Taarifa kwa umma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taarifa kwa umma

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Crashwise, Nov 3, 2011.

 1. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #1
  Nov 3, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  TAARIFA KWA UMMA
  TUKIO LA MHE GODBLESS LEMA (MB) KWENDA KWA RUMANDE KWA HIARI UJUMBE WA MSINGI WA KUZINGATIA.
  01 NOVEMBA 2011

  Ndugu wanahabari na Wananchi kwa ujumla,

  CHADEMA mkoa wa Arusha, imesikitishwa sana na utendaji kazi wa jeshi la polisi hususani OCD wa wilaya ya Arusha mjini. Katika kipindi na baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana OCD amekuwa akifanya kazi ya siasa kwa wazi wazi, mara nyingi tumekemea tabia hii na hata kutoa msimamo wa CHAMA kuwa huyu OCD ni chanzo cha migogoro yote hapa Arusha hivyo kuitaka mamlaka husika kuliangalia jambo hili na utendaji kazi wa OCD huyu.

  CHADEMA tumesikitishwa na tunaendelea kusikitishwa sana na double standard za jeshi la polisi hapa Arusha kwa kuendelea kufanya kazi kwa maelekezo ya kisiasa. Mtakumbuka Uvccm waliandamana na kufanya mkutano na maandamano ya zaidi ya saa nane, ambayo OCD huyu huyu aliyapiga marufuku, lakini kwa ajabu ndie aliyeyapa ulinzi kwa muda wote, ajabu zaidi ni pale Kaimu RPC aliponukuliwa akisema kuwa yale maandamano ni haramu ila jeshi la polisi litatoa ONYO kwa ccm.

  Walioandamana jeshi la polisi linatoa onyo na kwa CHADEMA ambao haijaandamana wanafunguliwa mashtaka,huu ni uhuni na uwendawazimu wa hali ya juu na kamwe hatutavumilia wala kukubali tabia hii ambayo ni hatari kwa usalama wa taifa.

  Kwa makusudi kabisa Ijumaa ya Tarehe 28, polisi alivamia ofisi ya Mbunge akiwa na zaidi ya polisi 80, kwenye magari matatu na kuanza kuwapiga,na kuwadhalilisha wapiga kura waliokuwa ofisini,tendo hili ovu lilifanyika kwa kisingizio kuwa kuna maandamano na mkutano, hatimaye hawa wananchi walifikishwa polisi na kufunguliwa mashtaka ya kuandamana bila kibali. Wengi wa waliokamatwa alikuwemo diwani wa CHADEMA kutoka DSM aliyekuja Arusha kwa safari yake binafsi na aliamua kwenda ofisini kwa mbunge kumsalimia. Mhe Azuri (Diwani) huyu akakutana na azama hii na sasa nae ana kesi mahakamani ya maandamano na kufanya mkutano wa hadhara, aibu tupu hii kwa jeshi la polisi kufanya kitendo hiki.

  Je wananchi kwenda kumwona Mbunge wao ni maandamano? Kutembea kutoka mahakamani nayo ni maandamano?

  Jumatatu tarehe 31.10.2011 wananchi pamoja na mbunge walifikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka ya kufanya mkutano kinyume cha sheria, hatimaye wapiga kura 19 walitoka kwa dhamana hadi 19 Novemba. Mbunge wa Arusha mjini alikataa dhamana kama njia ya kukataa uonevu, ukandamizaji,na dhuluma inayofanywa na polisi dhidi ya raia wema wa Arusha na Tanzania kwa ujumla.

  Kimsingi ni maamuzi magumu ila lazima yafanyike. Polisi wamekuwa na tabia na utamaduni wa kutisha wananchi,na kuwaogofya kuwa watawapeleka ndani(GEREZANI) kama vile gerezani ni adhabu kubwa sana.

  Mbunge Lema ameamua kwa hiari yake mwenyewe kutangulia CHADEMA tunatambua mbinu na mikakati yote inayofanywa na Serikali kwa kutumia polisi na usalama wa taifa mipango hii ina lengo la kukwamisha maendeleo ya Arusha, ili wananchi wakate tamaa na kuichukia CHADEMA, lakini pia kuna mipango michafu ya kuwabambikia Kesi viongozi wa CHADEMA pamoja na vijana na wanachama walio msitari wa mbele.

  Mtakumbuka kuwa waliwahi kumtuhumu mwenyekiti wa wilaya Mhe Ephata Nanyaro kwa tuhuma za kula njama za kuua, jaribio hilo ovu pamoja na mengine yameshindwa na hata haya nayo YAMESHINDWA.Na sisi tulio upande wa haki tutashinda.

