Muhimbili Wafanya Upasuaji Wa Moyo

Jim

Member
Mar 7, 2008
70
4
Operation za moyo zimekuwa zikifanyika hapa nchini muda mrefu tu ndugu yangu. Swala sio operation ya moyo. Swala ni nini kinafanyika kwa maana ya complexity ya procedure yenyewe. Lakini kama ni kugusa tu moyo hizi zimekuwa zikiendelea nyingi.
 

kalld

Member
Jun 14, 2007
87
0
jim
hebu nifafanulie kuna operation na kugusa moyo?
nafahamu operation za moyo zinafanyika KCMC na kwa dr masau .sikujua kama muhimbili wanafanya operation za moyo na ndio maana nikawapongeza.
 

Jim

Member
Mar 7, 2008
70
4
Wakati Dr. Massawe alipofanya op ya moyo kwa mara ya kwanza na kutangazwa kama pioneer. Madaktari wa MMC (wakati huo) walimjibu kwamba hizo operation za kiwango hicho zimeendelea kwa muda nchini and there was nothing new about it then. There isn't now.
 

ZeMarcopolo

JF-Expert Member
May 11, 2008
14,005
7,180
Kama wanafaya kwa kutumia cardio-pulmonary bypass basi ni big step forward!
Hongera Muhimbili.
 

Kinyau

JF-Expert Member
Nov 24, 2006
908
681
mtangazaji mmoja jana aliniacha hoi baada ya kutangaza Hospitali ya muhimbili imeanza kufanya MAJARIBIO YA UPASUAJI WA MOYO. Yaani majaribio? on who' s heart? unless they tell us majaribio on rats and dogs and not human beings' precious organs. I beg you guys dont take your hearts for majaribio.
 

Kinyau

JF-Expert Member
Nov 24, 2006
908
681
by the way bado kuna utata mwingi serikali(wizara ya afya) inashindwa kutuambia kwa nini Dr masau apewi ushirikiano katika kutoa huduma za upasuaji wa moyo. Bado focus ni kupeleka watu njeee weee.
 

Ngereja

JF-Expert Member
Feb 27, 2007
798
332
Mbona habari zinasema hiyo operation ya moyo ilfanywa na Dr. Masau? walimkodi kwenda kufanya hiyo operation?
 

Mama Lao

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
238
5
mtangazaji mmoja jana aliniacha hoi baada ya kutangaza Hospitali ya muhimbili imeanza kufanya MAJARIBIO YA UPASUAJI WA MOYO. Yaani majaribio? on who' s heart?
...wako sahihi ..wanafanya majaribio na sisi ndio "guinea pigs" wao. Mpaka hapo watakapojiamini na utaalamu waliofundishwa huko India.
 

Lambardi

JF-Expert Member
Feb 7, 2008
12,925
10,426
Hapo kuna walakini na kikoroshoo...maana walimsema vibaya dr mwenzao....alipotangaza anafanya op za moyo..ila wao wamemualika hata PM....politics kwenye proffessional???
 

mkama

Member
Oct 19, 2007
67
9
Habari za uhakika ni kwamba dr masau hakualikwa.aliyeongoza upasuaji wa moyo ni dr.Mahalu.huyu ni mmoja ya madactari wazawa ambae hapo awali alikuwa akifanya upasuaji wa moyo nchini Zimbabwe,na alikuwa akiheshimika saana nchini humo.

Swala la kuwa operation za moyo zilikuwa zikifanyika,nusu ni kweli na nusu si kweli.Hapo awali kilichokuwa kikifanyika ni upasuaji mdogo wa moyo kama kuondoa ganda la juu la moyo yaani pericardioctomy hapa moyo hauguswi ndani,na alikuwa akizifanya Prof L,Lema wa muhimbili, na labda kufunga vitundu vidogo ambavyo watoto wengine huzaliwa navyo yaani pantent ductus arteriosus.

Tofauti na KCMC ambayo hutegemea wataalam kutoka marekan,sasa kinachofanyika Muhimbili ni OPEN HEART SURGERY ambayo ni operation kubwa ya moyo,moyo unafunguliwa ndani kurekebisha shida husika,na kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi imefanywa na madaktari,na manesi wazawa ambao wamesomeshwa na hela ya watanganyika.Hili ni jambo la kujivunia ambalo nilitegemea lingepata postive publicity kama iliyotolewa kwa Ile ya SAGA ya MOI yaani Emmanuel Mgay et al.

Kwamba ni majaribio,si kweli watu hawa wametrain vyema,kuna wazoefu wawili kama nilivyokwisha eleza,Dr Mahalu na Dr.Wandwi huyu ni mzawa,katrein na kufanya kazi Israel kwa mda wa takriban miaka mitano au saba kama sikosei.Kwa pamoja naamini watasaidiana na hawa vijana walotrain India.

Kwamba Dr.Masau anabaniwa na Serikali,sidhani kama ni kweli nafikiri pia yeye hana ushirikiano na wenzake.Nilipata bkuambiwa na nikashuhudia mwenyewe-yeye anatibu kama kadiologist,halafu kama kadiac surgeon na pia kama kadothoracic surgeon.Kwa mazingira ya kawaida na hata ya nchi zilizoendela hamna mtu anaeweza kufanya kazi hivyo na nafikiri ya Dr.Masau inastahili kuitwa MADE IN TANZANIA

Rai yangu,tuwaunge mkono na tuisihi serikari iwape msaada sitahili.Pia imsaidie Masau afikie lengo lake kwa wote wakiweza anaefaidika ni mtanzania

Nawasilisha
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom