Taarifa ya Mh.Godbless Lema bungeni. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taarifa ya Mh.Godbless Lema bungeni.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by apolycaripto, Feb 12, 2011.

 1. apolycaripto

  apolycaripto JF-Expert Member

  #1
  Feb 12, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 633
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Hii kweli siasa!Lema amekuwa mbumbu akidhani taarifa atakayowasilisha bungeni kulingana na maagizo ya Spika itamnusuru kwa Waziri Mkuu kuonekana kweli kadanganya Bunge na wananchi.Lema hatokuwa na cha ziada mbali na taarifa ileile iliyofahamika kama “Tamko la Chadema” juu ya Mauaji Arusha ambayo imekwisha tolewa na Viongozi wa Chadema na kutaka Nahodha na Mwema kujiuzuru.Mambo yatakuwa kama ifuatavyo:

  1)Lema atawasilisha utetezi wake ambao nadhani hautakuwa na jipya mbali ya yale tuliyoyasikia katika media na wengine kujionea.Hapa msingi mkuu wa Lema itakuwa kusisitiza kuwa ilikuwa haki ya kikatiba chadema kuandama na kwa kuwa ilikuwa imekubalika na Kamanda wa Polisi Wilaya ya Arusha.Hapa kosa la Polisi ni kuuwa Raia japo mpaka sasa haijajibiwa kama wenzetu waliuwawa kabla ya kutolewa amri na Viongozi wa Chadema kwa wafuasi kwenda kuwakomboa Lema na wenzie ama baada ya kauli hiyo ya ukombozi.

  2)Upande wa Serikali ni dhahiri sababu zao zimekwisha tolewa kuwa maandamano yalikuwa haramu isipokuwa mkutano ulikuwa halali kutokana na kauli ya IGP Mwema kabla ya kikao cha tarehe 5/1/2011.Polisi walilazimika kutumia nguvu pindi Chadema walipolazimisha maandamano na matukio ya vifo vya wenzetu yalitokana na uchochezi wa Viongozi wa Chadema hasa baada ya kuamuru Lema na wenzie wawe wamekombolewa kutoka katika kituo cha Polisi na kufikishwa katika viwanja vya Unga Ltd ndani ya saa moja.Polisi walitumia risasi kama “final resolution” baada ya kuona wanazidiwa nguvu na vijana wa Chadema waliokuwa na “munkari” wa hali ya juu wakitaka kuvamia kituo chenye silaha lukuki.Ni dhahiri hapa ndipo serikali inasema “bahati mbaya” wenzetu watatu waliuwawa.


  Bungeni huu ni mtego tu ili haki ionekane kutendeka na Lema ameadhibiwa kwa kufungiwa kuhudhuria vikao visivyopungua vitano bungeni na kulazimika kufuta kauli yake.Na imani kwa bunge ninaloliona mchango wa kile atakacho kiwasilisha Lema uta kuwa ule wa Mudhihir na Zitto kabwe.Lema ata kama anadhani utetezi wake utakuwa “extraordinary” asitarajie maamuzi yatam-favour.

  Hii kweli siasa!

  Nionavyo mimi hatima ya suala hili ni pale tutakapo pata jibu la kuku na yai kipi kilitangulia?.
   
 2. kipindupindu

  kipindupindu JF-Expert Member

  #2
  Feb 12, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 1,051
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Alipohojiwa na waandishi,lema alisema asingependa kuongelea suala hilo ili asidhoofishe ushahidi wake.lazima ana kitu kipya.
   