  CHADEMA mkoa tunaupongeza ujasiri huu wa Mbunge wa Arusha mjini,na tunawataka wanachama wetu, wapenzi wetu na wananchi wote wa Arusha kuamka na kupinga dhuluma, uhuni, ukandamizaji na ukiukwaji huu wa sheria kwa vitendo. Ni wajibu wa kila mmoja mpenda haki kuungana nasi katika kipindi hiki.

  Kamwe tusikubali mtu mmoja OCD eti tu kwa kuwa ana polisi wenye silaha kututisha,au kutuogopesha. Hatuogopi wingi wa askari,au wingi wa silaha, kwani hakuna silaha itakayoweza kushindana na NGUVU YA UMMA.

  Hatuogopi silaha wala magereza na wakitaka waongeze silaha na kupanua magereza kwani tupo wengi majasiri ambao tupo tayari kupoteza chochote hata ikibidi uhai wetu ili haki na ukweli,na usawa upatikane.

  Tumeonewa vya kutosha tumenyanyaswa vya kutosha tumedhulumiwa vya kutosha tumekandamizwa vya kutosha na sasa tunasema HAPANA IMETOSHA. Vijana tuamke, Wanawake tuamke, wazee tuamke kwa ujumla wetu tuamke na tuipinge tabia hii ya jeshi la polisi ya kuwatia hofu wananchi na wanasiasa kwa kiasi cha kuleta mahusiano mabaya na dola hii muhimu.

  Nimalizie kwa kunukuu maneno ya mhe Godbless Lema (MB) katika waraka wake wakati akikataa dhamana, ameandika;

  "Wale mlionitishia kunipeleka jela sasa nimetangulia kwa hiari yangu na wale mliobaki msiogope jela endeleeni kupigania ukombozi utakaoleta usawa katika nchi yenu".


  Akamalizia kwa kusema kuwa;

  "Watakaotubeza na kututukana wasameheni kwani wanahitaji ukombozi wa fikra, watakaotupongeza na kutuonea huruma wafundisheni ujasiri na waambieni mapambano bado yanaendelea tunahitaji umoja wao. Nitarudi mapema. MSIOGOPE, MSIOGOPE, MSIOGOPE , MUNGU YUPO UPANDE WETU"


  Kwa tukio hili tunataka masuala ya msingi ya Arusha yashughulikiwe:

  1. Uonevu wenye nia ya kujenga hofu kwa wananchi, wanachama wa CHADEMA, Mbunge na viongozi wa chama – njama hizo zikome na jeshi lifanye kazi yake kwa haki.
  2. Suala la UMEYA – Haki ni msingi wa maendeleo. Dhambi iliyofanywa ya kumchagua MEYA wa CCM mhe Gaudence Lyimo kwa hila bila kufuata utaratibu itaitafuna Arusha na itakuwa kikwazo cha maendeleo. Haki ifuatwe na uchaguzi urudiwe. CHADEMA hatumtambui MEYA huyo.
  Tunawaomba wakazi wa Arusha na wanachama wetu wote waendelee kudumisha utulivu, umoja na amani vitu ambavyo ndivyo hasa tabia yetu na kamwe tusishiriki katika vurugu na tusiharibu mahusiano yetu na jeshi la polisi ambao tunawatarajia watafanya kazi zao kwa haki. Wakazi wa Arusha tufanye kazi na tujitume kwa bidii kwa maendeleo ya jimbo letu.
  Mungu Ibariki Arusha, Mungu Ibariki Tanzania.

  Amani Golugwa

  KATIBU WA CHAMA MKOA – ARUSHA.


   
 2. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #2
  Nov 3, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Mkubwa! Nakwambia hawa magamba kutumia nguvu ya dola kwa ajili ya sisiem yao,,,,,,,,,,,hakika wananchi na wapiga kura wa hapa Arusha mjini imewasikitisha sana,,,,,,,,!

  Na uzuri moja hata leo wakisema wanataka kurudia uchaguzi sisiem wamweke mtu na CDM waweke kivuli cha mtu,,,,nawahakikisheni KIVULI kitashinda kwa 100% na tangu jana nimeshasema ktk ID ya kwamba labda wafufuke wale waasisi wa TAA na TANU labda wanaweza wakaleta ukombozi wa hawa magamba hapa A town!

  Nitakachoweza kusema kwa sasa kama Mi mpiga kura wa hapa A town,,,,kwanza kbs huyu OCD aliyetuita raia PANYA nakwambieni yeye ametamka kama yeye lakini ajuwe kabisa ya kwmb hilo neno halitaenda bure hata punde na iko siku atajutia matamshi ya kinywa chake na huyu huyu OCD amezidi kuwa mchochezi, mtumia madaraka yake ktk hali ya siasa na siyo fani yake na kujenga chuki na raia wema wa Jiji la Arusha,,,,,

  Atajutia siku si nyingi kwanini alipewaga nafasi hiyo. Huyu amekuwa kichefuchefu hapa lakini hebu twendeni mbele kidogo tu kwn tutaona ujasiri wake uko wapi.........!!
   
