Naendelea kujifunza namna ya kukabiliana vema na matatizo kila siku ya kimaisha ambayo hakuna mtu anayeweza kuyazuia kama ili kufiwa na mtu wa karibu. Katika kipindi hiki kigumu kwangu nina jaribu sana kuruhusu fikira zenye kunipa furaha kuingia katika mfumo wangu mkuu wa kufikiri maana taarifa ya msiba wa niliyekua nampenda sana imeutikisa mwili wangu wa hisia.
Mama hakuugua kwa muda mrefu au kakuwa na magonjwa ya hatari, Baba akanipigia simu na kunijulisha kuwa tulipokua katika kusali asubuhi kama ilivyo kwaida yetu, mama yako akaniambia ''Nakwenda nyumbani''. Kisha akayafumba macho yake, baada ya kupelekwa Hospitali, daktari wa zamu baada ya kumpima akatoa ripoti ya kuwa amefariki.
Asubuhi ninasafiri na watu wa familia yangu wasiopungua 7, ''All eyes on me''. Taarifa hizi za msiba zimenijia kipindi ambacho nina tatizo la kifedha ndiyo maana nikasema ''michango inakaribishwa''.
Pia napenda kutumia nafasi hii kuwashukuru wale wote ambao wamenitumia jumbe za kunitia moyo na watakao fanya hivyo baadaye.