Tambara Bovu
JF-Expert Member
- Dec 19, 2007
- 585
- 140
Hapa Spika alishachemsha na kwa hatua yeyote itakayofuata itamsafishia njia Lema na CDM.hii ni nafasi nzuri ya ukweli kuwa wazi ili hata wale walioshindwa kusikia basi wasikie na kuelewa.
Kutoa mawazo si kiburi.
Ongelea hoja, kama Lema hana elimu ya kutosha tusiseme?
Mtazamo wangu nakuona kishongo hufikirii vizuri,na kama unafikiria basi ni kinyume,hivi wewe huoni kama PM alijibu lile jibu kisiasa? Unajua fika wenzetu wamekufa kwa uzembe wa polisi?Hivi polisi yetu ingepelekwa tunisia au misri kutuliza maadamano ingeua watu wangapi? Polisi arusha walitumia nguvu zaidi kutokana na maelekezo ya dola,tumeona nchi mbalimbali zenye polisi wenye maarifa wanavyopambana na waandamanaji ambao ni hatari na wanafaulu kuwatulizaHana jipya.
Lema bado ni kinda kisiasa. Anadhani siasa zinaendeshwa kihuni.
Semina aliyohudhuria Ubungo ilikuwa bure, pesa za serikali zilipotea pale.
Bila shaka upeo wake ulivyo unatokana na elimu yake pamoja na malezi aliyopewa na chama chake.
Hatuna cha kufanya, machalii wa Arusha wamemchagua.
Hata hivyo bado kidogo tu watatambua kuwa imekula kwao - ni hasara ya miaka 5.
Unatumia basis ipi kusema hawezi kufanya alichoanzisha. take it from me Last week tayari wanafunzi zaidi ya 500 walikuwa wameshajaza fomu za kusaidiwa na mfuko tayari umeshachangiwa mamilioni ya hela na wapiga kura wapenda maendeleo wa Arusha na mimi ni shahidi kwani tumekuwa tukifanya very close follow up. Mfuko ni well coordinated na kama unabisha nenda ofisi ya Mbunge wa arusha iliyoko ofisi ya mkuu wa wilaya ya Arusha. Batilda asingeweza haya kwani alikuwa anatafuta ubunge kama ngazi ya kuwa waziri na hiyo ndiyo ilikuwa END GOAL YAKE TUU.
Nyerere alikuwa amekwenda shule.
Ni mtu aliyekuwa anaona mbali na kupanga mikakati sawia - dunia ni mashahidi.
Kumlinganisha Nyerere na Lema ni tusi kubwa...kwa Mwalimu mwenyewe na kwa WaTz.
Ukweli ni kwamba Lema na majority ya viongozi wa cdm ni immature kisiasa. They are just political opportunists.
Bahati mbaya ni kwamba mashabiki wao watakuja kugundua hili wakati imeshakula kwao.
M... Hivi polisi yetu ingepelekwa tunisia au misri kutuliza maadamano ingeua watu wangapi?.
Kama kweli wewe ni mdau kwenye huo mfuko utakuwa umeshasikia malalamiko kuwa 90% ya wanafunzi waliojaza fomu ni Wachagga na wanachama wa Chadema.
Ndiyo sera ya cdm kujenga matabaka ya kikabila na kichama?
Arusha kuna Wamasai, Waarusha, Wasonjo, Wameru nk nk. Kwa nini wao watengewe 10% tu?
Tunatilia shaka madhumuni ya kuanzisha mfuko huo.
heshima kwako Kishongo,
nimekusoma sana mkuu na kukufuatilia kwenye thread nyingi, unaonekana una chuki binafis na Chadema tena kubwa sana iliyoota mizizi moyoni mwako.
ningefurahi kama ungekuwa huru katika mawazo yako. Lakini unaonyesha ushabiki na kupenda chadema ikosee na kufa kabisa.
kwa taarifa yako viongozi wa Chadema ni makini na werevu kuliko ndg zako wapendwa wa ccm, unapowaponda viongozi wa chadema una maana wa ccm ndio makini??
kinachowasaidia watu kama nyie na ccm yenu ni ujinga na umasikini wa wa tz bt one day yes tutapata ukombozi wa kweli. Na Mnara wa Babeli lazima utaanguka kwani hiyo ni saturation point yao na imekaribia.
nitafurahi sana kama utakuwa mjenga nchi na sio kuishambulia Chadema hata kama wana haki(kama hii isu ya Arusha) una tuaminisha wengi kwamba wewe na wenzako mnatumiwa au kununuliwa muharibu muv za kimapinduzi na kimageuzi.
we mwenyewe mbaguzi unaposema elimu ya Lema ndogo hastahili kuchaguliwa.Lete ushahidi wa allegations zako usiendeshwe na hisia.Naona mmeongezwa idadi kwenye kitengo cha propaganda.
duh sasa wewe mwenye elimu mbona umeshindwa kutambua kuwa kama kigezo cha kuwa mbunge ni elimu basi wengi wasinge kuwa wabunge.Ndugu yetu Lameck Airo(mbunge CCM) mbona anaelimu ya darasa la saba na anawatumikia watu na ni mmiliki wa mahotel makubwa tu ya LAKAIRO.Usiwe mbaguzi wa elimu leo umeanza elimu kesho itakuwa dini,jinsia kesho kutwa rangi.
