Tabia za kishamba za mabasi ya mikoani

Tabia za kishamba za mabasi ya mikoani

Naomba kuelimishwa, ni wapi ambako sio mkoani nami nihamie huko?
 
Vipi wale wanaopanda na kuku na makorombwezo mengi mengi wanatumezesha mate wengine
 
Dar to Mbeya nilikaa siti moja na mdada mmoja mnene balaa kakaa dirishani
Yaani robo tatu ya siti mbili kaenea mwenyewe mimi nimekalia tako moja

Njiani sasa kila basi likisimama au wauzaji wakipanda mara kanunua mayai mara keki mahindi ya kuchoma/ kuchemsha chips parachichi......yaani yule mama njia nzima anakula tuuuu

Kuongea sasa khaaaa, yaani safari nzima anakuongelesha unaona ngoja nimjibu kwa kichwa tu ajue sipo interested, mdada anakuongelesha tu, nikasema ngoja nisiwe namjibu yaani ndio kwanzaaaa anakuongelesha huku mdomoni anatafuna kitu na kucheka cheka tuu

Mbaya kuliko yote, baada ya kula hayo mamichanganyiko yake akaanza kuachia mashuzi
Aisee sijawahi kutana na ushuzi unanuka kama wa yule mdada khaaaa
Halafu sijui ni ule unene hata kubana ushuzi utoke kama pancha ule wa kupuliza hawezi.....yeye alikua anuachia kabisa unasikia kabisa prraa tatataaa

Yaani akiwa anaongea ghafla utamuona kama anasitasita kama anasweta sweta halafu utasikia tu kitu kimeitika
Sasa sijui muda huo anakua anajaribu kuubana ushuzi ila inashindikana.?
Halafu atapotezea kama dakika 3 ushuzi ukipoa harufu anaanza maneno...kila kitu anajua yeye

Kama bahati kabla ya kufika Mbeya kuna abiria akashuka....yaani niliikimbilia ile siti fasta hata sikumuaga

Nimepata changamoto nyingi safarini ila nadhani hii ilikua funga kazi
kusafiri raha sana aswaaaa ukae na chibonge,
 
Tena namba 4 ndo wahovyo kabisa, unakutana na mtu anakulazimisha na wewe ucheke kama yeye anavyocheka, wengine huwa tuna mambo yetu hatuna mda wa kurazama movie ama nyimbo.
 
Umesahau wale wanaonunua mayai, wanayamenya halafu wanakula.

Ile shombo ya mayai ni noma sana.

Ikibidi, punguzeni tabia ya kula kula hovyo.
Ni kula kula hovyo au kununua vyenye harufu..!? Maana anayenunua mayai manne hawezi lingana na anayenunua kuku mzima
 
Ushamba nyumbani kwao si huko mikoani jamani sasa cha ajabu nini hapo?
 
Usiombe ukae na mdada mneneee aaf ana matako makubwaaa anakulakula hovyo akianza kuachia vile vishuzi vyao vya sailensi daaah utaomba poo
 
Hii ni tabia mbaya sana, baadhi ya abiria wanafanya hivyo, sio poa kabisa.
Hii Id yako napoiona basi akil zangu huwa zinarud kwenye Java Programming concepts & tools
 
Hii ni tabia mbaya sana, baadhi ya abiria wanafanya hivyo, sio poa kabisa.
Hii Id yako napoiona basi akil zangu huwa zinarud kwenye Java Programming concepts & tools
 
Kuna wale matumbo mpakile, yakipita mahindi ya kuchoma twende, ya kuchemsha twende, mayai twende, sijui biscuit mpaka inakua kero though pesa ni zao.

Let's meet at the top, cheers 🍻
Ngoja ajambe sasa ,lazima u mind hata kama pesa ni zao
 
Ila Huwa wana roho nzuri ya kugawa vitu vyao, Kuna mmoja alinikaribisha ndizi za kukaangwa na kuku af asubuhi tu, kila centre kubwa tukifika ananunua kitu cha kutafuna iwe mayai, matunda hadi mahindi.

Tulipofika kituo cha kupata lunch naye akashuka kula ubwabwa na kuku. Nilishangaa kimoyomoyo ila sikumind
Ahajahaja...uta mind vp zaid ya kufarahia na ushasema kila kitu alikua anakula anakupa na ww😂😂
 
Waha, Wasukuma, Wamasai na Wanyakyusa haya makabila ni wasumbufu sana safarini.

Waha ubishi ubishi, Wasukuma kula kula, Wamasai mafuta yao wanatopakaa na kuongea na simu kwa sauti, Wanawake wa kinyakyusa wanajamba sana akigeuka kajamba.
Dah umenichekesha sana mkuu
 
Back
Top Bottom