Taasisi ya Moyo Tanzania yafungwa!

Ericus Kimasha

JF-Expert Member
Oct 27, 2006
488
470
Miaka mitano (5) iliyopita, hapa JF kulikuwa na mjadala endelevu mkali sana juu ya ugomvi kati ya Taasisi ya Moyo (THI) na Serikali kupitia Wizara ya Afya. Sakata hili sasa limehitimishwa rasmi kwa kunadishwa kwa mali za THI na huduma kufungwa. Kwangu binafsi hii ni habari mbaya katika mfululizo wa taarifa chungu juu ya matendo ya Serikali kwa Wazalendo wanaojitoa kwa Taifa lao na watu wa nchi yao. Kwa masikitiko makubwa tukio hili linatokea wakati huduma katika Sekta ya Afya zimepolomoka na wadau muhimu wako katika mgomo wa kupigania kuboreshwa kwa mazingira bora ya kazi.

JF imekua sana. Wanachama wa leo karibu ni zaidi ya mara 15 ya wanachama wa mwaka 2007. Wako waliotoka ujana kuja utu uzima na wako waliotoka dalaja la kukosa taarifa kuja kwenye ulimwengu wa habari (hasa mitandao/simu). Hawa wote wanaweza kuwa hawajui mlolongo wa matukio na historia nyuma ya Watendaji kugoma kuboresha mazingira (vifaa, huduma, maslahi ya watumishi, n.k) au kupolomoka kwa UZALENDO wa kweli. Lakini kwa kupitia mfululizo huu ninahakika kwa kiwango fulani watafumbua mawazo na kupata mitazamo sahihi juu ya yote mawili.

Enzi za Kumkoma Nyani Giledi Mchana Kweupe!

Mon, Jul 9th, 2012

Tanzania |
Dar es Salaam-based Tanzania Heart Institute (THI) properties were sold at a public auction yesterday following the High Court's (Land Division) order to recover over 6.9bn/- the former owes the National Social Security Fund (NSSF).
Possible-buyers-look-at-hospital-equipment-and-other-items-that-were-on-sale-during-an-auction-in-Dar-es-Salaam.jpg


Possible buyers look at hospital equipment and other items that were on sale during an auction in Dar es Salaamyesterday after the High Court ordered that Tanzania Heart Institute properties be sold to recover 6.9bn/- in rent owed to the National Social Security Fund. The event was supervised by Erick Auction Mart workers. (Photo: Tryphone Mweji)
FAUSTINE KAPAMA
Daily News; Friday,August 15, 2008 @20:03
THE Court of Appeal yesterday set aside an order by the High Court's Land Division seeking to evict the Tanzania Heart Institute (THI) from the premises owned by the National Social Security Fund (NSSF).
.....
My Take:
My original position has not changed. Kitendo cha NSSF na Waziri Kapuya kutishia kuwahamisha wagonjwa kwa nguvu kilikuwa ni kitendo cha ufisadi mkubwa na matumizi mabaya ya madaraka.

Sakata la Dr. Masau: Msimamo wa Serikali na Hatima ya Taasisi ya Moyo (THI)

Dr. Ferdinand Masau (Bingwa wa Magonjwa wa Moyo na Upasuaji) aliamua kuacha kazi nzuri ya kulipa huko Marekani na kurudi nyumbani kuleta ujuzi wake na vipaji vyake ili kusaidia Watanzania wenzake. Daktari huyo alisomea chini ya Daktari Bingwa wa Kimarekani Dr. Denton Cooley ambaye ni Mwanzilishi na Mpasuaji Mkuu katika Taasisi ya Moyo ya Texas (Texas Heart Institute). Kwa wale wasiofahamu Dr. Cooley na wenzake ndio waliofanya upandikizaji wa moyo wa kwanza Marekani na kituo chake hicho kimefanya upasuaji wazi wa moyo mara 97,000 kuliko kituo kingine chochote duniani!!
dacbnite.jpg




Sasa, Mtanzania ambaye amefuzu, ana uwezo na anaweza kuishi na kuhudumia wamarekani na kulipwa "kishenzi" anapoamua kuachana na hayo yote na kuamua kurudi nyumbani kwake, ilistahili siyo tu apokelewe kwa mikono miwili bali pia kwa shukurani na kutiwa moyo. Hilo halijatokea kwa Dr. Masau na sitashangaa akiamua kufunga taasisi yake na kurudi Marekani kwani wabongo "hawana mpango wala shukurani"!

