Maadam THI wameshindwa kulipa deni walokopesha mkuu wangu tutashindwa kuwatetea isipokuwa haya matatizo yana mwanzo wake ambao nyie wenyewe hamtaki kutazama upande huo, mmelifumbia macho kabisa tatizo linakoanzia wakati mnajua fika wapi tumeharibu...
Sababu kubwa ya kushindwa ama kufa kwa THI ni fedha - wameenda Bankrupt! na pengine credit yao mbovu vile vile maana kufikia kunadiwa mali zao sijui tuwahurumie vipi wao ama wananchi..Makosa yapo ktk muundo wa AFYA nchini (the making of EL wenu mnayemsifia sana. Kama serikali inaunda Muafaka na makanisa wakati fedha zote za mikopo na grants zinazotolewa nchini Hospital za watu binafsi hazipati kitu hata tax exemptions sasa mnategemea nini kitokee maana tukisema wengine mnasema ni Udini na Uislaam. Ukiuliza utaambiwa hii THI ilikuwa private, sijui hizo za makanisa sio private? Haya madaktari wanagoma hadi Bugando ukiuliza ati wanaunga mkono wenzao, jamani jamani tunadanganyana nini hapa?..
Lini Private hospital doctors wanaweza kuingia ktk mgomo wa watumishi wa serikali ktk mafao yasiyowahusu?, lini madaktari wa private wakagoma kwa madai ya vifaa vya kutendea kazi ikiwa Hospital zao hazihusiki wala hazina matatizo hayo?. Tusidanganyane...Something has to be done nacho ni kuua kabisa hii bureaucracy na kuunda Upya mfumo mzima wa Elimu na AFYA otherwise kuna walimu wanakuja nao na mgomo, utasikia hadi shule za makanisa wakigoma kosa bado ni la JK...
Fedha zipo lakini inakuwa allocated kwa mambo mengine kabisa tena bado ni matumizi ya kawaida halafu tunailalamikia serikali ya JK afanye nini yeye ikiwa wananchi wenyewe hamtaki kuona muafaka unakufa?. Hii ni sawa kabisa na wakazi wa bondeni Jangwani ambao wamekufa kwa mafuriko wakaambiwa wahame wakakataa katakata na wananchiu mkawaunga mkono, yametokea tena mafuriko wakafa wengine imekuwa kosa la serikali, wasamaria wema wakaweka kambi zao kusaidia huku wakiilaumu serikali kutowahamisha watu wale. Yaani tafran tupu, maana matukio mengi nchini ni ya kujitakia sisi wenyewe.