Tabia za boss wangu zinanikera

Tabia za boss wangu zinanikera

Kwa sababu wakati unaomba kazi ulienda mikono yako ikiwa nyuma na sasa baada ya kupata kazi unatembea huku mikono iko mbele. Kuchelewa kazini, kurudi mapema wakati wa lunch na kutokuwa makini kazini ni baadhi ya mambo yanayowaudhi sana maboss wengi. Jirekebishe wewe She.

Sio kwamba kila anayechelewa anakuwa anafanya makusudi, kuna foleni, kuna breakdowns n.k.
 
Usifanye makosa. Kuwa km robbort. Boss wako amesoma vizur ile theory (mbwa).."management by walking". Hana muda na "mbo" theory.
 
Ndugu, sio kila thread inayoandikwa humu inamface mwandishi. Nyingine zinawekwa kwa niaba, zingine zinawekwa ili zitoe fundisho fulani, zingine ili kufurahisha wasomaji n.k

Asante

Kumbeee!!!!!!!!!!!!!
 
  • Tenganisha cycle ya bosi ya interaction na ya kwako. Watu wanaomzunguka na wanaokuzunguka wawe tofauti.
  • Akikusahihisha however atakavyofanya, ni changamoto kwako ili uongeze bidii. Kwama wewe ni mtu wa kujitahidi hii itakusaidia sana ila kama ni mvivu basi huo ni mzigo mzito kwako.
 
Salaaaam wanajukwaa hili,

Awali ya yote namshukuru Maulana kwa wingi wa Rehma zake kwetu, ndio maana tumekutana tena katika jukwaa hili

Back to topic, mie hapa ni Cashier by professional. Nina boss wangu ambaye nareport kwake. In short tuko wawili tu katika office yetu. Boss huyu kiukweli hajawahi kunitaka wala kunitamkia mambo ya mapenzi na hata kuonesha dalili ila amekuwa kero sana kwangu kwa tabia zake ambazo kwazo wengi wetu tunaziita (tabia za kike).

Boss huyu ana GUBU jamani sijapata kuona, nikifanya kosa badala ya kuniambia basi atanuna the whole day or 2-3 days. Naweza kumsalimia akanyamaza tu nikimuuliza kitu hanijibu ataitikia sawa na halifanyii kazi, nikichelewa kufanya kazi fulani anazira na kuifanya mwenyewe ilhali sometimes anakuwa amenipatia (kaji kumi) kazi nyingi.

Boss huyu hawezi kutofautisha ofisini na mtaai, kila kitu cha ofisi tukifanyacho anakiexpose kwa watu. Leo nikichelewa kazini watu watajua, nikienda lunch nikachelewa kurudi watu watajua, kila ninachofanya hasa kibaya nitakikuta mtaani. Hawezi kuniita akanisahihisha bali anayapeleka mtaani na hao hao watu wanarudi kuniambia kuwa boss wako anasema hivi na vile.

Boss huyu anaamini sana maneno ya kuambiwa, akishayapeleka hayo mtaani naye ataambiwa ya kwangu ya uongo kisha anakuja anabwata kweli.

Yote tisa, kumi ni kuwa kila kinachofanyika ofisini atamwambia mwanamke wake. Nikikosea hesabu mwanamke wake atajua, nikikosea spelling mwanamke wake ataambiwa, nasema hivi kwa sababu mara kibao tu huwa anaongea na mwanamke wake kwa loud speaker akidhani nikiwa ofisini kwangu simsikii kumbe nasikia kila kitu. Huyu mwanamke akiambiwa wanaanza kucheka jambo ambalo linanikera sana.

Naomba ushauri wenu kwa yeyote ambaye ameshapitia situation kama hii huwa mnasolve vipi???
ungemtag hii thread mambo yangekuwa kuntu kweli mtongoze kama vipi mkuu au unaona noma..
 
[

Boss huyu hawezi kutofautisha ofisini na mtaai, kila kitu cha ofisi tukifanyacho anakiexpose kwa watu. Leo nikichelewa kazini watu watajua, nikienda lunch nikachelewa kurudi watu watajua, kila ninachofanya hasa kibaya nitakikuta mtaani. Hawezi kuniita akanisahihisha bali anayapeleka mtaani na hao hao watu wanarudi kuniambia kuwa boss wako anasema hivi na vile.

Boss huyu anaamini sana maneno ya kuambiwa, akishayapeleka hayo mtaani naye ataambiwa ya kwangu ya uongo kisha anakuja anabwata kweli.

kwani mnaishi jirani?
 
Huku niliko ni mji mdogo kiasi kwamba umbea wote wa mji hutapakaa haraka sana. Akisema neno jioni asubuhi litanifikia.

Tuko ofisini wawili, nifanyacho mie anajua yeye na afanyacho yeye ninajua mie. Inakuwaje mfano nikosee hesabu aje mtu wa nje aniambie "Oyaa nasikia umepata shot leo kwenye hesabu zako kazini" nani atakuwa kamwambia isipokuwa boss?

Hata nisipowasikiliza watatuma hata sms, ina maana ujumbe utanifikia.
ofisi gan ya watu wa2 bwana we sema ukweli tu mpe ki2 a2lie acha kutudesh
 
Wewe na bosi wako huyo mtakuwa mnagombea bwana! Haiwezekani mambo ya ofisini kwake apeleke mtaani na wewe mambo yake binafisi ulete huku...
 
Back
Top Bottom