Tabia za kishamba za mabasi ya mikoani

Tabia za kishamba za mabasi ya mikoani

Hahaha! Umenikumbusha beki tatu mmoja nilikjwa natoka Mtwara sasa ile asubuhi gari ikasimama maeneo ya Mnazi Mmoja Lindi kama saa tatu asubuhi hivi, sasa yule beki 3 akanunua miwa ya 1000 ambayo haijamenywa, nilidhanilabda ni zawadi huko aendako,

doooh akaanza kuimenya na meno na kuanza kuila hehehe! Akajaza dust bin ya gari na makapi ya miwa na hakuchukua round akaanza kutapika juice ya miwa alitapika sana vitenge vyake vyote vililowa matapishi hadi vingine ilibidi gari isimame achukue bag kwenye buti ili atoe vitenge vya ziada.
Nimecheka hapo kwenye kufungua buti
 
Hamna tabia inanikwaza na kuniudhi kama kuweka nyimbo za dini za kikristo full time, basi bora hata wangekuwa wanabalance na nyimbo za wenzetu waislam Hamna.

Yaani watendaji wa mabasi hawana ubunifu kabisa.
Na sie tunaokaa pwan kwenye dala dala ful mawaidha tena ya kukashifu upande wa pili yale .
Na ndan tumejaa abiria.utafanyaje sasa?
Ndio hivyo tuvumiliane tu
 
Nilishangaa sana jamaa aliponiomba ear phones asikilize muziki. Seriously unaomba earphones za mtu humjui hakujua. Niliona kama kanidharau, hivi unaanzaje kuomba earphones.
Una roho ndogo sana.
Sina maana alikua sahih kukuomBa ila ww hupaswa kuona kama kakudharau!?how yan?!!
 
Vitu vinavyoondoa kinyaa ni safari za nchi za nje, kuuguza na uzazi. Kama ukiyapitia hayo yote na ukabaki na kinyaa basi hakiwezi kuisha.
Hata mimba changa hana huyu unaongea na vitu above level yake..
 
Dah mi yotee navumilia ila kwenye swala la kunuka mdomo asee huwa na vurugwa Sanaa.

Unakaa na mtu Siti moja ananuka mdomo alafu ndo kila saa anauliza ma swali hapa wapi mara tunafika sangap.
Huku na vicheko asee dah Acha tuu
 
Hiyo namba 2 huwa inanikera Sana
Nikishakaa na mtu anafungua madirisha, asiponisikia nikimwambia namwita konda anihamishe siti..kuumizana tu vichwa
Nimeshawahi hama siti mara kibao kwa huu upuuzi wa mtu kufungua fungua madirisha,sijui wanakuwa na vichwa vya chuma wale upepo mkali namna ile hauwaumizi,mtu anapambana tu kufungua madirisha utadhani sifa
Mwingine unakuta amekaa siti ya mbele yako anafungua dirisha ule upepo wote unakuja kuwapiga nyuma ,nitavumilia kero zote safarini ila si hii ya kufunguliana madirisha hovyo.

Nahiyo #4,kuna majitu utadhani Yana ving'ora midomoni,yaani kuna mtu aliwahi kukaa nyuma ya siti yangu,jamani jamani linapayuka hilo hadi ngoma za sikio zinauma
Jitu zima linashangilia movie ndani ya basi kwa kelele utadhani tupo uwanja wa maonyesho ya sinema
Kuna watu mliumbwa rojo rojo sana.sometimes nasomaga come kama hiz halaf najaribu kuzi relate na maish yangu dooh!!japo sio sifa ila naona kabisa vitu vngine sio vya kulalamika.ni vya kawaida sana
 
Kero yangu:-

- Wale wanaotangaza dawa na vibiashara vingine kwenye bus. Sijui kwanini dereva na konda huwa wanawaruhusu hawa watu wenye kero hivyo watupigie kelele abiria

- Wanavyoweka filamu zilizotafsiriwa au za kibongo za hovyohovyo za kina Mau n.k filamu inaitwa Bangi, au eti mbuzi wa birthday na action za kipumbavu za bongo.

Hasa magari yanayokwenda Tanga
Ajahaha mbuzi wa bday 😂😂 nimekutana nayo hii aise kwenye mabas wanatuwezaa!!!
 
Kuna wale waliokwisha angalia zile bongo movie, afu wanacheka ili nanyi mcheke au mtazame, huwa wananikera sana.
 
Na sie tunaokaa pwan kwenye dala dala ful mawaidha tena ya kukashifu upande wa pili yale .
Na ndan tumejaa abiria.utafanyaje sasa?
Ndio hivyo tuvumiliane tu
Hao laanatullah inabidi tu uwapuuze kwasababu hawana elimu hao, kwenye ubongo kuna juzuu na laana tu
 
Duuh hili suala linakera sana, siku moja nilikaa na mdada mmoja kutoka Dar hadi mkoani yule mdada kutapika hasa akila kitu. Ila k
 
Kwa kweli kuna mdada mmoja nilikaa nae siti moja alikuwa anatapika hasa akila kitu. Ila cha ajabu kila kitu akiona kwenye gari ananunua na akila anatapika. Yaani alinikera sana yule mdada siku ile.
 
Usisahau na wale kila mda wanaopiga simu kuongea na wapenzi wao yan kila mda baby ndo tuko.... Baby ndo tunaelekea lunch...yan alaf ukute ana smartphone kila mda inachokonolewa kama mtu flan busy mweny text nyng na email
 
Kwa kweli kuna mdada mmoja nilikaa nae siti moja alikuwa anatapika hasa akila kitu. Ila cha ajabu kila kitu akiona kwenye gari ananunua na akila anatapika. Yaani alinikera sana yule mdada siku ile.
Kuna watu utopolo sana.
 
Bora wawili, niliwahi kukaa na mama ana watoto watatu imagine, halafu kakata siti moja tu! Ilibidi tu nimuelewe tubanane hivyo hivyo na kupakata mmoja maana hakukua na namna.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii iko sana Kigoma na usukumani, unakuta mama ana watoto watatu na mimba juu alafu anakata siti moja, magari yenyewe 3 by 2! Utaomba ukakae kwa Dereva. Alafu ana mafurushi kibao na dumu la Maji, maziwa mtindi na ugali! Mkuu acha kabisa, nimekaa tabora nimeyashuhudia siyo kwa kuhadithiwa. Hatariii
 
Back
Top Bottom