimaskhara kweli?
 
Waha, Wasukuma, Wamasai na Wanyakyusa haya makabila ni wasumbufu sana safarini.

Waha ubishi ubishi, Wasukuma kula kula, Wamasai mafuta yao wanatopakaa na kuongea na simu kwa sauti, Wanawake wa kinyakyusa wanajamba sana akigeuka kajamba.
Whaaaaaat?
 
Mimi nishawah panda bus siti yangu pemben kulikua na mmama pamoja na mtoto wa kama miez Saba HIV
Sasa yule mtoto kwanza alinikaribisha kwa kilio kikali Kama kile Cha watoto wa nguru, tulipiga masafa marefu tukiendelea kuskiliza mlio wa yule mtoto

Baadae akanyamaza kikaingia kikwazo kingine,,,, alivobanwa na mkojo akawa anaonesha ishara za kutaka kukojoa Sasa yule mama yake ujinga aliokua anaufanya ndo ulikua unanikera Sana,. Alikua anampa kanga yule mtoto na anamwambia haya kojoa yaani alikua anaikojolea Ile kanga halaf anaendelea kuipakata ...Ile kanga ilikojolewa Mara nying Sana Jambo lililopelekea harufu kwenye eneo tulilokaa kubadilika na kuwa sio salama Tena




Tukio lingine hili mnisamehe tu kwaa kulichomekea

Mimi nikiendaga kazin huwa sinyoagi nywele kabisa had navokua narud hom so huwaga nakuwa na kale kamuonekano ka matajiri wakinga au wabena

Kuna safar nilikosa ndege nnayoipenda Ivo ikabidi nipande fly Dubai, Kama unavojua Tena Ile ndege kwa wadada wengi wanaopanda wanakuwaga ni mabeki tatu na kawaida ya Hiv viumbe Mara nyingi huwa vinatokea uswahilini na kwao ndege ni big deal

Hiyo siku nilikaa siti moja na beki tatu mmoja alikua ndo anarud bongo, jaman hakuna siku nilinyanyapaliwa Kama Ile siku yaan nilitaman mle ndan kuwepo na saloon nipunguze nywele.

Yule dada alikua ananiona Kama kichaa iv.
Tulivofika zenji watu wengi walishuka so kulikua na siti nyingine zipo wazi, nikajitosa kwenda kukaa siti moja na mzungu(mdada) Yan tulivokua tunapiga stori unaweza kusema tumewah kuonana sehem na hakuwa na nyodo yyte

All in all wadada sometimes wanakosaga bahati kwa fikra zao potofu japo yule beki tatu hakunivutia kwa chochote Ila kunidharau na wakat nimemzd vitu vngi hyo kitu iliniuma sana
Sentensi ya mwisho nimeipenda. Ulimzidi huyo dada vitu vingi mpaka nywele!
 
mimi kero yangu ni watu wa kuanzisha story.. naweza kukaa hta na mdada mkali sana na nisiongee chochote hadi mwisho wa safari.. sipendi story na mtu nisiemfahamu, kingne sipendi maswali.
sipendi kabisa kuulizwa maswali. .
 
Dar to mwanza, picha linaanza pale ubungo zinaingia familia tatu za ndugu zangu wasukuma (watu kama nane wakiwa na watoto wadogo).


Hawakukaa pamoja, wengine walikaa nyuma kabisa, wengine katikati. Kazi inaanza akina ngosha walipoamua kupiga story kwa lugha yao, yani jamaa yuko siti ya nyuma kabisa ila anapiga story na ngosha mwenzie aliekaa siti ya kati.

Balaa zaidi ni pale walipoanza kupasiana vikombe vya maji (walibeba maji ya kunywa kwenye ndoo ndogo ya lita kumi). Kikombe kinapasiwa toka nyuma kule mpaka kinamfikia mlengwa kule katikati.

Mara watoto wakaanza kuzurula ndani ya bus, toka nyuma kuja kati endivaisi vesa bila kusahau vilio vya hapa na pale. Kuna wakati nikahisi labda niko kwenye darasa la chekechea, kumbe niko kwenye bus asee!

Kusema kweli Mwanza nilifika, ila cha moto nilikiona.


Safari ya kurudi dar, najikuta nimekaa jirani na mbibi msumbufu. Anyway, hiyo ni story nyingine!
Hao wasukuma hawakubeba na ugali wa udaga?
 
(1) Unakuta mtu anaongea kwa simu kwa kupaza sauti hadi inakuwa kero kwa wengine. Sijui unataka uonekane mtu wa mipango au ndo vipi? Eti unajua kwenye ile indavyuu mimi pekee ndo nilifanya vizuri. mmxxsh hiyo intavyuu yako sisi inatuhusu nini.

(2) Gari ina AC wenzio wooooote wamefunga vioo wanakula unyunyu wewe umeacha madirisha wazi ukidai eti hupendi AC, mbona gari zisizo na AC ni nyingi kwanini usingeenda kupanda hayo?

(3) Umewekewa video au redio kwa sauti ya wastani kuruhusu hali ya utulivu ndani ya gari. Wewe unapaaza sauti kwa konda eti sauti ni ndogo iongezwe. Sio kila mtu anapenda sauti ya juu achilia mbali hiyo video au redio unayosikiliza.

(4) Kwenye hizi video hasa za action au vichekesho. Wewe unapatwa na mdadi unaanza kurukaruka au kuchekacheka hovyohovyo tena kishabiki utafikiri mwehu. Sio kila mtu anapenda makelele.

(5) Unalala kwenye siti yako hadi unakoroma kama nyau wa mwituni. Kibaya zaidi unamuegemea mtu wa siti ya jirani na kumwagia maudenda yako.

(6) Muda wote wewe unachezeachezea simu yako wakati unajua huna chaja. Matokeo yake unaanza kugongea chaja ya simu kwa wasafiri wengine.

Ukijiona unafanya hayo kuanzia sasa ujijue wewe ni mshamba na unakera wengine, jirekebishe.
Teh teh
 
Back
Top Bottom