Tabia hizi za wageni zinakera

Mtoa maada ana hoja, sema kuna mijitu inajifanya haielewi. Hiyo ndo inasumbua watu. Chaja ina uzito gani mpaka usibebe yako!!? Sasa mwenyeji wako anataka kuchaj nawe ndo unasema niazime chaja. Unajua atakosa dili ngapi kwa kutokuwepo hewani!!?
Karudi jioni toka kazini hivyo anacharge simu zake, asubuhi kazini sasa naye mgeni ambaye yupo zaidi na zaidi imekaaje hapo, unakuta mgeni simu yake kila wakati simu ipo kwenye moto halafu charge ya kuazima

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shida sana. Wanaompinga mleta mada hayajawahi kuwatokea. Au ile umeweka simu yako chaji ina asilimia 5 kutoka kidogo kurudi unakuta mgeni kachomoa chaji kachomeka kwake daah
Hapo sasa mwenyewe una mambo yako na tanesco wasivyo na hiyana ile unataka kuweka na wanabeba umeme wao, mie wageni wakuamka asubuhi asubuhi wana nikera balaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii mada watu tu wameichukulia very negative, lakini ni very informative maana inakupa nafasi ya kujua ukiwa ugenini mambo gani ujirekebishe


Mi ananikera mgeni wa kuleta umbea wa huko atokako maana lazima achukue na ya hapo arudi nayo

Unasikia, mtoto wa flani, alifeli yule, alizungusha...tena unasimulia kwa bashasha mara flani anakusema kweli ni kama vile katumwa kuja kukuvuruga maana unaweza kujikuta unamchukia huyo uliyeambiwa anakusema

Nakereka balaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mgeni si Mzazi wala ndugu wa tumbo moja Mara unasikia nipo stand nimefika nakuja kukusalimia njoo nichukue!! Anakaaa siku nyingi mara Nipe nauli unataka kuondoka upo Lindi kwao bukoba. Hii mitihani
 
1. Mgeni kutaka mkeshe sebuleni mkiongea wakati kesho yake unawahi job
2. Kung'ang'ania remote
3. Siku ya kuondoka kuacha kitanda hakijatandikwa / mashuka machafu
4. Mgeni kurudi usiku baada ya baba mwenye nyumba kurudi na kumpigia simu amfungulie geti
5. Kukaa bila kusaidia kazi (kama amekaa zaidi ya siku tatu /nne).
 
unampa shuka na kagodoro kadogo ka dharula (uwe nako standby) akija unampa ajistiri sebuleni pale chini...easy
 
Back
Top Bottom