 3. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #3
  Feb 12, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mimi nadhani katika hili Makinda hakuonyesha ukomavu wa kisiasa; swali lililoulizwa na Mbowe lilimpa mh. Pinda fursa nzuri kuisafisha serikali dhidi ya sakata la mauaji ya Arusha. Na Pinda alikuwa ameitumia fursa hiyo vizuri sana, Hivyo Makinda amemtifulia Pinda kwa kuzua jambo hilo upya. Mimi naamini ushahidi wa kudhibitisha ya kuwa ukweli wa mambo ni tofauti va alivyoeleza Pinda upo, na bila shaka Lema atahuwasilisha. Serikali kwa kutumia wingi wa wabunge wake inaweza hisitilia maanani ushahidi huo na ikala njama za kumuadhibu Mlema; ikifanya hivyo itakuwa imejidhohofisha na kumjengea umaarufu mlema
   
 4. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #4
  Feb 12, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,153
  Likes Received: 844
  Trophy Points: 280
  ...Mbona mimi nilivyoelewa ni kwamba uongo wa Pinda ni jinsi alivyoelezea kiini cha matatizo ya arusha ambayo kimsingi ni upatikanaji wa meya wa Arusha..mauaji ni matokeo ya upatikanaji wa meya + kukamatwa kwa viongozi na kudhuiliwa licha ya wana sheria kutimiza hatua zote za kisheria juu ya kuwawekea mdhamana.
   
 5. Kishongo

  Kishongo JF-Expert Member

  #5
  Feb 12, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hana jipya.

  Lema bado ni kinda kisiasa. Anadhani siasa zinaendeshwa kihuni.

  Semina aliyohudhuria Ubungo ilikuwa bure, pesa za serikali zilipotea pale.

  Bila shaka upeo wake ulivyo unatokana na elimu yake pamoja na malezi aliyopewa na chama chake.

  Hatuna cha kufanya, machalii wa Arusha wamemchagua.

  Hata hivyo bado kidogo tu watatambua kuwa imekula kwao - ni hasara ya miaka 5.
   
 6. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #6
  Feb 12, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,909
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 145
  acha dharau kwa umma wa arusha.ni lema huyuhuyu kupitia NCCR alimpeleka puta Felix mrema katika uchaguzi wa 2005.sasa uzoefu wa siasa si tatizo kwake.
  He is aggressive because he experienced the problems of arusha residents.the issue is not uzoefu wa siasa but to represent and present matarajio ya waliokuchagua.
   
 7. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #7
  Feb 12, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,176
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Crashwise hat mimi ndivyo nilivyoelewa lakini nashangaa watu wamejikita kwenye vurugu za 05.01.2011.
   
 8. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #8
  Feb 12, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,153
  Likes Received: 844
  Trophy Points: 280
  uzoefu upi unauzungumzia, Nyerere wakati anachukua nchi alikuwa na uzoefu upi?
   
 9. Kishongo

  Kishongo JF-Expert Member

  #9
  Feb 12, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nyerere alikuwa amekwenda shule.
  Ni mtu aliyekuwa anaona mbali na kupanga mikakati sawia - dunia ni mashahidi.
  Kumlinganisha Nyerere na Lema ni tusi kubwa...kwa Mwalimu mwenyewe na kwa WaTz.

  Ukweli ni kwamba Lema na majority ya viongozi wa cdm ni immature kisiasa. They are just political opportunists.
  Bahati mbaya ni kwamba mashabiki wao watakuja kugundua hili wakati imeshakula kwao.
   
 10. Kishongo

  Kishongo JF-Expert Member

  #10
  Feb 12, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Jipe moyo lakini mmechagua garasha safari hii.
  Lema hajui siasa, mbaya zaidi hakwenda shule, pia ana historia ya kuwa na kesi kesi zilizomchafulia jina hapo Arusha.
   
 11. peck

  peck JF-Expert Member

  #11
  Feb 12, 2011
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 204
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  NO NEED OF FAVOUR!!! We need no fovour but let the truth be true no matter what pain comes your way. LEMA BIG UP:clap2:
   