Hivi karibuni kumekuwa na majaribio ya mara kadhaa ya kuikejeli na kuidhihaki taasisi hii ya moyo na kwa namna fulani kuikatisha tamaa. Juhudi hizi zimeongozwa na baadhi ya viongozi wa Wizara ya Afya ambao wamedaiwa kukwamisha mipango ya maendeleo ya taasisi hiyo ikiwemo kukataa kutia sahihi mkataba ambao ungekiwezesha kituo hicho kuwa cha kisasa zaidi na kikitoa huduma bora zaidi.

Ninachosema ni kuwa, wakati wa malumbano na migongano isiyo ya lazima umepita. Serikali badala ya kumfanya Dr. Masau na timu yake wakate tamaa au kuona ya kuwa "wanawekewa magogo" waamue kwa dhati kuisaidia taasisi hiyo. Ilani ya CCM ya 2005-2010 inasema hivi kuhusu suala la utoaji wa huduma za jamii:

Kukamilisha mipango itakayowezesha huduma za upasuaji wa moyo kutolewa humu humu nchini. Ibara ya 66 (g)

Sasa nafasi ipo kwanini tusiitumie. Ni kweli kuwa mara nyingi Watanzania hatutukuzi vitu vyetu wenyewe ila vile vinavyoletwa na wageni. Tatizo jingine ni kuwa Watanzania hatupendi vitu vizuri, kwani tunaona hatuvistahili kwani ni "vya wazungu". Zinapowekwa nguzo za taa mtaani, watu wanazitungua kwa manati!, tunajenga barabara za lami tunataka kupitisha maboti kupita uzito unaoruhusiwa! Jamani tupende vitu vyote na tuhakikishe vinadumu tusiviharibu au kusubiri viharibike!!

Tunaiomba serikali imuwezeshe Dr. Masau na Taasisi yake kwani haya si mashindano! Kuendelea kuikandia taasisi hiyo na kuiacha ihangaike wakati ina mtu mwenye uwezo na ujuzi wa kuiongoza ni kujipiga ngwala wenyewe! Au hadi taasisi ya namna hiyo ianzishwe na mtu "mkubwa"?
Jambo la kutisha sana ni kuwa Waziri muhusika anasimama tena bila woga na kusema eti maamuzi ya kuwatoa wale wagonjwa pale THI ni sahihi kabisa wakafie mbele.
Na ajabu kubwa zaidi hata Ikulu inaridhia wakafie mbele ili Deal za watu ziendelee. Ama kweli tumekwisha! Kama sio mahakama ya Rufani hali ingekuwaje kwa wale wagonjwa ambao NSSF na serikali hii hii tunayoita yetu walitaka kuwasomba kama wanavyo peleka ma buldozer kubomoabomoa?

Mh, hili la watu kupigwa mabao India halijaanza leo wakuu. Maswali ni mengi sana lakini bahati nzuri au mbaya majibu tunayo na yametuzunguka..... Je wahusika ina maana hajatosheka? Lions Club, Wizara husika etc etc etc, jamani haijatosha tuuu?? Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni japo imechelewa!
Kama walivyosema wenzangu, na kichwa habari pia kimesema "The saga continues......"
Tusubiri kama MMK alivyosema, kwenye posti yake hapo juu mmstari wa mwisho.... Ha aha aaaaaa
Mungu Ibariki Tanzania, Mungu tubariki waTanzania!!!

....Mfano inategemea benefits za kazi husika ukiwa Tanzania, au nje.
Ukienda ndani zaidi utakutana na matatizo ya watu kama Dr. Masau, huyu nadhani ukienda kum-qn juu ya kurudi nyumbani kufanya kazi au kubaki nje unaweza pata majibu tofauti.

