Tabia Ya Kudhulumu Vibarua Au Maskini Wanaofanya Kazi Haiwezi Kumwacha Mtu Salama

Samson Ernest

JF-Expert Member
Aug 28, 2014
404
651
Kum‬ ‭24:14‭-‬15‬ ‭SUV‬‬
[14] Usimwonee mtumishi mwenye ujira aliye maskini na uhitaji, kama ni wa nduguzo, au kama ni wageni wako mmojawapo walio katika nchi yako, ndani ya malango yako; [15] mpe ujira wake kwa siku yake, wala jua lisichwe juu yake; kwa maana ni maskini, moyo wake umeutumainia huo; asije akamlilia BWANA juu yako, ikawa ni dhambi kwako.

Uonevu kwa maskini au wale vibarua wanaofanya kazi kwenye maeneo mbalimbali, inaweza ikawa viwandani, au nyumbani, au kwenye Biashara, au mashambani.

Watu waliowaajiri hao vibarua, huwa hawawapi haki zao kwa wakati, hadi wamzungushe pesa yake, Ile posho yake aliyopaswa kumpa huyu kibarua inaweza kuchukua muda mrefu sana bila kupewa.

Mungu aliliona hili, akawatahadhaharisha mapema Waisraeli, hawapaswi kumwonea kabisa maskini au yule kibarua aliyefanya kazi kwao.

Wapo matajiri ni Maarufu kwa kudhulumu vibarua haki zao, mtu amefanya kazi kwake akiwa na matumaini ya kupata fedha ya kwenda kujikimu na familia yake, mwisho wake anaambulia maneno matupu.

Napenda Leo ufahamu kuwa kufanya hivyo unamchokoza Mungu mwenyewe, unajiingiza kwenye kundi la watu wanaomchokoza Mungu vibaya.

Amwoneaye maskini humsuta Muumba wake; Bali yeye awahurumiaye wahitaji humheshimu. Mithali 14:31

Hebu fikiria mtu ni maskini au ni mhitaji, amekuja kwako kuomba kazi ya kufanya au umetangaza kuna kazi za kufanya kwako, anafanya vizuri na kumaliza, kwenye malipo yake unakuwa mgumu.

Jiulize ingekuwa ni wewe unapewa ahadi ya kutolipwa mshahara wako uliofanya kazi mwezi mzima, uambiwe utapewa mwezi ujao, alafu una mahitaji muhimu ambayo unapaswa kuyafanya kupitia hiyo fedha, ungejisikiaje?

Tusije tukajiona kuwafanyia maskini hayo hakuna lolote watatufanya, tujue kufanya hayo tunajipatia hukumu mbele za Mungu.

Tunamkasirisha Mungu kwa kuwanyima haki zao vibarua, jambo ambalo halipaswi kuwa kwa Mwamini kabisa, mtu anayesema anamwamini Mungu.

Nami nitawakaribieni ili kuhukumu; nami nitakuwa shahidi mwepesi juu ya wachawi, na juu ya wazinzi, na juu yao waapao kwa uongo; na juu yao wamwoneao mwenye kuajiriwa, kwa ajili ya mshahara wake, wamwoneao mjane na yatima, na kumpotosha mgeni asipate haki yake, wala hawaniogopi mimi, asema Bwana wa majeshi. Malaki 3:5

Tunapaswa kuelewa kuwa mtu aliyekuja kwako kufanya kibarua au shughuli yeyote ile kwa makubaliano ya malipo baada ya kazi, hakikisha unamlipa kiasi chake mlichokubaliana.

Acha ahadi za njoo kesho, akija unabadilisha kingine tena, akikomaa kudai haki yake unakuwa mkali na kuanza kumtishia mambo mabaya, kwa sababu unamwona maskini na hakuna kitu atakufanya.

Utakuwa unajidanganya sana kwa kufikiri huyo maskini au kibarua hana uwezo wa kukufanya lolote kwa sababu wewe una uwezo wa kifedha, jua huyo maskini kesi yake Mungu anaisimamia.

Ikiwa Mungu ndiye wakili wa maskini au kibarua wako ujue hiyo kesi huwezi kushinda kwa namna yeyote ile, unachopaswa kufanya ni kulipa gharama zote unazodaiwa na vibarua wako wote.

Nakukaribisha kwenye group la kusoma biblia kila siku na kutafakari, wasiliana nasi kwa wasap namba +255759808081 ili uunganishwe kwenye group hili zuri.

Mwisho, nikukaribishe kwenye channel yangu ya wasap kupata maarifa mbalimbali kama haya kwa mtiririko mzuri, bonyeza link hii kujiunga=>>Samson Ernest

Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia yako
Mungu akubariki sana
Samson Ernest
+255759808081
 
Back
Top Bottom