Zambi ataka serikali ilazimishe wasomi wa KiTZ warudi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zambi ataka serikali ilazimishe wasomi wa KiTZ warudi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lunyungu, Aug 15, 2008.

 1. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #1
  Aug 15, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Leo mapema nikiwa ndani ya ukumbi wa Bunge , ndugu Zambi alisimama kuchangia na akataka kujua kwa nini Serikali isitumie nguvu kuwarudisha nyumbani ma expert wote watanzania wanaofanya kazi nje ya Nchi na kupata kipato kikubwa .Haya yalizuka baada ya Bunge kuelezwa kwamba watu wakisha soma Ulaya hubakia na kupata mishahara minono huko .
  Kombani kasimama na kusema serikali inaweza kusema nasi kwa utaratibu wa kutuomba na si kuomba kwa nguvu tunyimwa ajira .Huyu Zambi nimeshangaa uwezo wake wa kuelewa mambo .Mwaka 2008 yeye anafikiria miaka ya 60 ? Wewe unasemaje ?
   
  Last edited by a moderator: Aug 15, 2008
 2. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #2
  Aug 15, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  He Mkuu Lunyungu, Zambi alikuona akaamua kukurushia kijembe au ni coicidence tu?!?
   
 3. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #3
  Aug 15, 2008
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,505
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 135
  Kasema hayo maneno au wewe umeongezea tu na kuja na title zako tu?Mwanakijiji nadhani anafaa kuwa Mwandishi wa Lowassa kwa sasa.
   
 4. G

  Ghwakukajha Senior Member

  #4
  Aug 15, 2008
  Joined: Apr 27, 2008
  Messages: 172
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Ndo yaleyale,ya kuangalia tulipoanguka badala ya pale tulipojikwaa.Ni muhimu kuchunguza kiini hasa cha experts hawa kubaki nje ya nchi.Je ni maslahi?Usalama wao(tindikali?),au ni lipi hasa?Kisha hatua za makusudi zichukuliwe ktk kurekebsha pale palipo na tatzo.Nakumbuka msemo mmoja unaopenda kutumiwa na walemavu(no offence) kuwa "nothing about us without us" hapa nadhan ktk kufanya mabadiliko haya,hao experts washrkshwe kwa ukaribu.Sasa kaul za kuendelea kulalamikia brain-drain litakuwa ni kibwagizo tu,kama hatua za maksudi haztachukuliwa.
   
 5. Mambo Jambo

  Mambo Jambo JF-Expert Member

  #5
  Aug 15, 2008
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 1,100
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Sioni ubaya ni kwa nini wasirudi, cha msingi hapa ni kuwashawishi warudi na kupatiwa ujira mzuri, sasa wewe uko nje ya tanzania kwa ajili ya masomo, ukisha maliza masomo basi rudi nyumbani kasaidie kujenga inchi kwa utaalamu elimu na exposure uliyopata, daima inchi hujengwa na wenye inchi....narudi tena serikali itengeneze mazingira mazuri ya kuwashawishi na kuwalipa ujira mzuri, ikifanya hivyo hakika watarudi, nani anayefurahia baridi, vyakula vya kopo, maisha ya speed ya ajabu, kazi zisizopungua watu wanafanya hivyo kwa ajili ya maisha....wanandugu na jamaa ambao wanawategemea nyumbani Tanzania...watu wanatamani kurudi nyumbani, kunjwa kilimanjaro baridi, nyama choma na vyakula fresh na vitamu vya nyumbani....wanatamani kurudi na kufanya kazi masaa nane...kinachoshindikana ni ujira mdogo....ni hayo tuu
   
 6. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #6
  Aug 15, 2008
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Lunyungu, good to see you back.

  Namuunga Zambi mkono in principal kwamba wale wote waliosomeshwa na serikali huku nje warudi kuitumikia Taifa japo kwa muda fulani kama kurudisha fadhila and offcourse kujenga nchi. Sioni kama ni matumizi makini ya kodi za wananchi iwapo hela zinatumika kusomesha wananchi nje halafu hawarudi kuwatumikia wananchi waliowasomesha.

  Sasa tunaweza kujadili iwapo kubaki nje ya nchi kunaweza kuongeza uzalishaji Tanzania kwa namna moja au nyingine.

