Transistor
JF-Expert Member
- Aug 8, 2013
- 970
- 1,461
Heri ya mwaka mpya wakuu,
Taa za LED zimepata umaarufu miaka ya hivi karibuni kutokana na kuwa na mwanga mkubwa huku ulaji wake wa umeme ukiwa ni kidogo.
Licha ya faida hiyo kutokana na tafiti mbalimbali taa za LED,zimeonekana kuwa na madhara kiafya,licha ya wataalamu wanao unda taa hizi kuzidi kuziboresha,ili kuepukana na madhara hayo.
Mwaka 2016,shirika la kimarekani la American Medical Association(AMA),lilisema tekinolojia ya taa za LED,yana athari kwa afya ya binadamu.
Taa za LED zinazalisha mwanga wake kwa kutumia mawimbi mafupi,mawimbi haya yana kiasi cha nguvu ya juu cha miale ya blue na violet yaliyo katika kiwango cha kuonwa na jicho la binadamu.
Endapo macho ya binadamu yatazama mwanga huu huweza kuathirika kwa kiasi fulani katika uwezo wake wa kulala,mara kadhaa baadhi ya watu wamekuwa wakikumbwa na tatizo la kuwashwa macho ama kichwa kuuma baada ya kuwa katika mwanga wa taa za LED kwa muda mrefu.
Endapo mtu atakua katika mazingira haya ya mwanga wa taa za LED,basi miale ya blue inayozalishwa na mwanga wa taa hizi huweza kusababisha ugonjwa wa mtoto wa jicho (cataract) ,au tatizo la uoni hafifu (Macular degeneration).
Pia tafiti zinaonesha kuwa miale inayozalishwa na mwanga wa taa za LED,husababisha mabadiliko ya "retinal" katika jicho hata kwa matumizi ya muda mfupi tu ya taa hizi.
Tafiti ya mwaka 2014 ya shirika la afya ya mazingira inaonesha panya ambao waliwekwa katika mazingira ya taa za mwanga wa LED,walionekana kuathirika macho zaid dhidi ya wale waliowekwa katika vyanzo vya mwanga mwingine.
Watafiti wanashauri matumizi ya mwanga kuepuka matumizi ya mwanga mweupe hasa unaozalishwa na taa za LED,ambao una kiasi kikubwa cha miale ya blue,ambayo ni hatari kwa afya ya macho,na watumie taa za tubelight hasa sehemu za kupumzikia au sehemu ya kulala.
Wataalamu wanasisitiza kuwa macho ya binadamu yana uwezo wa kupambana na miale hii ya blue,lakini uwezo huu hutofautiana kati ya mtu na mtu kwa sababu za kimaumbile lakini pia sababu ya umri,ambapo watoto na watu wazima wapo katika hatari zaidi ya kudhurika na miale hii.
Taa hizi pia husababisha kichwa kuuma kwasababu huwaka na kuzima kwa kila hatua kwa asilimia 100,hii husababisha ubongo kufanya kazi kwa kasi zaidi wakati ukiutafsiri mwanga,kwa kifupi taa hizi hazifai kwa kusomea.wakati taa za kawaida za mwanga mweupe tubelight zenyewe huwaka na kuzima kwa asilimia 30 tu,hivyo hizi hua haziumizi kichwa.
Wataalam wanashauri kuzuiwa kwa miale ya blue katika taa hizi angalau kwa kiwango cha 415-455 nanometer kwa taa ambazo zinatumika majumbani.
Imeandaliwa na Transistor.