Taasisi ya Moyo Tanzania yafungwa!

Tutafute ukweli kabla ya kulaumu kwani tutatetea mambo yasiyofaa kutetewa. Dr. Masau alikuwa amefika point ya kutosaidika kutokana na kujisahau kama ilivyo kawaida ya Watanzania tuliowengi. Ilifika wakati bodi ya hospitali ikakaa pembeni maana alikuwa hasikilizi mtu yeyote!

Kwa uzito wa majukumu iliyokuwanayo THI isingewezekana tena kuendeshwa kama mali binafsi ya kuhesabu mapato na matumizi mfukoni. Dr. Masau alikataa shauri mbalimbali alizopewa za namna ya uendeshaji bora wa THI. Mpaka kufika hapo kumekuwa na mambo mengi lkn yote yalipita kuashilia sikio la kufa.
 
Naamini serikali inania ovu na wananchi wake, na hii inawezakuwa ni kwa maslahi ya Mafisadi na maafa kwa watanzania,
 
We unatukana anayeumwa kama alipenda!!! yatakupata hayo unayoyacheka mana ni kwa neema tu upo hivyo. Si wewe tu bali yeyote yule ktk ukoo wako hakika atapata maradhi makubwa ili iwe fundisho dharau zako shetani wewe.

Mkuu niseme tu kuwa hujaisoma comment yangu vizuri au la hujaielewa especially kwenye mabano, otherwise usingekuwa na sababu ya kuwa that much emotional! ipitie tena comment yangu mkuu!
 
Msilete majungu katika mambo msiyoyajua, huyo Dr Massau ni tapeli zaidi ya tapeli bora ifungwe tu hiyo taasisi.

Tena mkinikera nitamwaga mafaili yake hapa hizi siasa zisiwafanye muwe vipofu kushindwa kuona right na wrong!
 
Mwanakijiji,

Hata kama ni mtaalam kweli ndio asilipe madeni anayodaiwa? Mbona tunataka kuibebesha serikali lawama zisizohusu?
 
Hiyo THI ingekuwa na sifa tusingekuwa tunapeleka watu India, walete statistics zao hapa kwanza wameshafanya surgery ngapi?

Wacheni ushabiki wabongo pale kulikuwa hamna kitu ni hospitali ya kusaidia wagonjwa wa moyo wasukume siku tu walale kwenye vitanda vyao watozwe mahela mengi.

Kwanza uliona wapi hospitali ya moyo inapakana na Club ya starehe ambapo makelele from time to time hayaepukiki tena usiku kucha!! Nadhani na serikali ilikosea kumpa Dr Massau kibali ilitakiwa wamnyime.
 
Ama haya ndio maboresho ya sekta ya afya tanzania? Kwamba...tunaanza kwa kufunga taasisi kama hizi ili wote tukatibiwe Apollo huko India?
 
wewe nawe siku hizi akili zako kama za williy malecela...ukishaingia ccm bana akili zinahama kabisa.....

Mtu mzima Yo Yo,

1. Kwenye mgogoro wa THI na NSSF, Dr. Masau ndio mwenye makosa. Pesa alizokuwa analipia pango zilikuwa zinatoka kwa wafadhili Ujerumani. Wafadhili hao walikataa kuendelea kutoa pesa baada ya Dr. Masau kutokutekeleza wajibu wake wa kupanga kwenye jengo linalokidhi viwango walivyokubaliana. Matokeo yake akakosa pesa zza kulipa pango. Ukishidhwa kulipa pango unatolewa kwenye jengo, its that simple.

2. NSSF siyo charity organisation. Wanahitaji lile jengo kwa ajili ya uwekezaji.

3. Dr. Masau asitafute wa kumlaumu kwa sababu tatizo kubwa ni kwamba alikuwa NAIVE na akawa anatuymia theory kuliko uhalisia. Sasa uhalisia anaujua, so atafute tena definition ya uwezo wake.

4. Kulikuwa na mkataba kuwa serikali imshaidie kuendesha hiyo hospitali tangu kipindi cha Anna Abdallah kama waziri wa afya, lakini Masau alikataa vipengele vinavyompunguzia nguvu za maamuzi. Sasa ana nguvu zote za kuamua anachotaka, asimlaumu mtu kwa sababu kwake yeye nguvu za maamuzi zilikuwa muhimu kuliko huduma kwa wagonjwa.
 
kwa hiyo unafurahi kakomolewa? naona kama hoja zako zimekaa kaa kama vile..ukome!

Sifurahii kukomolewa na siamini kama kakomolewa, ila natambua kuwa amefanya makosa na anachokutana nacho ni matokeo ya makosa aliyofanya. Sio sahihi kulaumu watu wengine kwa makosa yake.
 
Mmh! Watanzania tuanze kuomba sana kila mtu kwa imani yake maana naona mambo yote yanageuka nyuma ndo kunakuwa mbele sasa, tutafika?
 