My take,
Kurudi nyumbani au kuwa nje na unafanya kazi kunategemea sana na kukubalika kwako na kukubali mazingira husika sehemu unayopenda kufanyia kazi, hivyo hakuna ulazima wa watu kuelekezwa na kulazimishwa wapi sehemu ya kufanyia kazi.

HII ITAPUNGUZA VIFO KWA WAGONJWA WA MOYO NA GHARAMA ZA USAFIRISHAJI INDIA.INABIDI TUWAPONGEZE NA KUWAPA MOYO WAENDELEE.
source;habari katika picha:HabariLeo | Gwiji la Habari Tanzania

Ni porojo za kisiasa kudai THI haina wataalam - Dk Masau

2007-04-08 11:24:07
Na Joseph Mwendapole
Wakati serikali ikisisitiza kuwa Taasisi ya Moyo Nchini (THI), haina sifa za kufanya upasuaji wa moyo, Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Dk. Ferdinand Masau amesema kauli hizo ni za kisiasa na kwamba hazimzuii kuendelea na shughuli zake.

Amesema taasisi yake ina vifaa na madaktari bingwa wa kutosha kufanya upasuaji wa moyo na kwamba yanayozungumzwa kuwa haina sifa ni uzushi mtupu.
Akizungumza na Nipashe jana, Dk. Masau alisema anashangaa kuona Naibu Waziri wa Afya, Bi. Aisha Kigoda akisema kuwa taasisi hiyo haina sifa za kufanya upasuaji wa moyo wakati hajawahi hata kufika kwenye taasisi hiyo.

Bi. Kigoda alisema msimamo wa serikali ni uleule kuwa taasisi hiyo bado haijawa na hadhi ya kufanya upasuaji wa moyo kutokana na kutokuwa na vifaa muhimu.

``Ile ni hospitali binafsi...serikali haiwezi na haina mpango kama huo, hospitali ni nyingi za watu binafsi tutasaidia ngapi?``alihoji Naibu Waziri, Bi. Aisha Kigoda

Aidha, alisema THI haijawa na hadhi ya kufanya upasuaji wa moyo kwa kuwa kuna vifaa vingi vinavyohitajika ambavyo taasisi hiyo haina.
``Kuna vitu vingi vinavyohitajika, vifaa, madaktari na wataalamu mbalimbali,`` alisema.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, alitembelea taasisi hiyo hivi karibuni ambapo aliimwagia sifa kemkem na kuahidi kuisaidia kwa hali na mali.
SOURCE: Nipashe
 
sheria ni kama utando wa buibui,too strong for the weak and too weak for the stronger!
Huyu Dr Ferdinand Masau natibu wagonjwa ambalo ni neno zito na huduma ya uhakika.
Ili kutenda haki ni vizuri tukafahamishwa kwa nini hajawalipa NSSF pango la 6 BILLION tanzania shillings?
 
sheria ni kama utando wa buibui,too strong for the weak and too weak for the stronger!
Huyu Dr Ferdinand Masau natibu wagonjwa ambalo ni neno zito na huduma ya uhakika.
Ili kutenda haki ni vizuri tukafahamishwa kwa nini hajawalipa NSSF pango la 6 BILLION tanzania shillings?
KOMBESANA,
Umenena vema na tena sahihi kabisa juu ya sheria. Jibu lako kwa nini deni limetokea, kukua na kushindwa kulipwa linapatikana katika quotes nilizotoa; lakini kwa ufupi limelala katika ahadi na vivutio vya mdomo wanavyohadaiwa Watanzania wanapokutana na Wakuu wetu nje ya nchi.
 
Serikali ya CCM kwasababu ya kuishi ki-CULT inaua taaluma za wengine kwasababu wanaogopa watapendwa na

Wananchi, na kwasababu CCM Viongozi wao ni Dhaifu hao wenye taaluma watachukua Utawala...

Lakini huyu Dr. Masau alikuja kuisaidia nchi kutopoteza hizo DOLLAR kwenda kutibu watu nje ya nchi; lakini Wizara

ya Afya Mafisadi wengi 10% ni powerful hadi IKULU wanaijua; they just kill him technologically...

