Yo Yo
JF-Expert Member
- May 31, 2008
- 11,210
- 1,719
WAGONJWA WA KITANZANIA WANAOTIBIWA NARAYANNA HOSPITAL BANGALORE ,INDIA.
Mwezi wa saba mwaka 2008 huu tarehe za 21/22 Watanzania 17 wagonjwa wakiongozana wa wasaidizi wao 11 waliondoka nchini kuelekea nchini india kwa ajili ya kupatiwa matibu ya ugonjwa wa moyo katika hospitali iliyo katika mji wa Bangalore huko India,wagonjwa hao wengi wao wakiwa ni watoto na watu wazima wachache.
Kwa mujibu wa habari zinazofahamika nchini Tanzania wagonjwa hao waliweza kwenda kutibiwa nchini India wa ushirikiano kati ya Regency hospital chini ya Dr Kanabah na Lions club ambaye mwenyekiti wake ni Dr Yusuph Dalali,wagonjwa hao walifika katika hospitali ya Narayanna na kuanza matibabu yao kama kawaida kwani tayari walikuwa wameshafanya malipo yao nchini Tanzania .
Wakati matibabu hayo yakiwa yanaendelea yalijitokeza matatizo ambayo yaliweza kusababisha baadhi ya wagonjwa matibabu yao kusimamishwa kwa muda,hii ikiwa na maana kwamba fedha ambazo narayana hospital ilizipokea kutoka nyumbani Tanzania zilikuwa zinawezesha kutibu wagonjwa wachache kulingana na fedha zenyewe,hali ilipozidi kuwa ngumu ilibidi wagonjwa kutaka kujua ni kiasi gani cha fedha kilitumwa kutoka Tanzania? Na je kiasi hicho kilichotumwa kinaonyesha nani aliyelipa na nani asiye lipa? Jibu la hospitali likawa fedha ni ndogo ,ikabidi baadhi ya wagojwa waweze kutolewa wodini mpaka hapo fedha zitakapotumwa .
Habari zisizo rasmi zinazoendelea nikwamba fedha zimeshatumwa wagonjwa wawili ndio watakao weza kufanyiwa upasuaji siku yeyote kuanzia jumatatu ya 18/08/2008 Bw Robert Kewel na Bw Wilfred Kirika Laizer , mwingine imeonekana hana ugonjwa wa moyo kabisa na wala hana tatizo la aina yeyote kulingana na vipimo vya Narayanna hospital ambaye ni bwana Chacha,na mwingine imeonekana kuwa anatatizo la miguu kujaa maji inabidi kurudi nyumbani ,arudi tena Narayanna hospital baada ya miezi sita bw Athmani Juma Abdallah,kwa mujibu habari zilizopo watoto wawili Abdulkarim Abdul Ipande na Ester Paulo Mwita wao jopo la madaktari limeona itakuwa ni hatari sana kuwaopereti watoto hao kulingana na hali zao,ni bora wakaendelea na dawa tu ,mtoto Abdulkarim Abdul Ipande yeye ni mara yake ya pili kuletwa Narayanna hospital,alishaletwa mwaka 2007 na mwaka huu 2008 kwa mujibu wa habari rasmi ni kwamba wagonjwa wote hao waliongozana na mkuu wao wa msafara Dr Ally Amour kutoka mnazi mmoja hospital Zanzibar ambaye pia ni daktari wa moyo.
Wagonjwa wote kwa pamoja wameshtushwa na habari zilizoandikwa na gazeti la Bangalore India,"Sunday express la jumapili 10/08/2008 ukurusa wa 3"lenye kichwa cha habari kisemacho "17 AFRICANS TREATED IN CITY", kwamba wao ni masikini sana walioshindwa kumudu gharama za matibabu nchini kwao,lions club ya Dar es salaam imegharamia matibabu ,usafiri,malazi,na matumizi mengine katika muda wote wa matibabu yao,wakizungumza kwa uchungu mbele ya wanafunzi wa kitanzania wanaosoma Bangalore University,India ambao waliwatembelea tarehe 15/08/2008 siku ya ijumaa majira ya jioni kwa ajili ya kuwapa pole,wagonjwa hao wamesikitishwa na hilo kwani wao wamejilipia usafiri wenyewe kuja na kurudi ,malazi wanajilipia wenyewe katika hostel wanazo kaa za na pia wanapika wenyewe , Shantinikethan hostel boomasandra area , wamejinunulia masafuria,sahani ,vikombe na vyakula kama mchele,maharage,kuku kwa ajili hiyo , hii ni kutokana kushindwa kumudu vyakula vya kihindi kutonakana na pilipili,sehemu za malazi zenyewe zinaonekana kuna kunguni,chawa na pia hazina mpangilo mzuri wa uwekaji wa vitu ,kwani hakuna makabati hata ya kuwekea nguo na baadhi ya vitu vidogo vidogo,baadhi ya wagonjwa wameshindwa kukaa katika hostel hiyo na kuamua kutafuta nyingine ambayo ni nzuri inajulikana kwa jina la online suite Boomasandra area ,kwani wanapata chakula kizuri,na vyumba vina Tv na simu kwa ajili ya mawasiliano,kwa mujibu wa wagonjwa hostel zote hizo ziko karibu.
Wagonjwa wamelalama pia inakuaje wanaambiwa wamelipiwa matibabu,na kwamba hata wao wenyewe waliambiwa wachangine kiasi Fulani cha fedha? Kulingana na uwezo wa mgojwa aliokuwa nao? Na pia wameshtushwa sana na wao kutopewa risiti wakati wa malipo na kudai kuwa malipo waliyafanya kwa mwenyekiti wa lions club bw yusuph Dalali , Gents corner DTV round about ambako ndio duka lake la nguo/vitambaa lipo,na pia wameshtushwa na uwepo wao Bangalore India ,bila ya ubalozi wao wa Tanzania New Delhi kufaham? Na je kama mabomu yaliyojitokeza maeneo ya madiwala market ,ambapo ni umbali wa kilomita 17 kutoka eneo walipo yangeweza kutokea eneo la hospitali ingekuwaje?
Baadhi ya wagonjwa wamshtushwa pia kutokumjua mkuu wao wa msafara Dr Ally mapema ,kwani wameanza kumjulia Nairobi wakati wakibadilisha ndege ya Kenya air ways ya kwenda Bombay,na wengine kumjua kwamba yeye ndio mkuu wa msafara walipofika Narayana hospital,India.
Wagonjwa hao wamewashukuru wanafunzi wa Kitanzania wanaosoma Bangalore University,India waliotembelea katika hostel wanazo kaa na kujionea hali ilivyo na pia kuwasaidia kutambulika ubalozi wa Tanzania New Delhi India.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari mbalimbali ni kuwa wagonjwa hao wanategemea kuwasili nyumbani Tanzania siku ya jumatano saa tisa mchana wakitokea Bombay India kupitia Nairobi ,kwa shirika la ndege ya Kenya airways.
Maoni yangu:
Kazi kweli kweli......malipo yamefanywa dukani kwa mdosi tena bila risiti,malazi walioandaliwa machafu kiasi kwamba wangepata maambukizo mengine ya magonjwa,fedha wamelipa huduma hawajapata(zimeliwa?)........ni ufisadi juu ya ufisadi sasa tutaanza kuona umuhimu wa THI......
Source:http://kamerayangu.blogspot.com/ huyu kijana yuko nchini India kwa hiyo kaandika aliyoyaona.

Last edited: