Taarifa ya diwani wa Igoma dhidi ya sakata la umeya jijini Mwanza na mbunge Wenje

TAARIFA KWA UMMA WA TANZANIA NA VYOMBO VYA USIMAMIZI WA SHERIA ZA NCHI.

Naomba nitumie fursa hii kutoa ufafanuzi wa taarifa zilizojiri kwenye kikao cha baraza la Madiwani tarehe 15/05/2012 la Halmashauri ya Jiji la Mwanza na hujuma na uonevu ninazofanyiwa mimi Chagulani Adams Iblahim diwani wa Kata ya Igoma kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Nyamagana Ezekia Dibogo Wenje, kutokana na mchango wangu wa kutoa mawazo nilioufanya tarehe tajwa hapo juu ya kusema Mstahiki Meya Josephat Manyere kuwa sina imani naye, Hoja yangu ilisimama na kujikita katika vipengele vya kikanuni, Sheria na katiba ya nchi yetu.

SABABU ZA KUTOKUWA NA IMANI NA MSTAHIKI MEYA JOSEPHAT MANYERERE
1. Hajui majukumu yake na mamlaka yake kama Mwenyekiti na msimamizi mkuu wa shughuli za halmashauri ameshindwa kujua kuwa jukumu la kuitisha vikao na Mkurugenzi kazi yake ni kutoa taarifa kwa mujibu wa kanuni ya saba hivyo kutoa visingizio vya kushindwa kufanya vikao kuwa Mkurugenzi hajaitisha mikutano (vikao)ni kutojua jukumu lake.

2. Amevunja kanuni 77(1) – (2) kwa kutia saini lakiri ya utangazaji tenda bila idhini ya baraza hivyo kuingilia mamlaka na madaraka ya baraza la madiwani kwa kutangaza tenda kabla baraza halijaidhinisha. Alisaini sheria ya usafi (sharifu) ikaanza kutumika bila idhini ya baraza, pia utaifishaji wa shule ya msingi mbungani ulifanyika yeye kusaini bila idhini ya baraza la madiwani.

3. Ana upendeleo katika kusimamia ugawaji wa miradi ya maendeleo katika kata mbalimbali amekuwa akitumia nafasi yake kujilimbikizia miradi katani kwakwe yeye na Naibu wake mfano kata yangu mwaka wa fedha 2011/2012 ilipangiwa miradi takribani kumi na saba mpaka leo hii hakuna hata mradi mmoja uliofanyika kwenye kata yangu. Pia Bajeti ya 2012/13 kata yake amejitengea mradi wa kujenga barabara yenye urefu wa 0.5 kwa milioni sabini, huku kata yangu km 6 kwa 50 millioni hapa uwiano uko wapi km 6 kwa 50 milioni huku nusu kilometa kwa 70 milioni.

CHAGULANI ADAMS IBRAHIMU
DIWANI HALALI KATA YA IGOMA

Mawasiliano
Email: chagulaniadams@ymail.com
Simu: 0767 137831/ 0717 137831/ 0783 137831

Pamoja na kujitahidi kutoa maelezo marefu kama utetezi wako kwa jamii ya wana mwanza na watanzania kwa ujumla. inaonekana una mapungufu makubwa kama si hivyo basi unatumiwa na magamba, kama kweli mlikaa madiwani wa chadema na kukubaliana mtakachosema ktk baraza , na wewe ukaenda kuwasaliti basi hufai na hustahili, Kwa sababu kama ni mapungufu ya meya uliyajua kwanini usiyamalize ndani ya vikao vya chama kiwilaya/kimkoa hatimae kitaifa.
umedai wenje amekuwa anakusukia njama akuondoe, naona hilo ni bora zaidi , kuliko dai lako la kusema huna imani na na meya. sababu hiyo ni kudhoofisha peoples power, ukichamba sana mwishoe utashika mavi.
 
Mkuu bado unaisimamia hii kauli yako au umebadilika?
 
mkuu Ritz naona utaamini kuwa JF ni kisima cha habari ukiacha wachache wanaotaka kuichafua kwa vioja. Hii thread ilikuwepo muda na jamaa alitoa tuhuma dhidi ya Meya na kusema hana imani naye. Watu wakamdhihaki lakini leo hii Meya kang'olewa hivyo maneno ya Chagulani yametimia. Mkuu Invisible ungeunganisha hii thread na hiyo mpya ya MEya wa Jiji la Mwanza (CDM) ang'olewa kwa kuwa thread mpya ni mwendelezo tu wa hii.
 
