matunduizi
JF-Expert Member
- Aug 20, 2018
- 6,587
- 15,371
Mwanadamu umeumbwa kwa mfano wa Mungu. Baadhi ya sifa za Mungu ni kufanya kazi. Tena kwa ufanisi na ubora, huu uwezo kila mtu ameumbwa nao maana kila mtu ameumbwa kwa mfano wa Mungu.
Watu wengi wanabagua kazi, na wengine kufanya kazi kwa uvivu bila morali ni kwa sababu wanafikiri dhumuni la kazi ni kuwaingizia wao kitu (fedha) tu.
Kimsingi kwa mujibu wa bibilia, Kila kazi halali ina faida. Kazi nyingine zinakusaidia kukuondolea tabia mbaya kama kujiinua, matumizi mabaya ya fedha, kukuongezea kufikiri, kukufanya uone mambo ambayo usingeyaona kama ungepata kazi unayoipenda.
Katika kila kazi halali kuna faida. Jifunze kutanua wigo wa faida unazopata nje ya kipato chako kazini.
Ni hilo tu.
Barikiwa.