Angalia cv yake ndio ushahidi.
Hii kweli siasa!Lema amekuwa mbumbu akidhani taarifa atakayowasilisha bungeni kulingana na maagizo ya Spika itamnusuru kwa Waziri Mkuu kuonekana kweli kadanganya Bunge na wananchi.Lema hatokuwa na cha ziada mbali na taarifa ileile iliyofahamika kama Tamko la Chadema juu ya Mauaji Arusha ambayo imekwisha tolewa na Viongozi wa Chadema na kutaka Nahodha na Mwema kujiuzuru.Mambo yatakuwa kama ifuatavyo:
1)Lema atawasilisha utetezi wake ambao nadhani hautakuwa na jipya mbali ya yale tuliyoyasikia katika media na wengine kujionea.Hapa msingi mkuu wa Lema itakuwa kusisitiza kuwa ilikuwa haki ya kikatiba chadema kuandama na kwa kuwa ilikuwa imekubalika na Kamanda wa Polisi Wilaya ya Arusha.Hapa kosa la Polisi ni kuuwa Raia japo mpaka sasa haijajibiwa kama wenzetu waliuwawa kabla ya kutolewa amri na Viongozi wa Chadema kwa wafuasi kwenda kuwakomboa Lema na wenzie ama baada ya kauli hiyo ya ukombozi.
2)Upande wa Serikali ni dhahiri sababu zao zimekwisha tolewa kuwa maandamano yalikuwa haramu isipokuwa mkutano ulikuwa halali kutokana na kauli ya IGP Mwema kabla ya kikao cha tarehe 5/1/2011.Polisi walilazimika kutumia nguvu pindi Chadema walipolazimisha maandamano na matukio ya vifo vya wenzetu yalitokana na uchochezi wa Viongozi wa Chadema hasa baada ya kuamuru Lema na wenzie wawe wamekombolewa kutoka katika kituo cha Polisi na kufikishwa katika viwanja vya Unga Ltd ndani ya saa moja.Polisi walitumia risasi kama final resolution baada ya kuona wanazidiwa nguvu na vijana wa Chadema waliokuwa na munkari wa hali ya juu wakitaka kuvamia kituo chenye silaha lukuki.Ni dhahiri hapa ndipo serikali inasema bahati mbaya wenzetu watatu waliuwawa.
Bungeni huu ni mtego tu ili haki ionekane kutendeka na Lema ameadhibiwa kwa kufungiwa kuhudhuria vikao visivyopungua vitano bungeni na kulazimika kufuta kauli yake.Na imani kwa bunge ninaloliona mchango wa kile atakacho kiwasilisha Lema uta kuwa ule wa Mudhihir na Zitto kabwe.Lema ata kama anadhani utetezi wake utakuwa extraordinary asitarajie maamuzi yatam-favour.
Hii kweli siasa!
Nionavyo mimi hatima ya suala hili ni pale tutakapo pata jibu la kuku na yai kipi kilitangulia?.
Hana jipya.
Lema bado ni kinda kisiasa. Anadhani siasa zinaendeshwa kihuni.
Semina aliyohudhuria Ubungo ilikuwa bure, pesa za serikali zilipotea pale.
Bila shaka upeo wake ulivyo unatokana na elimu yake pamoja na malezi aliyopewa na chama chake.
Hatuna cha kufanya, machalii wa Arusha wamemchagua.
Hata hivyo bado kidogo tu watatambua kuwa imekula kwao - ni hasara ya miaka 5.
Sijasema kuwa elimu yake haimruhusu kuwa bungeni, la hasha, anastahili kuwepo kama walivyo profesa Maji M,arefu na Airo uliyemtaja.
Nilichosema ni kwamba elimu yake na malezi yake ya kisiasa (siasa za cdm) yanamfanya afanye vituko vya kipuuzi bungeni.
Sijasema kuwa elimu yake haimruhusu kuwa bungeni, la hasha, anastahili kuwepo kama walivyo profesa Maji M,arefu na Airo uliyemtaja.
Nilichosema ni kwamba elimu yake na malezi yake ya kisiasa (siasa za cdm) yanamfanya afanye vituko vya kipuuzi bungeni.
Ni kichaa atakae subutu kumlinganisha Nyerere na kiongozi yoyote wa hapa Tanzania....Nyerere alikuwa amekwenda shule.
Ni mtu aliyekuwa anaona mbali na kupanga mikakati sawia - dunia ni mashahidi.
Kumlinganisha Nyerere na Lema ni tusi kubwa...kwa Mwalimu mwenyewe na kwa WaTz.
Ukweli ni kwamba Lema na majority ya viongozi wa cdm ni immature kisiasa. They are just political opportunists.
Bahati mbaya ni kwamba mashabiki wao watakuja kugundua hili wakati imeshakula kwao.