JOHNGERVAS
JF-Expert Member
- Mar 22, 2016
- 1,470
- 2,561
Mwezi wa Desemba ni mwezi wangu wa kuzaliwa. Kila mwaka nautumia mwezi huu kama fursa ya kuwakumbuka na kuwagusa wale wanaoishi mazingira magumu, hususan watoto na wazee wanaoishi mtaani bila kuwa kwenye vituo vya kulelewa, hivyo kukosa msaada wa moja kwa moja.
Kuna familia nyingi sana katika jamii zetu zinazopitia changamoto kubwa za maisha. Wengine hawana hata nguo za kubadilisha, achilia mbali uhakika wa kupata mlo hata mmoja kwa siku. Hali hii hunigusa sana na kunisukuma kutumia kile kidogo nilichonacho kuwapa tabasamu wenzetu hawa.
Mwezi huu, tarehe 23 Desemba, nitaendelea na zoezi hili la upendo kwa kuwafikia familia kadhaa (takribani familia sita) zilizopo Kibaha. Nitakuwa nikijitolea kuwasaidia kwa mahitaji mbalimbali ili nao wapate furaha kama sisi wengine.
Kwa yeyote anayependa kushiriki nami katika zoezi hili la kutoa tabasamu:
Napokea vitu tu, sipokei fedha kabisa. Fedha ni fedheha.
Kama una chochote unachoweza kuchangia na hutumii, tafadhali nitumie ujumbe binafsi (PM) uniambie ulipo ili nipate kufika kukusanya, kisha kwa pamoja tufanikishe zoezi hili la upendo.
Asante sana kwa moyo wako wa kujali. Pamoja tunaweza kuleta tabasamu.

- Nakaribisha nguo nzuri lakini ambazo huzitumii (sio chakavu),
- Nguo za watoto kuanzia chini ya darasa la 3 hadi form two,
- Nguo za watu wazima, hasa wazee wenye umri wa miaka 45+,
- Pia wapo vijana wachache (takribani watatu) kuanzia miaka 30+ wanaohitaji msaada.