Tabia za kishamba za mabasi ya mikoani

Tabia za kishamba za mabasi ya mikoani

Dar to mwanza, picha linaanza pale ubungo zinaingia familia tatu za ndugu zangu wasukuma (watu kama nane wakiwa na watoto wadogo).

Hawakukaa pamoja, wengine walikaa nyuma kabisa, wengine katikati. Kazi inaanza akina ngosha walipoamua kupiga story kwa lugha yao, yani jamaa yuko siti ya nyuma kabisa ila anapiga story na ngosha mwenzie aliekaa siti ya kati.

Balaa zaidi ni pale walipoanza kupasiana vikombe vya maji (walibeba maji ya kunywa kwenye ndoo ndogo ya lita kumi). Kikombe kinapasiwa toka nyuma kule mpaka kinamfikia mlengwa kule katikati.

Mara watoto wakaanza kuzurula ndani ya bus, toka nyuma kuja kati endivaisi vesa bila kusahau vilio vya hapa na pale. Kuna wakati nikahisi labda niko kwenye darasa la chekechea, kumbe niko kwenye bus asee!

Kusema kweli Mwanza nilifika, ila cha moto nilikiona.

Safari ya kurudi dar, najikuta nimekaa jirani na mbibi msumbufu. Anyway, hiyo ni story nyingine!
 
Dar to Mbeya nilikaa siti moja na mdada mmoja mnene balaa kakaa dirishani
Yaani robo tatu ya siti mbili kaenea mwenyewe mimi nimekalia tako moja

Njiani sasa kila basi likisimama au wauzaji wakipanda mara kanunua mayai mara keki mahindi ya kuchoma/ kuchemsha chips parachichi......yaani yule mama njia nzima anakula tuuuu

Kuongea sasa khaaaa, yaani safari nzima anakuongelesha unaona ngoja nimjibu kwa kichwa tu ajue sipo interested, mdada anakuongelesha tu, nikasema ngoja nisiwe namjibu yaani ndio kwanzaaaa anakuongelesha huku mdomoni anatafuna kitu na kucheka cheka tuu

Mbaya kuliko yote, baada ya kula hayo mamichanganyiko yake akaanza kuachia mashuzi
Aisee sijawahi kutana na ushuzi unanuka kama wa yule mdada khaaaa
Halafu sijui ni ule unene hata kubana ushuzi utoke kama pancha ule wa kupuliza hawezi.....yeye alikua anuachia kabisa unasikia kabisa prraa tatataaa

Yaani akiwa anaongea ghafla utamuona kama anasitasita kama anasweta sweta halafu utasikia tu kitu kimeitika
Sasa sijui muda huo anakua anajaribu kuubana ushuzi ila inashindikana.?
Halafu atapotezea kama dakika 3 ushuzi ukipoa harufu anaanza maneno...kila kitu anajua yeye

Kama bahati kabla ya kufika Mbeya kuna abiria akashuka....yaani niliikimbilia ile siti fasta hata sikumuaga

Nimepata changamoto nyingi safarini ila nadhani hii ilikua funga kazi
 
Kunywa maji kidogo
Oyaaa!!mzee baba sikila mtu kalipa nauli take?mbonaa unatufokea Kama tumepewa lift.....usinipangie hi ni public transport Kama vipi panda ndegee,afu eti wa mikoani kwani uko jijini kwenu hakunaa watu Kama hao Tena ndo vishoiaa balaa,wanataka kujifanya wajuajii kupita kila mtu
 
....konda muna serenget lite au safari kubwa? ... hamuuzi humu basi sawa....ata short hamupimi..??? ooohh sorry.... jaman nipo ke bus la mkoani... kiu htr
 
Hujasoma nilichoandika ama Umesoma hujaelewa labda sababu ya usingizi....lala kidogo utasoma badae

Unajiashebedua tu. Jamaa kakuchana 'black & white'.
Mwanamke gani unakua na roho ya korosho kwa wanawake wenzio wenye watoto!
Viungo vyako vya 'jinsia' ya kike vimekamilika kweli?
 
Bila kusahau wale kina mama wanaosafiri na watoto wawili huku wamekata seat moja

Nilishawahi kujikuta dada msaidizi wa mtoto mwanzo hadi mwisho wa safari,yaaani kale kadogo nimekashikilia mimi,kale kengine kadada mtu kameshikwa na mama yake

Mbaya zaidi kale katoto kalinipenda na kunizoea mapema sana,kila muda dada hivi dada vile mara kanilishe vitu kanavyopewa na mama yake

Sio kwa ubaya,lakini ni usumbufu...kama una watoto wadogo wawili jitahidi kuweka seat mbili aseee

Siku hizi namuagiza anayenikatia ticket ahakikishe nakaa na mkaka

Siku nyengine ukiwa unataka kusafiri naomba unitaarifu tukate siti moja mimi na wewe hata kama sina mpango wa kusafiri nitasafiri tu kwa ajili yako.

Hutakaa ujutie.
 
Hahahah rafiki zangu hakuna mwenye ratiba ya kuwa na mtoto

Ngoja niangalie kwa ndugu labda nijaribu

..... tutakutana tu siku🤣 mundende bwiiiii..... ila siyo msumbufu hata kdogo! Nikitaka kutongoza nakuomba ruhusa ukininyima natulia tuliii....yaani chochote mpaka upende ww! Sina makuu.... sijalewa kiiivyoooo nikashindwa kuchangia mada
 
Siku nyengine ukiwa unataka kusafiri naomba unitaarifu tukate siti moja mimi na wewe hata kama sina mpango wa kusafiri nitasafiri tu kwa ajili yako.

Hutakaa ujutie.

😂😂😂 nitafanya hivyo ukuwi
 
..... tutakutana tu siku🤣 mundende bwiiiii..... ila siyo msumbufu hata kdogo! Nikitaka kutongoza nakuomba ruhusa ukininyima natulia tuliii....yaani chochote mpaka upende ww! Sina makuu.... sijalewa kiiivyoooo nikashindwa kuchangia mada

🤣🤣🤣🤣
 
Bila kusahau wale kina mama wanaosafiri na watoto wawili huku wamekata seat moja

Nilishawahi kujikuta dada msaidizi wa mtoto mwanzo hadi mwisho wa safari,yaaani kale kadogo nimekashikilia mimi,kale kengine kadada mtu kameshikwa na mama yake

Mbaya zaidi kale katoto kalinipenda na kunizoea mapema sana,kila muda dada hivi dada vile mara kanilishe vitu kanavyopewa na mama yake

Sio kwa ubaya,lakini ni usumbufu...kama una watoto wadogo wawili jitahidi kuweka seat mbili aseee

Siku hizi namuagiza anayenikatia ticket ahakikishe nakaa na mkaka
Ilishawahi kunikuta hii nilibeba mtoto masaa 9 mama yake akawa analala tu bila aibu, mtoto akienda kwake anamuuliza unamtaka ankoo uende kwa ankoo.
 
Pia unakuta yeye wakati ni mdogo mama yake aliwahi kusafiri nae akiwa na mdogo wake na akabebwa na abiria wa jirani, Mimi sijawahi kuwanyanyasa kabisa wa mama wenye watoto na mizigo mana ndio nature ya mama zetu, Naweza kukoromeana na Age mates au Mwanaume mwenzangu ila sio wamama kabisa
Unaanzaje kwanza?
 
Back
Top Bottom