 3. V

  Victim Member

  #3
  Nov 3, 2011
  Joined: Aug 15, 2010
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  This OCD was here in Arusha as the OC-CID abou 4-5 yrs ago as is known to many as a very corrupt person;getting involved with domestic problems and always harassing the husbands ( obvious why). Am sure there are many who will recall this guy Zuberi and can vouch for what I have said from experience.
   
 4. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #4
  Nov 3, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,421
  Likes Received: 435
  Trophy Points: 180
  akhsante sana katibu!
   
 5. DASA

  DASA JF-Expert Member

  #5
  Nov 3, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 1,031
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Yani mimi nikianza kuongelea huu unyanyasaji wa magamba na mapolisi, natamani kulia, lakini Ishalaah! ipo siku Mungu atajibu maombi yetu.

  Hongera Chadema Kwa kutuamsha kutoka usingizini. Kazeni buti, Mkikubali kulegea basi ndio tutakwisha kabisa na vizazi vyetu.

  Mi machozi yameshaanza kutoka!!!!. Naumia mie jamani.
   
 6. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #6
  Nov 3, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Umeongea kiingereza kigumu kiasi sijaelewa umeongea nini. Hizi lugha za watu ni wito.
   
 7. s

  saxzu Member

  #7
  Nov 3, 2011
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  tunashukuru sana katibu wa chama kwa taarifa wananchi wa Arusha tumezidi kuonewa na hawa panya ambao wanaishi maisha ya shida hadi mwisho(ndani ya mabati) alafu ndo viherere badala watulie ila tunawashukuru sababu wanatukomaza na sasa tunawaona ni watu wakaida na bomu wamelitengeneza wenyewe....Then Mheshimiwa ni hatua gani zinaweza kufatwa sababu Arumeru mashaniki ni sawa na hakuna mbunge then magamba wamenyamaza tu.
   
 8. s

  sem2708 JF-Expert Member

  #8
  Nov 3, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 3,093
  Likes Received: 505
  Trophy Points: 280

  Muammar Gaddafi Called The Rebels Rats and Was Cought In a Hole ! | NIGERIA ENTERTAINMENT | Top Nigeria Entertainment Site

  gadafi aliwaita waasi rats na amekamatwa kwenye shimo kama panya
   
 9. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #9
  Nov 3, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Craaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaap hakuna kitu hapa
   
 10. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #10
  Nov 3, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Craaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaap ! broken english
   
 11. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #11
  Nov 3, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  kachukue posho Nepi kashaona kazi yako....
   
 12. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #12
  Nov 3, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Kamfundishe mmeo nkwele kinglish...mwambie aongee kiswahili kama hawezi lugha, sio analeta vigugumizi kama beberu aliyenusa mkojo wa mbuzi jike.
   
 13. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #13
  Nov 3, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,143
  Trophy Points: 280
  Kwani lazima uandike kiingereza? au ndio tayari? maana wengine Kiingereza hupanda pale tu wanapokuwa ya 5.
   
 14. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #14
  Nov 3, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Basi muwe mnampa boss wenu mvinyo asiwe anapata kigugumizi akiwa anaongea na wanaume.
   
 15. DASA

  DASA JF-Expert Member

  #15
  Nov 3, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 1,031
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Ugonjwa gani huo unaokuwasha wewe!!!
   
 16. DASA

  DASA JF-Expert Member

  #16
  Nov 3, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 1,031
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  But msg SENT!
   
 17. DASA

  DASA JF-Expert Member

  #17
  Nov 3, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 1,031
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Unaongea nini wewe Ajuza!! Mbona upo nje ya Mada!! Loh!
   
 18. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #18
  Nov 3, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Mimi naamini na ninashuhudiwa moyoni mwangu kwamba uonevu wa dhahiri unaofanywa na ccm na vyombo vyake vya dola ni dalili kuwa siku za chama hiki kuwa madarakani zinahesabika. Mungu ninayemwamini lazima atatenda kile kitakachobatizwa jina la 'maajabu ya dunia' pale ambapo chama kilichokaa madarakani tangu uhuru kitakapong'olewa kwa nguvu ya umma.
   
 19. DASA

  DASA JF-Expert Member

  #19
  Nov 3, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 1,031
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Ni vile wanajifanya wagumu kusoma alama za nyakati!.
   
 20. F

  Fanfa JF-Expert Member

  #20
  Nov 3, 2011
  Joined: Sep 25, 2009
  Messages: 538
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ndio maana NEPI alikupitia
   
Loading...