Last edited by a moderator:
Na wewe chagulani nenda chama cha ADC ndio kinachokufaa kina wanafiki wenzako kina shibuda, zitto na Arfi....
 
Na wewe chagulani nenda chama cha ADC ndio kinachokufaa kina wanafiki wenzako kina shibuda, zitto na Arfi....
Sitaki kuamini wewe ni CHADEMA, huyu diwani ana hoja japo yawezekana zinakukera. Did you take trouble to read the whole 1st post?
 
Wanaotaka Diwani akae kimya ili kumlinda Meya wa chama chake sidhani kama wanajitambua. Sababu kubwa inayofanya ufisadi ushamiri ni kulindani kichama, kikanda, kikambi, kirafiki etc. Iwapo diwani amerikdhia kuwa meya hatendi haki kwa jamii halafu akakaa kimya ili kulinda maslahi ya chama, kutakuwa na manufaa gani kwa jamii?
Mtu anayedhani maslahi ya chama ni muhimu kuliko jamii ni sawa na mtu anayekata tawi la mti alilolikalia.
 
Napata mashaka namna ambavyo watu wanapinga ukweli humu ndani na baadae inakuwa aibu baada ya kuthibitika kuwa mtu alisema ni kweli .....hata kama tunaipenda Chadena lazima tukubali kukosolewa ili siku moja Chadema kiwe chama cha siasa na sio kiendelee kuwa Vugu vugu la msimu la mageuzi kutoka kaskazini mwa tanzania
 
mkuu Ritz naona utaamini kuwa JF ni kisima cha habari ukiacha wachache wanaotaka kuichafua kwa vioja. Hii thread ilikuwepo muda na jamaa alitoa tuhuma dhidi ya Meya na kusema hana imani naye. Watu wakamdhihaki lakini leo hii Meya kang'olewa hivyo maneno ya Chagulani yametimia. Mkuu Invisible ungeunganisha hii thread na hiyo mpya ya MEya wa Jiji la Mwanza (CDM) ang'olewa kwa kuwa thread mpya ni mwendelezo tu wa hii.

Mkuu Kimbunga nanyi muige kutoka Chadema, inapotokea kiongozi wenu ameshindwa kutimiza majukumu yake achukuliwe hatua mara moja.
Kila siku tunasikia viongozi mbalimbali wakilalamikiwa lakini chama chenu na serikali yenu iko kimya!
 
Last edited by a moderator:
Hapa sijaelewa.

Wenje alitataka waipinge Bajeti ya Chadema (Msaliti), Chagulani akaitetea waimalizie kisha waipigie kura mkutanoni (Mtetezi).

Chagulani alikosa imani na Meya wa Chadema (Msaliti!!),
Wenje akamtetea (Mtetezi).

Anyway, mwisho wa siku tumeona Meya ameondolewa.
 
Sera mpya migomo migomo hata kwenye bajeti uliyotengeneza mwenyewe

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Mkuu Kimbunga nanyi muige kutoka Chadema, inapotokea kiongozi wenu ameshindwa kutimiza majukumu yake achukuliwe hatua mara moja.
Kila siku tunasikia viongozi mbalimbali wakilalamikiwa lakini chama chenu na serikali yenu iko kimya!

Mkuu Mwita Maranya
Mbona sisi tukifanya hamumpongezi raisi?

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Mkuu Kimbunga nanyi muige kutoka Chadema, inapotokea kiongozi wenu ameshindwa kutimiza majukumu yake achukuliwe hatua mara moja.
Kila siku tunasikia viongozi mbalimbali wakilalamikiwa lakini chama chenu na serikali yenu iko kimya!
Mwita Maranya mimi napenda utaifa zaidi siyo vyama. Tatizo langu ilikuwa ni wakati ule Chagulani alipokuja na hoja hizi zaidi ya mia moja hapa JF watu wakamdhihaki lakini leo imeonekana Chagulani alikuwa akiitakia CDM mema! Nadhani hata TUNTEMEKE naye anaitakia CDM mema ila anazimwa tu kwa nguvu za ajabu.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom