misskijiji
Member
- Feb 23, 2023
- 27
- 72
Naandika kwa uchungu sana Ndugu zangu wa Jamii Forums.
Mimi ni mdada mjasiriamali mdogo ambaye nimepambana kutafuta Ajira baada ya kumaliza Degree yangu 2021 bila mafanikio.Kupitia biashara zangu ndogongodo,nimefanikiwa kuwajengea nyumba ndogo ya vyumba viwili Wazazi wangu huko Kijijini kwetu Ikungi, Singida.
Kwa kuwa umeme bado haujafika, niliwatumia Pesa Wazee wangu mwezi Januari mwaka huu ili wakakope Sola ya Kampuni ya MYSOL ili wapate mwanga. Walienda ofisini kwao wakiongozana na mdogo wangu wa Kidato cha Nne, wakajaza Fomu zao na kulipa malipo ya awali ya shilingi 220,000 tarehe 11 Januari 2023. Hivi ninavyoandika, leo ni tarehe 20 Machi na hao wahusika wa Kampuni hawajawahi kwenda kuifunga Sola hiyo nyumbani kama makubaliano yalivyo.
Kila nikiwapigia simu ni danadana na sasa wameni-block kabisa. Jitihada za kwenda ofisini kwao mara kwa mara nazo hazijazaa matunda. Na ikumbukwe kutoka Kijijini kwetu mpaka Mjini kwenye Ofisi zao ni kilometa 278 hivyo mtu hawezi kwenda kufuatilia kila siku hasa ukitilia maanani Wazazi wangu ni wazee.
Niliwasiliana na Kituo cha Polisi Ikungi nao wamenijibu kwamba hiyo si Kesi ya Jinai ni Kesi ya Madai hivyo hawawezi kushughulikia. Naomba msaada kwa anayejua jinsi ya kutatua tatizo hili ili wanirudishie Pesa yangu.
Na pia nawapa ANGALIZO NA ONYO Watanzania wenzangu hasa wa vijijini kuiogopa Kampuni hii ya Sola ya MYSOL ambayo zamani ilikuwa inaitwa MOBISOL maana ni MATAPELI NA MAJAMBAZI WAKUBWA.
Nitashukuru Sana Kwa Msaada wa Ushauri nitakaopata.
ASANTENI Ndugu zangu, MBARIKIWE sana