Tabia ya kuaga maiti ni ya hatari sana

Tabia ya kuaga maiti ni ya hatari sana

Waislamu hua wanaaga ila ni wanandugu wa karibu tu, tena mwili ukiwa ndani kama haujui ni vema kukaa kimya
Kweli kabisa mkuu. Tena tunaaga mwili ikiwa umeshavishwa sanda. Hata sura huoni!
 
Waislamu hua wanaaga ila ni wanandugu wa karibu tu, tena mwili ukiwa ndani kama haujui ni vema kukaa kimya

Waislamu hua wanaaga ila ni wanandugu wa karibu tu, tena mwili ukiwa ndani kama haujui ni vema kukaa kimya
Unachosema ni mazoea kwenye uisilamu hakuna kuaga maiti kama una ushahidi weka muisilamu akifa kinachofata ni mambo manne tu 1.kumuosha.
2.Kumvisha sands
3.Kumswalia
4.Kumzika
Kama kuna lingine lete
 
Binadamu anapokufa mwili wake huachana na roho,(nafsi /uhai) mwili huo hubaki kasha tupu lisilo na chembe yoyote ya uzima.

Na roho yake huenda sehemu inayostahili kulingana na matendo yake duniani.

Roho ndo uzima, roho ndo nafsi kamili, roho ndo uzima wenyewe. Kifupi ni kwamba binadamu hufa mwili ilihali roho ikiendelea kuishi katika ulimwengu mwingine wa roho ambao huwezi kuuona kwa macho ya damu na nyama.

Binadamu akifa anatisha, ukiambiwa ulale chumba kimoja na maiti huwezi, Hata Kama ni maiti ya mtoto bado utaogopa tu .

Sura ya maiti hukaa kwenye kumbukumbu ya ubongo kwa muda mrefu sana, kwa mtu yoyote atakayeikodolea macho maiti usoni.

Tabia ya kuaga maiti haina mashiko na sababu yoyote ile.
Kuaga maiti ni kuisanifu maiti, unaagaje kitu kisicho na uhai? Ni kipi kinakusaidia kumwangalia mfu?

Napenda sana utaratibu wa ndugu zangu waislamu, wao huiandaa maiti na kwenda kuzika basi, kuliko tabia ya mabwana wale wanaopenda kupanga foleni ili kuaga maiti msibani, foleni kubwa utadhani walimu wanachukua mshahara kwenye ATM ya NMB.

Mwisho wake huwa ni mayowe, watu kuzimia na kuanguka hovyo msibani.

Sura ya marehemu unaitakia nini? Unamuaga marehemu ili iweje?
Mkuu sasa pointi yako ni ipi sasa maana naona umetiririka na kukashifu mila desturi na tamaduni za watu.kama huna la maana ni aheri ukakaaa kimya tu mkuu haitadhuru itapendeza
 
Huu utaratibu ulikuja na lile meli kubwa kama ile lugha ngumu inayomsumbua yule mbunge wetu.
 
Waislamu hua wanaaga ila ni wanandugu wa karibu tu, tena mwili ukiwa ndani kama haujui ni vema kukaa kimya
marehemu akishasafishwa na kuvalishwa sanda haruhusiwi kuonekana zaidi ya wale waliomuandaa zaid mtaangalia alivyofungwa sanda sio sura.
 
Lakini 'kuaga' mwili wa marehemu sio lazima, ukitaka waenda au unauchuna kwa hiyo ubaya unaosemwa ni suala binafsi.

Vv
 
Ni kweli. Hata wayahudi hawasanifu maiti. Haya mashiko wanayo wakristo tuu, moja ya bad customs waliyo inherit toka kwa wazungu. Inatokana na mashiko ya kipagani.
 
hata iweje haipo namna maiti haitaonwa na watu, kama kafia nyumbani wapo watakaona kabla haijafunikwa, kama kafia wodini vivyo hivyo, akiwa mortual ataonekana tu, hata wakati wa kumuosha pia, hata anapoingizwa kabulini wapo tu watakaoona hata kama wachache, ndio maana kuna baadhi ya mila zinaruhusu kuangalia buriani maana haipo namna itakuwa siri maana hadi anafikia hatua ya kuzikwa anakuwa kaandaliwa na zaidi ya mtu mmoja na hakuna siri ya wawili. pia buriani ni desturi ya hiyari ulazimishwi kwenda kuaga.
 
Kuaga maiti kunaleta kuamini kweli your lovely one has really dead and gone forever.
 
Kifo noma sana bas tu
Hamna bana kifo sio noma kawaida tu maana policcm wana komaa na mishe hizo aaagh kifo very simple aisee sema tatizo kila mtu atakufa hata anaye ua wenzie yaan hapo ndio kifo kilipo weza , we uwa weeeeeeeeeee wakati wako ukifika na wewe down .
 
Waislam hawaagi Maiti (Marehemu) kinachofanyika ni kutoa utambulisho wandugu au watoto wa marehemu endapo wakati wa tukio la mauti hawajakuwepo kinachofanyika ni yule mtu wa karibu aliyekuwepo wakati umati unamfika kuwaeleza ndugu/watoto wa marehe kwamba huyo ndiye baba yenu au ndugu yenu tena wakati mwingne hutoa hata story fupi ya ugonjwa mpaka umauti kumfika
Huo "utambulisho" unaofanyika, Hao wanafamilia WANAMWANGALIA marehemu au HAWAMWANGALII?
 
Huwa napita mbele ya maiti bila kumtazama. Usipoenda kuaga hawachelewi kukusingizia ushirikina
Imebidi nichekeeeeee eti....... hawachelewi kukusingizia ushirikana
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hili zoezi mie huwa linanipa wakati mgumu sana na mara nyingi huishia kuingia mitini.
 
Back
Top Bottom