Taarifa ya kifo cha wazazi wangu

Ndugu wa JF, Salaam,

Nasikitika kuwafahamisha kuwa wazazi wangu usiku wa kuamkia tarehe 2 May 2011 walivamiwa na majambazi wasiojulikana WAKAWAUA WAZAZI wangu wote kwa kuwachoma visu huko Muganza, Rulenge, Ngara.

Nimasikitiko makubwa sana.

Pole sana.Mungu akutie nguvu.
 
Pole sana Mungu akupe moyo wa uvumilivu na nguvu katika kipindi hiki kigumu. Anayefariji ni Mungu pekee, pia tumia muda wako mwingi kutafakari neno la Mungu. Itakusaidia sana.
 
Duh! Pole sana mkuu kwa msiba mzito sana. Mungu awafariji katika wakati huu mgumu. Jamani, hii nchi yetu sijui inaelekea wapi. Ubinadamu hakuna kabisa siku hizi.
 
Ndugu wa JF, Salaam,

Nasikitika kuwafahamisha kuwa wazazi wangu usiku wa kuamkia tarehe 2 May 2011 walivamiwa na majambazi wasiojulikana WAKAWAUA WAZAZI wangu wote kwa kuwachoma visu huko Muganza, Rulenge, Ngara.

Nimasikitiko makubwa sana.

Mungu wetu na akupe faraja wewe na ndugu zako kipindi hiki kigumu kwenu.
 
Pole sana mpendwa! Mungu akupe faraja na ujasiri ktk kipindi hiki kigumu cha kupoteza baba na mama kwa namna ya kikatili mno! May the Lord give them eternity Peace!
 
Laaaaa! Sijui hii nchi ye2 inaelekea wapi!!! Laaa Pole sana ndugu yangu, namwomba mwenyezi Mungu akupe moyo wa uvumilivu kwenye kipindi hiki kigumu.
 
Kwa kweli ni kifo cha kinyama, nilikua huko kikazi na nilihudhuria mazishi nilichokisikia na kukiona siwezi kukiandika hapa ni kifo cha kinyamaa sehemu za siri walizikata na kuziweka puani na mengine mabaya zaidi jamani acheni tu wale jamaa ni wanyama kabisa pole sana bro.

Kuna tatizo la msingi sana ile sehemu ni mpakani na burundi majambazi wote wanakuja kupitia njia ile na hali ya ulinzi kwa upande wa kule sio nzuri serikali haijawekeza vizuri katika usalama wa raia

RIP your parents
 
Innalillah wainailaih rajiuun,

nimasikitiko makubwa sana.

Pole sana ndugu yangu wote tutakufa tarehe ya kufa tu ndio tufauti.
 
Back
Top Bottom