Sio yeye wako wengi sana... CCM inatakiwa iondolewe Madarakani; kwanini hadi leo hawataki kutatua matatizo ya

Umeme? Matatizo ya Usafiri Dar? matatizo ya Usafiri Mikoani watu wanakufa? Matatizo ya Maji? ni ULAJI
 
Taasisi ya Moyo Tanzania yafungwa...mali za pigwa mnada... Jengo apewa mwekezaji angalia katika Picha hapo... kwa maana hiyo kwa sasa Mwendo kwenda India ni kama kawa...?
Mwenye taarifa za Taasisi hii kufungwa tunaomba atujuze.
 

Attachments

  • THI.jpg
    THI.jpg
    31.5 KB · Views: 168
Naona finally Wizara imefanikiwa kumuangusha Dr Shayo ktk huu mradi wake uliokuwa ukiwasaidia sana watu masikini wenye matatizo ya moyo. Baadhi ya Viongozi wa Wizara ya Afya walikuwa hawapikiki kabisa na mmiliki wa hii hospitali, na jamaa waliahidi wangemtia adabu na wamefanikiwa kweli!
 
Hivi ndivyo Unafiki na wivu unavyo rudisha nyuma maendeleo.
 
Naona finally Wizara imefanikiwa kumuangusha Dr Shayo ktk huu mradi wake uliokuwa ukiwasaidia sana watu masikini wenye matatizo ya moyo. Baadhi ya Viongozi wa Wizara ya Afya walikuwa hawapikiki kabisa na mmiliki wa hii hospitali, na jamaa waliahidi wangemtia adabu na wamefanikiwa kweli!

wanasema usishindane na serikali, lakini si kwa mambo ya kishenzishenzi namna hii. hii ni laana kwa nchi.

hawa watu wanafurahi sana wakiona mtu anajitangaza kwa tv kuomba msaada wa kwenda kutibiwa india?

why?
 
Taasisi ya Moyo Tanzania yafungwa...mali za pigwa mnada... Jengo apewa mwekezaji angalia katika Picha hapo... kwa maana hiyo kwa sasa Mwendo kwenda India ni kama kawa...?
Mwenye taarifa za Taasisi hii kufungwa tunaomba atujuze.

So, Interesting... Nimeweka hii topic Mapema kabla yako na imehamishwa kwasababu sio ya KISIASA lakini

Yako bado ipo hapa ....???
 
wanasema usishindane na serikali, lakini si kwa mambo ya kishenzishenzi namna hii. hii ni laana kwa nchi.

hawa watu wanafurahi sana wakiona mtu anajitangaza kwa tv kuomba msaada wa kwenda kutibiwa india?

why?
ili mjue kuwa selikali iliyojiweka madarakani ipo na inatoa ruzuku apollo indiaaaaaaa!
 
ili mjue kuwa selikali iliyojiweka madarakani ipo na inatoa ruzuku apollo indiaaaaaaa!

Tena manesi na madaktari huwa wanafurahia sana wanapoteuliwa kusindikiza wagonjwa India maana huko kwa kipindi chote wanachokaa, kwa siku huwa wanalipwa si chini ya dola 280, Mtu ukikaa zako mwezi, akhaaaaaaa maisha baridiiiiiiiiiiiiiii!
 
Naona sasa wamedhamiria kuuwa sekta ya afya nchini baada ya hapo mishen zijiandae, huu ni utekelezaji wa ilani ya chama chetu cha kijani. "Selikali makini ingeungana na huyu dr. Wa myoyo"
 
Tena manesi na madaktari huwa wanafurahia sana wanapoteuliwa kusindikiza wagonjwa India maana huko kwa kipindi chote wanachokaa, kwa siku huwa wanalipwa si chini ya dola 280, Mtu ukikaa zako mwezi, akhaaaaaaa maisha baridiiiiiiiiiiiiiii!
hizo per diem ni tatizo mkuu
 
Kuna mhindi analitaka ametumia kila njia kuhakikisha anamuangusha huyu mtanzania mzalendo..ndio watanzania tuanteswa na wakuja nchini kwetu kutokana na fedha walizotuibia
 
Back
Top Bottom