 12. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #12
  Feb 12, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 15,709
  Likes Received: 8,507
  Trophy Points: 280
  Ubongo wako umeathirika na maneno ya kiimla, "ukomavu ama ukinda" ni maneno ya kifisadi, yamechochea kutokuwaji
  Ka, yamepalilia rushwa na kulindana kwenye lichama lao,ni miongoni mwa vimisemo vilibuniwa kwenye chuo cha propaganda kivukoni kwa lengo la kuwanyima nafasi watanzania kujihusisha na siasa, kwa taarifa yako nasisitiza pinda amelidanganya bunge na wenyenchi, kasema walikufa watanzania watatu,ukweli walikufa watanzania wawili, huo ni uongo wa kwanza, pm hajui thamani ya raia kwenye nchi yake, kwa vimaneno vya "ukomavu wa kisiasa" ameshindwa na hawezi kujua kukamata viongozi wa wananchi kwa staili ile ni kuwa-provoke wananchi usitegemee watu wasifanye jaribio au jitihada zozote, jeshi la polisi liliwaalika wananchi kwenda kituo cha polisi pale walipomshikilia kiongozi anayependwa na wananchi bila kuyasoma mazingira. Kwa taarifa yako hakuna atakayemng'oa GL kwa uchaguzi wowote pale A town.
   
 13. Kishongo

  Kishongo JF-Expert Member

  #13
  Feb 12, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hakusema Watanzania watatu, alisema watu watatu. Hata kama alikosea na kusema Watanzania watatu, hiyo si hoja kubwa ya kumfanya Mbunge amuite PM muongo. Wabunge wote walifundishwa namna ya kuongea Bungeni kwenyue semina pale Ubungo. Hata hivyo kwa kuwa baadhi ya watu ni wazito wa kuelewa mambo ya kawaida, na kutokana na watu hao kujazwa itikadi za kipuuzi za kichama, maneno ya kashfa yameshuhudiwa bungeni.
   
 14. Nsiande

  Nsiande JF-Expert Member

  #14
  Feb 12, 2011
  Joined: Jul 27, 2009
  Messages: 1,649
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Garasha ...?? Garasaha! Huh ? Garasha ! What ?

  People decided to see beyond his cases and other inabilities, infact people and not just one or two..but multitude of people of Arusha..the wise included..chose him to represent them..

  they looked beyond his human flaws ..who are you to judge them ? During campaign session..alirushiwa madongo mazito,mengine ya kweli mengine ya uongo..guess what ???

  we voted FULLY AWARE of the person we are bringing foward to represent us....!! Oh yes ! Even me who is struggling with my PhD ! I knew for a fact his level of education, don't u doubt that for one second..

  Pity are those who chose Rostam blindly!

  Kishongo....u gat a long way to go !!

  In the people's open court of opinions and options...Mr Lema is the best thing in Arusha since bread and butter...

  Copy and paste that please.
   
 15. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #15
  Feb 12, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Sasa wewe kipi kinakuuma kama siyo Mshabiki wa CDM
   
 16. c

  carefree JF-Expert Member

  #16
  Feb 12, 2011
  Joined: Dec 19, 2010
  Messages: 265
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Tumemchagua tukijua anajua kusoma na kuandika , uwezo wake kuchambua mambo magumu kama quadratic equation tutayapeleka kwa wataalam , jamaa yeye anajua msoto tunaokabiliana nao ndiyo tuliyomtuma akaseme , tunataka utawala wa sheria hilo ameamza kulitatua , barabara finyu , mji wa kimataifa mchafu na mengine mengi ambayo tunahakika msela anamudu
  Batilda anamjua zaidi lema kama anapitaga humu aweke wasifu wake
   
 17. MwanaCBE

  MwanaCBE JF-Expert Member

  #17
  Feb 12, 2011
  Joined: Sep 23, 2009
  Messages: 1,774
  Likes Received: 533
  Trophy Points: 280
  Jifariji tu. Chadema ndo sauti ya watanzania wazalendo wa sasa na baadae.
   
 18. Kishongo

  Kishongo JF-Expert Member

  #18
  Feb 12, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  I have no guts to vote for a character with such a terrible criminal record to represent me. It is hard to believe that some people can be so blind and do so!

  Time will tell, soon you will realise where you went wrong.
   
 19. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #19
  Feb 12, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Chenge ALIUA na sasa yuko Mjengoni na ana Ujiko Kwenye CCM yenu
   
 20. Kishongo

  Kishongo JF-Expert Member

  #20
  Feb 12, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Atasimamiaje utawala wa sheria wakati yeye ana rekodi mbaya ya kihalifu?
   
Loading...