Wanaoijua vema Taasisi hii na namna kiongozi wake alivyokuwa anawatumia wagonjwa wa Moyo, kama chambo cha kufanikisha mambo yake, Wataunga mkono saaana kufungwa kwake. Hata Hivyo ukifanya biashara ni lazima ulipie gharama zake, ikiwa pamoja na pango la nyumba! Hongera sana waliofanikisha kufungwa kwa Taasisi Hii
 
Naona finally Wizara imefanikiwa kumuangusha Dr Shayo ktk huu mradi wake uliokuwa ukiwasaidia sana watu masikini wenye matatizo ya moyo. Baadhi ya Viongozi wa Wizara ya Afya walikuwa hawapikiki kabisa na mmiliki wa hii hospitali, na jamaa waliahidi wangemtia adabu na wamefanikiwa kweli!
Ugomvi nadhani ulikuwa ni ile tenipasenti ya wagonjwa wanaoenda kutibiwa nje........serikaili badala ya kuifadhili iweze kuendelea ndio kwanza inaididmiza.............Mungu awalaani waliohusika
 
Hizi ni habari mbaya sana. Nakumbuka ni katika Hospitali hii mwenzi wangu wa maisha alipata suluhisho la matatizo ya ugonjwa wake wa moyo baada ya kuchoka majigambo ya Dr. Rwakatare ambaye pamoja na kuwa na bei chafu ya huduma yake, bado ananyodo kupita kiasi. Tulipoanza kupata matibabu kwenye hospitali hii, baada ya muda mfupi alipata nafuu na hatimae tatizo kutoweka baada ya kutumia kwa muda dawa alizopewa.

Pamoja na hayo, sijui ni kwanini serikali inalaumiwa katika kufungwa kwa hii hospitali. Je ni kwa kuwa wizara ilikuwa inaipiga vita hii hospitali kwani ilikuwa inaingilia ulaji wa watu kwani badala ya kwenda India wangeweza kutibiwa hapa? Je ni kwa kuwa serikali iliendelea kuwapeleka watu India ingawa wangeweza kupata hiyo huduma hapa na hivyo kufanya malengo ya kuanzishwa kwa hospitali hii yasifikiwe (it was under capacity operating/under utilized) hivyo kutoweza ku-break point?

Je tunajua tumeisha jiuliza ni kwanini Dr. Masau alikuwa alipi kodi ya pango? Kuna maswali mengi zaidi ya majibu hivyo nasita kuilaumu serikali kwa hatua ya kuuzwa mali za Hospital unless nipate maelezo ya kutosha.

Tiba
 
Nimesikitishwa sana na taarifa hii, naujua umuhimu wake kwa walala hoi. Niliwahi kumshauri jamaa yangu ampeleke kijana wake hapo kwa matibabu ya moyo baada ya kupigwa kalenda za kutosha na maafisa wa W/Afya. alifanya hivyo na mpaka leo anafuha sana juu ya afya ya mwanae.

Ni pigo lingine kwa wanyonge wa nchi hii.
 
Hizi ni habari mbaya sana. Nakumbuka ni katika Hospitali hii mwenzi wangu wa maisha alipata suluhisho la matatizo ya ugonjwa wake wa moyo baada ya kuchoka majigambo ya Dr. Rwakatare ambaye pamoja na kuwa na bei chafu ya huduma yake, bado ananyodo kupita kiasi. Tulipoanza kupata matibabu kwenye hospitali hii, baada ya muda mfupi alipata nafuu na hatimae tatizo kutoweka baada ya kutumia kwa muda dawa alizopewa.

Pamoja na hayo, sijui ni kwanini serikali inalaumiwa katika kufungwa kwa hii hospitali. Je ni kwa kuwa wizara ilikuwa inaipiga vita hii hospitali kwani ilikuwa inaingilia ulaji wa watu kwani badala ya kwenda India wangeweza kutibiwa hapa? Je ni kwa kuwa serikali iliendelea kuwapeleka watu India ingawa wangeweza kupata hiyo huduma hapa na hivyo kufanya malengo ya kuanzishwa kwa hospitali hii yasifikiwe (it was under capacity operating/under utilized) hivyo kutoweza ku-break point?

Je tunajua tumeisha jiuliza ni kwanini Dr. Masau alikuwa alipi kodi ya pango? Kuna maswali mengi zaidi ya majibu hivyo nasita kuilaumu serikali kwa hatua ya kuuzwa mali za Hospital unless nipate maelezo ya kutosha.

Tiba
Daktari!
Huyu Daktari mali ya msaada aliifanya yake na alikuwa mbinafsi kupita kiasi halipi hata wafanyakazi wake,halipi kodi ya nyumba anayoendeshea shughuli zake halafu anataka saini kutoka wizarani ili misaada ya kifedha itoke na akiipata inashia kwake tu ,wizara ilifanya hivyo mara moja na waligoma kuendelea kugeuzwa rubber stamp ya yeye kujinufaisha.Wafadhili ndiyo wakagoma kuleta mshiko.Mimi naamini hajafilisika atarudi mlango mwengine kwani naye alikuwa akijua hiyo Taasisi itafilisiwa na alikuwa akiweka pingamizi mahakamani kwa kuvuta muda na kujipanga.
 
Back
Top Bottom