  Katika kuonyesha kujisafisha na lawama za kuiba wasomi waliosomeshwa na Serikali zao; waingereza wakaja na utaratibu kuwa iwapo umesomeshwa na Serikali au British Council ni lazima wakupe barua ya kukuruhusu kufanya kazi UK kabla hawajakubalia kukupa Work Permit. Sasa kwa kiasi fulani naona iwapo hii itafuatiliwa na makini kuliko ilivyo sasa inaweza kurudisha kodi za wananchi japo kidogo.

  Ukiwa mwingereza ukaenda kufanya kazi nje, sehemu ya mshahara wako inaingia kwenye serikali yako. Kwa maana ya kwamba haijalishi upo wapi, ili mradi unazalisha kipato pale ulipo basi serikali/ wananchi wako inafaidika moja kwa moja.

   
 7. Bubu Msemaovyo

  Bubu Msemaovyo JF-Expert Member

  #7
  Aug 15, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 3,436
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Hayo ni mawazo yaliyopitwa na wakati kwasababu pale Mlimani wasomi wanaelezwa kabisa SOMA ILA AJIRA HAKUNA. Sasa huyu jamaa akipata ajira huko nje anaanza kukodolewa mimacho na viongozi wanapotembelea mataifa hayo. Ushauri wangu ni kwamba Serikali irudi katika sera zake kuajiri hao ma-expert badala ya kuwaacha eti waunde NGO zao hapa nyumbani. Mnawasomesha wa nini wakati hamtaki kuwaajiri? Mbona kwenye mikutano yenu mnasema ajira hakuna sasa afanye nini awe Machinga? Hoja nyingine Bw.
   
 8. K

  Kijunjwe Senior Member

  #8
  Aug 15, 2008
  Joined: Mar 3, 2007
  Messages: 182
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hoja husika inaungika mkono kwa kuangalia baadhi ya mambo na kuna sehemu nyingine inakataa. Mfano inategemea benefits za kazi husika ukiwa Tanzania, au nje.

  Ukienda ndani zaidi utakutana na matatizo ya watu kama Dr. Masau, huyu nadhani ukienda kum-qn juu ya kurudi nyumbani kufanya kazi au kubaki nje unaweza pata majibu tofauti.

  My take,
  Kurudi nyumbani au kuwa nje na unafanya kazi kunategemea sana na kukubalika kwako na kukubali mazingira husika sehemu unayopenda kufanyia kazi, hivyo hakuna ulazima wa watu kuelekezwa na kulazimishwa wapi sehemu ya kufanyia kazi.
   
 9. streetwiser

  streetwiser Member

  #9
  Aug 15, 2008
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 30
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Kitu ulicho ongea Yebo Yebo ni sawa, kama wewe ulisomeshwa kwa pesa za walipa kodo wa TZ kwanini usirudi nyumbani kufanya kazi? hiyo system ya UK kukusanya kodi wa wanaofanya nje ya UK pia inatumiwa na South Afrika. Hivyo kama mtu atataka kubaki mtoni basi ni wajibu alipe kodi kufidia gharama ya kumsomesha.
  Pia Mh Zambi cjui atasema vipi kwa wale wapiga box wanao jisomesha wenye na si watoto wa MAFISADI?
   
 10. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #10
  Aug 15, 2008
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hivi unaweza kumlazimisha mtu afanye kazi iwe serikalini au private sector???????? Say walio nje wanaamua kurudi hizo ajira zipo???????? Serikali yetu haina hata statistics za waliohitimu elimu ya juu hata kwa mwaka mmoja tu kuhusu wako wapi na wanafanya nini hapo hapo bongo. Itakuwa walio nje????????

  Hizi ni siasa mufilisi...........Like it is said better close your mouth and let others think you are a fool rather than opening it and remove all doubts.
   
 11. H

  Hauxtable JF-Expert Member

  #11
  Aug 15, 2008
  Joined: Nov 5, 2007
  Messages: 386
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Watu aina ya Lunyungu na Mwanakijiji......Mkuu ngoja watu waseme wenyewe acha kupiga mayowe!!!
   
 12. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #12
  Aug 15, 2008
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Lunyungu

  Hii habari ndivyo hivi ilivyosemwa na huyo mhe au umeipinda??

  Iwapo alisema wale wote waliosomeshwa na serikali basi naona kuna ulazima wa kurudi au kuitumikia nchi kwa namna moja au nyingine.
   
 13. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #13
  Aug 15, 2008
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0


  Hao ndio wanaotakiwa kubembelezwa warudi nyumbani maana hiyo investment ya elimu wameingaramia wenyewe.
   
 14. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #14
  Aug 15, 2008
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Mhe hii ni dhana potofu ya kusema unasoma ili uje kuajiriwa. Inabidi tubadilike kwa haraka sana kama tunahamu ya maendeleo ya kweli.

  ELIMU sio lazima uje kuajiriwa ndio unufaike nayo. Mimi naona ni muhimu serikali iendelee kusomesha wananchi wake kuanzia msingi mpaka chuo kikuu. China na mataifa mengine yaliyoendelea walifanya hivyo na leo wapo mbali.

  Elimu kwanza hayo maswala ya ajira ni matokea, lakini ukiwa na elimu na ukaamua kuitumia vizuri hata ukiuza genge hautakuwa sawa na muuza genge mwenzako asiye na elimu.
   
 15. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #15
  Aug 15, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kwa kuwa Mkuu Lunyungu yupo hapa, na yeye ni mmoja wa hao walioseek greene pastures, basi atujibie swali hili
   
 16. Bubu Msemaovyo

  Bubu Msemaovyo JF-Expert Member

  #16
  Aug 15, 2008
  Joined: May 9, 2007
  Messages: 3,436
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mantiki ya maoni yangu haijapendekeza serikali iache kusomesha nilichobeza ni pale President anapowakuta wananchi wake huko nje wakitengeneza maisha yao halafu yeye ana come up na idea kwamba warudi waijenge nchi yao. Waijenge kivipi na wao wameajiriwa kule?
   
 17. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #17
  Aug 15, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Mkuu YeboYebo
  Salaam toka Dodoma .Umeuliza kama ndivyo alivyosema Mkuu Zambi nami nasema nime translate maneno yake maana Zambi anajua kuwa Yebo yebo, Lunyungu , Mwanakijiji , Jasusi na wengine ndipo nikaamua kutoka nje na kuwatumia ujumbe huu .Zambi alijawa na jazba na alitaka kusema asikike kama yuko Bungeni , alionekana akiwa na huzuni maana anasahau kwamba sisi watoto walalahoi hatuwezi kupata kazi Ikulu , Usalama wa Taifa , BoT,TRA nk .Ndiyo maana sisi tumeamua kuingia mitini na hata baada ya kuitumikia Tanzania kwa moyo wangu wote .

  Sasa hii ndiyo habari yenyewe toka Dodoma
   
 18. streetwiser

  streetwiser Member

  #18
  Aug 15, 2008
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 30
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Binafsi nimfahamu Zambi tangu alipokuwa akifanya TAZARA na nilikuwa karibu nae alipokuwa akifa post graduate ya law pale Dar Hill, yeye pia ni mtoto wa mlala hoi kama cc, maadam Lunyungu upo dodoma muulize afafanue lengo la issue yake, na kama una wasiwasi wa kufahamika nadhani unajua cha kufanya ili uweze kupata ufasaha wa mada yake.
  Huenda ukawa umehitimisha kivyako lakini hakuwa na lengo hilo.
   
 19. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #19
  Aug 15, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Yebo Yebo,

  Haturudi ng'o hata mtufunge kamba. Tutaendelea kufaidi pesa zetu Ulaya kwi kwi kwi!!!

  Wanatakiwa watumie power of percussion and not power of coercion.

  Watuache tuendelee kubeba mabox yetu.
   
 20. Pezzonovante

  Pezzonovante JF-Expert Member

  #20
  Aug 15, 2008
  Joined: May 1, 2008
  Messages: 643
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kama Kweli Tunapinga Kwa Dhati Ufisadi Na Matumizi Ya Ovyo Wa Pesa Za Uma Zambi Anapoint Pale,kukaa Njee Bila Kuja Kuwajibika Home Ni Ufisadi Nao Huo
   
Loading...